Ushauri tu: Anayekataa tumkatae

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
tunaweza kutoa ushauri kwa taasisi, serikali kwa ujumla, waziri, mkuu wa idara etc. Nadhani jambo jema ni kushauri ili ikifika 2020 wale tuliowapa dhamana tuwahoji huku tukiwakumbusha kuwa ushauri tulitoa na wenyewe pia tulijitolea kufikia malengo.
  1. Ushauri kwa serikali:
    1. Matumizi ya elimu na busara bado hajafikia kiwango tarajiwa!
      • Hii ni moja kati ya serikali za wasomi duniani, nadhani tunazizidi US, UK na Germany. idadi ya PhDs toka kwa raisi hadi wakuu wa idara na vitengo. hebu tunaomba kuona jinsi PhD zinavyoweza kulwta mabadiliko.
      • Hadi kesho utasikia malengo yenu ni kuwa kama serikali ya awamu ya kwanza, nadhani hii ni fedheha, sasa kuna wasomi wengi ukilinganisha na serikali ile ya mwalim! lkn pia dunia ya leo ni ya ukombozi wa kiuchumi na technolojia na sio juu ya kesi za mipaka na mambo ya ukoloni. badilisheni targets maana mtakuwa mna set too low!
    2. Mipango na utekelezaji
      • Awamu hii mmekuwa na mipango mingi, lkn hamtumpi vigezo tunavyopaswa kutumia ili tuwapime na nyinyi wenyewe mjipime!
      • shida za uchumi kwa wananchi mnatoa majibu mepesi ya kuwa wanaolalamika ni mafisadi, kukosekana kwa huduma mnasema mnajenga nchi, ajira mnajibu kuwa mnahakiki.
      • hebu leteni mipango ya muda mfupi 2-3 years, muda wa kati 5 - 10 years na muda mrefu beyond 10 years. mkitupa mchanganuo tutajua pa kuwauliza. lkn tupeni vigezo vya kuwapimia kwa kila hatua ktk maeneo yote mliyoainisha kuyafanyia kazi.
      • viwanda huu ni mpango wa category ipi? unaanzia wapi? lini?, elimu ipi? tunachkua hatua gani, ili tufikie wapi?
  2. Waziri wa fedha na mipango/ viwanda/Kilimo/waziri mkuu
    • ukitembelea masoko yetu ktk mwezi huu December unaweza kulia. masoko yamechafuliwa na matunda kama embe, mananasi na maparachichi na matikiti kidogo. matunda haya ikifika February tutayatafuta na kwa wachache watakaomudu itakuwa gharama kubwa. hadi sasa hatujaweza kutafuta suluhisho la huhifadhi wa matunda ktk taifa letu, kila zao la msimu huwa linaacha takataka lkn wiki kadhaa baada ya msimu kwisha, wananchi wanashindwa kumudu kupata hata mazao yale waliyotengenezea wenyewe pombe!
    • kabla ya kukamilisha ujenzi wa mji wa Dodoma na lile daraja la koko beach hebu jaribuni kupata wataalam watakaosaidia kusindika chakula. viwanda kwa ajili ya packaging na usafirishaji nje ya nchi.
  3. Wananchi
    • Tujitolee kufanya kazi kwa bidii. Juhudi zetu ndizo zitakuwa chachu ya maendeleo. tukifanya kazi kwa kushirikiana na serikali, then tutakuwa na haki ya kuhoji juu ya maendeleo maana tumejitoa kushiriki kila hatua. kinyume chake ni kushindwa kufikia malengo, endapo tutategemea watumishi wachache hasa wale wa juu wa serikali.

list inaweza kuendelea.
Nawe endeleza kwa kumshauri mtu/idara au serikali.....! (saa ya ukombozi ni sasa...Rev. Mtikila RIP)
 
2. NBS(takwimu) hivi karibuni imeimarika sana kwa nyalaka lukuki za tafiti mbali mbali. Ninaomba kwa waandishi wa vitabu wajitahidi kutumia taarifa hizo katika vitabu wanavyo andika sasa pia baadae. Inachukiza sana kuingia darasani wanafunzi wanafundishwa kwa mifano na takwimu za mataifa ya magharibi. Mfano mimi binafsi nasoma stashahada ya uchumi ila mifano yote ya "unemployment,inflation and production" ni takwimu za marekani, uchina na mataifa mengine ya ulaya. Na shida hususani ipo kwenye vitabu elekezi wanavyotoa. Mwisho siku wanahitimu ufanisi unakua mdogo, anapuuzia data hizo za mataifa mengine maana mtaani yana nafasi ndogo sana ya matumizi
 
2. NBS(takwimu) hivi karibuni imeimarika sana kwa nyalaka lukuki za tafiti mbali mbali. Ninaomba kwa waandishi wa vitabu wajitahidi kutumia taarifa hizo katika vitabu wanavyo andika sasa pia baadae. Inachukiza sana kuingia darasani wanafunzi wanafundishwa kwa mifano na takwimu za mataifa ya magharibi. Mfano mimi binafsi nasoma stashahada ya uchumi ila mifano yote ya "unemployment,inflation and production" ni takwimu za marekani, uchina na mataifa mengine ya ulaya. Na shida hususani ipo kwenye vitabu elekezi wanavyotoa. Mwisho siku wanahitimu ufanisi unakua mdogo, anapuuzia data hizo za mataifa mengine maana mtaani yana nafasi ndogo sana ya matumizi
Halafu wasomi wanatutangazia kuanza matumizi ya Kiswahili hadi chuo kikuu, wakati materials ktk archives zetu hawatumii!
Nadhani matumizi ya takwimu halisia za kwetu ni jambo la maana sana ili kujenga uelewa mpana Zaidi!
 
Back
Top Bottom