Ushauri: Tuwe makini tunapoibatiza miradi majina ya viongozi wakuu wa kisiasa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,228
2,000
Natoa tu angalizo, si vizuri kuibatiza miradi majina makabwa ya viongozi wa kisiasa kabla hata performance ya miradi hiyo haijaanza kuonekana. Niwapongeze wasimamizi wa uwanja wetu wa taifa kwa kuusibirisha ukomae kwanza ndipo uje upate ubatizo wa maji mengi. Nawasilisha!
 
mtima nyongo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,953
2,000
wao wenyewe ndio wanavyopenda, muda si mrefu utasikia jpm international airport chato
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,965
2,000
Kupenda sifa kwingi ndani yake kuna ubinafsi, umimi, kiburi, majivuno, majigambo, dharau, kejeli, dhihaka, husda, roho mbaya na mengine mengi yafananayo na hayo; na kwa pamoja yanaweza kuwa summarized kwa neno moja tu MAUTI. Ndio maana tunaaswa tujikane na kuzikana nafsi zetu; tuwe wanyenyekevu kwa kumaanisha; walioshauri hivyo hawakuwa wajinga; ila sisi ndio tunajiona tuna akili kuliko wao!
 
Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,449
2,000
Natoa tu angalizo, si vizuri kuibatiza miradi majina makabwa ya viongozi wa kisiasa kabla hata performance ya miradi hiyo haijaanza kuonekana. Niwapongeze wasimamizi wa uwanja wetu wa taifa kwa kuusibirisha ukomae kwanza ndipo uje upate ubatizo wa maji mengi. Nawasilisha!
Hmmm, ole wao wangejenga halaf wasiziite Faru Jo...wangeisoma namba!
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Mkapa alifanya busara sana kwenye suala la noti na sarafu kwa sababu duh, leo sijui tungekuwa kwenye hali gani. Sijui ile sheria iliyoondoa uwezo wa Rais aliyepo madarakani kuweka picha zake kwenye noti na sarafu (kama ipo) inasemaje. Kama ipo nadhani ipanuliwe na kujumuisha kwamba ni MARUFUKU kitu chochote kupewa jina la kiongozi miaka isiyopungua 50 toka kustaafu kwake.

Marekani ambako nadhani tumeiga utaratibu huu, ingawa najua kuna nchi nyingi zinaufuata, hauwezi kuona barabara, shule, jengo nk vinapewa jina la kiongozi wakati bado yupo madarakani. Wana sheria zao, inapita miaka mingi sana, wakati mwingine hadi kiongozi amekufa ndiyo unasikia vitu vinakuwa named after them. Hii inasaidia viongozi kutotumia rasilimali za nchi vibaya. Kama kweli ulifanya mambo mazuri (na muda ndiyo hakimu mzuri), utakumbukwa tu, hata ndege za kivita zitapewa jina lako.

Tatizo hatuna viongozi wenye humility. Kikwete alinisikitisha 'kukubali' jengo lile la moyo la Muhimbili kupewa jina lake. Angekataa ningemkubali sana tu.
 
wamaukweli

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
997
2,000
Natoa tu angalizo, si vizuri kuibatiza miradi majina makabwa ya viongozi wa kisiasa kabla hata performance ya miradi hiyo haijaanza kuonekana. Niwapongeze wasimamizi wa uwanja wetu wa taifa kwa kuusibirisha ukomae kwanza ndipo uje upate ubatizo wa maji mengi. Nawasilisha!
Wanapenda kiki
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom