Story of Change Ushauri: TCRA wafanye nini kumaliza tatizo la wizi wa simu

Viprealestate

Senior Member
Jan 21, 2014
125
250
Kuna vitu ni vigumu kuvisahau kwenye maisha yangu, vipo vyenye kufurahisha na vile vyenye kuleta maumivu moyoni mwetu. Jambo la kushukuru ni namna Mungu ameweka kitu kusahau ili maisha yaendelee, Mungu wetu ana nguvu sana.

Mwaka 2019 ninaweza nikasahau matukio yote yaliyojiri mwaka huo lakini sio tukio lililopelekea kuwekwa mahabusu ya kituo cha Polisi kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu. Japokuwa limepita lakini ni tukio lililoacha kovu kubwa kwenye moyo wangu, naamini maumivu yake ni mimi peke yangu ninayaelewa.

Ijumaa, Kimara Michungwani.

Ni wakati ambao ndio kwanza nimefika nyumbani kutoka Kariakoo nilikoenda kununua vitu fulani ili nitume huko Mpito kijijini kwetu, macho yangu yakiwa makini kufuatilia kinachoendelea kwenye Tv ghafla simu yangu iliita na kama ilivyo ada nilishika kutazama ni nani, namba ilikuwa ngeni.

Nilishtushwa kuambiwa mdogo wangu yupo mahabusu huko kwetu kwasababu anatumia simu ya wizi ambayo nakiri ni kweli mimi ndio nilimpatia. Lakini kwanini ya wizi ikiwa nimenunua ikiwa mpya pale Kariakoo? Nilijiuliza hadi pale nilipoambiwa natakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi cha karibu.

Tii amri bila shuruti, nami nilifanya hivyo pasipo kuweka uzito wowote huku nikiamini nipo salama na mdogo wangu atakuwa salama kwasababu tu ile simu ni mpya, huko niliyoyakuta yalizidi kunidhoofisha na kufuta kabisa matumaini ya kurudi mtaani kuendelea na maisha ya kawaida.

Baada ya wiki kadhaa za nenda rudi hatimaye swala liliisha lakini liliacha funzo kubwa ambalo nimeona vema nikiweka hapa ili kila mwenye kusoma apate kuelewa nini kinaendelea.

Kwako ni Mpya, kwao ni ya zamani chunga sana. Kumbe mchezo wote upo hivi:-

Kariakoo kitovu cha biashara nchi hii, pale kuna matumizi makubwa ya akili kwa wafanya biashara wa ngazi zote kuanzia wale wa chini hadi wafanyabiashara wakubwa.

Wapo baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu wanauza simu ambazo zimetumika(wao wananunua) kutoka kwa watumiaji wa hapahapa nchini ambazo zipo kwenye hali nzuri.

Wafanyabiashara hao baadhi wasiowaaminifu usafisha kwa weledi simu zile na kuzitafutia maboksi na kuzirudisha sokoni kama simu mpya, chunga sana ndugu msomaji wangu.

Ni ngumu kwa mtu wa aina yangu ambaye nimekuja mjini ikiwa tayari mwendokasi imeanza kazi kufahamu lolote juu ya hili.

Nili(na)tamani vyombo vyenye mamlaka yangefanya haya.

Bila shaka hawa ni TCRA ndiyo sehemu yao hii, naamini wanaweza kuanzisha mfumo rafiki wa kila mnunuzi wa simu kusajili IMEI namba yake kabla hajaanza matumizi ikihusisha pia na namba ya Nida.

Kupitia Kanzi data hiyo itakuwa rahisi kukataa kusajili IMEI mara mbili kama ambavyo kwenye baadhi ya mifumo inavyogoma kuingiza email yako ikiwa tayari ilishaingizwa zamani.

Kwa mfano, ukiweka IMEI ambayo ni mpya upokee ujumbe labda:
"Ndugu KAJO DININGI BUNO umefanikiwa kusajili kifaa(simu) yenye IMEI namba ×××××××××××".

Na ikiwa umeingiza pia IMEI ambayo imesajiliwa tayari ujumbe wa kuonesha kuwa hujafanikiwa utumwe.

Labda utaniuliza vipi huyu mtu akiamua kuuza simu yake ambayo ameisajili kwa taarifa zake, sahihi kabisa, hapa mfumo utamaliza sintofahamu yote hii na mmiliki wa pili atakuwa salama na wa kwanza atakuwa salama pia.

Kama ambavyo tunaweza kubadili namba zetu za siri kwa kuingiza namba za siri za zamani vivyo ndivyo tunaweza kuondoa taarifa za awali na kuweka mpya.

Imani yangu inaniambia mfumo ukiwa na muundo mzuri utarahisisha yote haya kwa kutengeneza mfumo rafiki kwa watumiaji wa wa aina zote.

NB. Haya ni mawazo yangu ambayo ni kama kuonesha tu nini kifanyike kuelekea kwenye uhuru wa vifaa vyetu, yeyote anaweza akaendeleza wazo hili kwa kulipanga vizuri na utaalamu zaidi ama hata kuliokosoa kabisa kwa lengo la kujenga.

Mwisho.
 
Upvote 50

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
7,077
2,000
Nashukuru umekuwa muwazi kusema kuwa ulikuja mjini tayari mwendokasi zikiwa zimeanza kuoperate
Hi kitu hata mtoto wa hapa hapa mjini bado anaweza kupigwa; nimemsoma vizuri sana jamaa na sijaona mtoto wa mjini anawezaje kukwepa hi kitu, sema wengine ni bahati tu ndio zimetusaidia kutokufikia alipofikia huyu tunae dhania kwamba ni mshamba
 
Abrianna

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
4,690
2,000
Kuna vitu ni vigumu kuvisahau kwenye maisha yangu, vipo vyenye kufurahisha na vile vyenye kuleta maumivu moyoni mwetu. Jambo la kushukuru ni namna Mungu ameweka kitu kusahau ili maisha yaendelee, Mungu wetu ana nguvu sana.

Mwaka 2019 ninaweza nikasahau matukio yote yaliyojiri mwaka huo lakini sio tukio lililopelekea kuwekwa mahabusu ya kituo cha Polisi kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu. Japokuwa limepita lakini ni tukio lililoacha kovu kubwa kwenye moyo wangu, naamini maumivu yake ni mimi peke yangu ninayaelewa.

Ijumaa, Kimara Michungwani.

Ni wakati ambao ndio kwanza nimefika nyumbani kutoka Kariakoo nilikoenda kununua vitu fulani ili nitume huko Mpito kijijini kwetu, macho yangu yakiwa makini kufuatilia kinachoendelea kwenye Tv ghafla simu yangu iliita na kama ilivyo ada nilishika kutazama ni nani, namba ilikuwa ngeni.

Nilishtushwa kuambiwa mdogo wangu yupo mahabusu huko kwetu kwasababu anatumia simu ya wizi ambayo nakiri ni kweli mimi ndio nilimpatia. Lakini kwanini ya wizi ikiwa nimenunua ikiwa mpya pale Kariakoo? Nilijiuliza hadi pale nilipoambiwa natakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi cha karibu.

Tii amri bila shuruti, nami nilifanya hivyo pasipo kuweka uzito wowote huku nikiamini nipo salama na mdogo wangu atakuwa salama kwasababu tu ile simu ni mpya, huko niliyoyakuta yalizidi kunidhoofisha na kufuta kabisa matumaini ya kurudi mtaani kuendelea na maisha ya kawaida.

Baada ya wiki kadhaa za nenda rudi hatimaye swala liliisha lakini liliacha funzo kubwa ambalo nimeona vema nikiweka hapa ili kila mwenye kusoma apate kuelewa nini kinaendelea.

Kwako ni Mpya, kwao ni ya zamani chunga sana. Kumbe mchezo wote upo hivi:-

Kariakoo kitovu cha biashara nchi hii, pale kuna matumizi makubwa ya akili kwa wafanya biashara wa ngazi zote kuanzia wale wa chini hadi wafanyabiashara wakubwa.

Wapo baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu wanauza simu ambazo zimetumika(wao wananunua) kutoka kwa watumiaji wa hapahapa nchini ambazo zipo kwenye hali nzuri.

Wafanyabiashara hao baadhi wasiowaaminifu usafisha kwa weledi simu zile na kuzitafutia maboksi na kuzirudisha sokoni kama simu mpya, chunga sana ndugu msomaji wangu.

Ni ngumu kwa mtu wa aina yangu ambaye nimekuja mjini ikiwa tayari mwendokasi imeanza kazi kufahamu lolote juu ya hili.

Nili(na)tamani vyombo vyenye mamlaka yangefanya haya.

Bila shaka hawa ni TCRA ndiyo sehemu yao hii, naamini wanaweza kuanzisha mfumo rafiki wa kila mnunuzi wa simu kusajili IMEI namba yake kabla hajaanza matumizi ikihusisha pia na namba ya Nida.

Kupitia Kanzi data hiyo itakuwa rahisi kukataa kusajili IMEI mara mbili kama ambavyo kwenye baadhi ya mifumo inavyogoma kuingiza email yako ikiwa tayari ilishaingizwa zamani.

Kwa mfano, ukiweka IMEI ambayo ni mpya upokee ujumbe labda:
"Ndugu KAJO DININGI BUNO umefanikiwa kusajili kifaa(simu) yenye IMEI namba ×××××××××××".

Na ikiwa umeingiza pia IMEI ambayo imesajiliwa tayari ujumbe wa kuonesha kuwa hujafanikiwa utumwe.

Labda utaniuliza vipi huyu mtu akiamua kuuza simu yake ambayo ameisajili kwa taarifa zake, sahihi kabisa, hapa mfumo utamaliza sintofahamu yote hii na mmiliki wa pili atakuwa salama na wa kwanza atakuwa salama pia.

Kama ambavyo tunaweza kubadili namba zetu za siri kwa kuingiza namba za siri za zamani vivyo ndivyo tunaweza kuondoa taarifa za awali na kuweka mpya.

Imani yangu inaniambia mfumo ukiwa na muundo mzuri utarahisisha yote haya kwa kutengeneza mfumo rafiki kwa watumiaji wa wa aina zote.

NB. Haya ni mawazo yangu ambayo ni kama kuonesha tu nini kifanyike kuelekea kwenye uhuru wa vifaa vyetu, yeyote anaweza akaendeleza wazo hili kwa kulipanga vizuri na utaalamu zaidi ama hata kuliokosoa kabisa kwa lengo la kujenga.

Mwisho.
Ushauri mzuri sana kwa TCRA maana wizi wa simu umekua janga na ukipeleka kesi polisi unaweza kutumia gharama kubwa kufuatilia kuliko hata gharama ya simu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom