USHAURI: Tatizo la kucheua

Freightliner

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
720
522
Wataalamu naomba kujua hili tatizo la kucheua linanikumba mara kwa mara hasa nikila vitu kama nyama yaaani nikiitafuna na kumaliza kula baada ya muda mfupi naanza kucheua na kurudi mdomoni poa baadhi ya matunda pia vivo hivyo naomba kujua tatizo hili shida yake ni nini haswa!!!
ASANTE
 
Sitaki kuamini tangu jamaa ametoa tatizo lake/ thread kuhusu matatizo ya KUCHEUA hajajibiwa hata na mdau mmoja..
 
Mkuu, pole sana kwa tatizo unalopata.

Hata mm nishawai kuwa na tatizo kama lako, baada ya kufuatilia sana nikagundua hiyo ni hali ambayo inasababishwa na uwezo mdogo wa mfupi wako wa chakula kusaga chakula unachokula. Maana yake unakula chakula kingi lakini mfumo wako wamengenye uwezo wake ni mdogo, wazungu huo mfumo wanataka digestion system.

Suluhisho nililogundua mpaka leo nimejitibu kabisa ilo tatizo ni kama ifuatavyo :-
1. Kula chakula kiasi, hakikisha usile mpaka ukashiba. Kama tulivyosema mwanzo uwezo wa machine yako ni mdogo, kula chakula kiasi ili machine iweze kumengenya chakula chote, ukila kwa kupitiliza then mwisho kinatoka kwa njia ya kucheua.
2. Jitahidi ule mapema especially mlo wa usiku. Make sure unakula then unapumzika kwa maana husijilaze at least masaa mawili then ndio unaenda kula.

In short tatizo la kucheua ni kwasababu ya kula zaid ya uwezo wako, hii haina maana ya kwamba unakula mpaka unavimbiwa au lah, hii maana yake uwezo mdogo wa mfumo wako wa kuDigest chakula, hata kama unajiona siku zote unakula kwa kiasi.

Jaribu kufatisha hizo vitu kwa muda then utaleta mrejesho hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom