Ushauri-TFF mechi ya Morocco iwe 10/10/10 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri-TFF mechi ya Morocco iwe 10/10/10

Discussion in 'Sports' started by Pengo, Oct 5, 2010.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu ni ushauri toka kwa Dr.Bruno Munufu aliyepo safarini uarabuni kwenda TFF,tafadhari wapange mechi kati ya Taifa Star na moroco ichezwe tarehe 10/10/10 kwani siku hiyo ndio haswa yenye bahati kwa watanzania.Mechi ikichezwa tarehe 10/10/10 tutawashinda waarabu kiurahisi sana lakini ikichezwa tarehe 9/10/10 hatutakuwa na ushindi zaidi ya sare ambayo bado haitatusaidia kitu.Kwa mujibu wa Dr.Munufu,hivi sasa waarabu wanahaha kuhakikisha mechi hiyo inachezwa tarehe 9/10/10 kwani wao ndio tarehe ya ushindi kwa mechi nyingi walizocheza tarehe hiyo.Wenyewe wanasema hivi "Tanzania inaanza na herufi ya T ambayo kwa herufi za alfabeti ni namba 20 wakati Moroco inaanza na herufi M ambayo kwa herufi ya alfabeti ni 13".Timu yenye nafasi kubwa ya kushinda mchezo ni ile ambayo herufi yake ya mwanzo ukajumlisha na tarehe ya mchezo jibu la jumla ni namba shufa(even number) na ile ambayo herufi ya mwanzo wake ukajumlisha na tarehe utapata jumla ya witiri(odd number) hiyo inanafasi kubwa ya kushindwa,ushindi wake ni sare.

  1).Mfano mechi ikichezwa tarehe 10/10/10
  .Tanzania(T=20 +10(siku ya mechi terehe 10) jumla =30 shufa(even)
  Moroco (M=13 + 10(siku ya mechi tarehe 10)jumla=23 witiri(odd)
  Kutokana na hapo (1)juu Tanzania ina jumla ya namba shufa(even) so Tanzania ina nafasi kubwa ya ushindi.

  2).Lakini mechi ikichezwa tarehe 9/10/10
  Tanzania(T=20 +9 jumla=29(witiri-odd)
  Moroco(M=13 + 9 jumla=22(shufa-even)
  Kutokana na hapo (2) juu Moroco ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania kwavile jumla ya namba zake ni shufaa(22).Kutokana na hayo Dr.Munufu amenambia nimuwakilishie ushauri wake kwa watanzania hasa wale waliopo karibu na Tafuna Fedha Faster(TFF) kwani jukumu la kupanga tarehe na siku ya mchezo ni la timu mwenyeji ambayo ni Tanzania.
  Tafadhari mjue kuwa haya ni mawazo ya Dr.Munufu aliyeniomba nimuwakilishie na si yangu binafsi mimi mzee wa S/Wanga.
   
 2. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waache vijana wafanye mazoezi wacheze soka.

  Kama wana uwezo watashinda, kama hawana hata wacheze tarehe 10 October, 2010 saa 10 dk 10 jioni, bado watachezea kichapo.

  It is time tuachane na hizi imani zinazoendekeza uvivu.
   
 3. a

  as me Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha hizo wewe kama ushindi upo upo tu, hata mechi ingechezwa cku isiyo na jina usituharibie wachezaji wetu kisaikolojia acha vijana wafanye kazi huko ndio kutafuta sababu na kuwatia uvivu, mwanamichezo bora hana hizo, goooo poulsen boys n make us shine like stars as ur the stars of the nation
   
 4. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nitamfikishia Dr.Munufu michango yenu
   
 5. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama wanaweza kucheza na shufwa na witiri,mbona wamehangaika sana kutafuta kocha,tena kutoka Ulaya! Tuachane na kutafuta sababu za nje ya uwanja,tukifungwa tuangalie performance ya timu siku hiyo(kulingana na falsafa aliyotutangazia ) na uwezo wa wachezaji wa wenzetu na si vinginevyo!
   
 6. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha imani za kichawi, mpira ni ufundi tu bila kujali unacheza lini. Hayo mambo ya Yahaya hayana nafasi karne hii. Na lazima ujue kwamba ratiba hizi zinapangwa na CAF/FIFA na sio TFF.
   
 7. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  CAF/FIFA wanapanga siku 3 za mchezo husika na TFF ndio wenye dhamana ya kuchagua siku ya mchezo kati ya Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.
   
 8. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Na mara nyingi timu za Uarabuni hupenda kucheza mechi zao ijumaa bila hata kujali kuwa siku hiyo itakuwa shufwa au witiri!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yani kuna watu bila uchawi hawawezi kuishi
   
 10. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna watu bila CCM hawawezi kupata ulaji!
   
Loading...