Ushauri: TRA waweke tozo na kuruhusu magari ya IT (in-transit) kubeba abiria

Marathon day

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
562
835
Ndugu zangu kutokana na wingi wa abiria wa usiku, na uchache wa mabasi yafanyayo safari mda wa usiku, kuepuka ajali kama ya Costa ya Morogoro jana, napendekeza TRA waweke tozo ya gari ndg (IT) kulipia tsh 30,000/; na gari Kama Noah tsh 50,000/ Costa tsh 80,000/; wapewe kibali kupakia abiria, badala kwenda Bure na kuacha abiria.

TRA Wangekusanya pesa nyingi ajabu, nijuavyo kwa siku Kun gari takribani 80+kwa siku, piga hesabu kwa mwezi na mwaka angekusanya kiasi gani? Sababu swala la kupakia abiria kwa it haliepukiki kutokana na wingi wa abiria, matokeo yake pesa hizi zinaishia kwa polisi barabarani.

Wote tunaona kinachoendelea. Kama inawezekana pick up kulipia C65 na kubeba mizigo kwa IT inashindikana nini kwa abiria? Polisi wasimamie mwendo Kasi na makosa mengine, la kupakia waliache kwa TRA, hakika tungeongeza MAPATO ya nchi yetu na kutoka kipato kwa vijana wetu.

Muheshimiwa Mwigulu liangalie hilo.
 
Wazo zuri lakini gari zile hazina bima, wala usalama wa kupakia abiria. Yakifika nchi husika hufanyia service upya, mfano matairi vipara na baadh ya viburi hakuna, inaweza kukuza ajali mara dufu mkuu.
 
Achaa police nao wapate pesa za Wageni hizo ili nao wajikimu,na pia itapunguza usumbufu kwa gari za ndani za Watanzania wenzao, ukiwabana sana police wa barabarani watakao umia sana ni Madereva,Bora waendelee kupokea za kubarashia kiwi viatu vyao!
 
Nimetoka kapa. Nilifikiri linaongelewa suala la magari yatolewayo bandarini, nakuta abiria wa usiku!
 
We unataka pesa zote ziliwe na wanasiasa pekee Acha police nao wale kupitia IT watu wanajenga, kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Swala la Abiria ni la Latra sio Tra.
Kwa sheria za latra hadi wanatoa kibali cha gari kupakia abiria , sio jambo dogo, kuna masharti mengi na makubaliano kadhaa na mmiliki wa chombo juu ya usalama wa abiria .
Hilo la gari za It kubeba abiria sidhani kama ni rahisi Latra kukubali.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom