Ndani ya hii miaka mitano mambo mengi mno yamebadilika - kibaya zaidi hata waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari nao wameingia na uwoga.
Huwezi kujenga uchumi wa Taifa huru kama Raia ni waoga, Waandishi wa habari ni waoga, Watumishi wa umma ni waoga - Taifa la watu waoga.
Sidhani kuna kituo cha TV kitakachoonyesha Live mkutanowa Lissu !! hakipo kwa sasa.
Upande wa Lissu, katika upande wake kuna tatizo kidogo kuonesha mikutano yake mubashara kutokana na kauli zake katika kampeni zake. Hakika endapo wangerusha kauli zake bw. Lissu(Best Loser) ningesema kweli vyombo vyetu vinakiuka sheria na weledi wao.
Mambo yanayofanya T. Lissu vyombo vya habari visitangaze habari zake ni:
1. Utoaji wa matusi na udhalilishaji wa vyombo vya kiusalama.(Ambalo ni kosa kisheria).
2. Kuhubiri chuki badala ya umoja katika nchi.
3. Kutoa taarifa za kuleta vurugu kabla na baada ya uchaguzi " Kuingia barabarani"
4. Kumtuhumu Mh. Magufuli kwa mambo ambayo ni unprovable hata mwenyewe anashindwa Kuthibitisha hizo tuhuma zake(Defamation).
5. Kuzungumza Maneno ambayo yapo nje ya maadili ya kitanzania, kama kuzungumzia ushoga n.k
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.