USHAURI: Tanroad Mkoa wa Mwanza ondoeni mataa ya Nyakato Sokoni

witzone2

JF-Expert Member
Jan 14, 2022
780
1,633
Haya mataa mmeyaweka kwa lengo zuri. Lakini ni hatari sana kila siku husababisha ajali ya magari kufeli break. Mteremko wa kutokea national kushuka buzuruga ni mkali sana.

Magari hasa ya Mizigo hufeli sana break. Na ikishafeli hamna namna ni kugonga tu magari kwa nyuma. Jana imetokea na kugongana magari matano. Juzi hivyo hivyo.

Yaondoeni kabla hayajaleta maafa makubwa. Kuna gari za coka na Peps zikiwa Zina mzigo hapo siku zikifeli hapo maafa yatakua makubwa mno. Huyo mteremko ni mkali sana kuweka mataa pale
 
hujaeleza ni mataa ya aina gani na je yanasababishaje ajali najua una point ya maana lakini toa ufafanuzi maana mteremko kama huo sio peke yake Tanzania hata ukitokea Mwenge kuelekea Tegeta hadi Bunju kuna sehemu kuna mataa ya namna hiyo.
 
Mataa hapa yanasaidia sana kuweka ustaarabu barabarani. Solution sio kuondoa mataa ila ni kuhakikisha magari mabovu hayaingii barabarani na hilo ni jukumu la polisi kusimamia sheria hizo shida ni hao polisi wala rushwa tu hawawezi kuismimamia sheria zetu na hata hizo ajali polisi wanapaswa kuwajibishwa. Ajali zimekuwa nyingi sana sababu ya uholela wa matumizi ya vyombo vya usafiri. Tunapoteza ndugu zetu wengi sana na nguvu kazi ya taifa kwa sababu ya kizembe sana. Wenye mamlaka simamieni hili.
 
hujaeleza ni mataa ya aina gani na je yanasababishaje ajali najua una point ya maana lakini toa ufafanuzi maana mteremko kama huo sio peke yake Tanzania hata ukitokea Mwenge kuelekea Tegeta hadi Bunju kuna sehemu kuna mataa ya namna hiyo.
Mataa ya kuongoza magar. Hazipiti siku tatu bila magari kugongana pale kwa kufeli break. Hasa magari ya Mizigo. Mimi ni dereva ule mteremko ni mkali. Na Bahat nzur Ile sehemu hua Haina jamu. Jana magar matano. Na tangu yawekwe haipoti siku tatu gari kwa kufeli break tatzo mteremko ni mkali sana
 
Haya mataa mmeyaweka kwa lengo zuri. Lakini ni hatari sana kila siku husababisha ajali ya magari kufeli break. Mteremko wa kutokea national kushuka buzuruga ni mkali sana.

Magari hasa ya Mizigo hufeli sana break. Na ikishafeli hamna namna ni kugonga tu magari kwa nyuma. Jana imetokea na kugongana magari matano. Juzi hivyo hivyo.

Yaondoeni kabla hayajaleta maafa makubwa. Kuna gari za coka na Peps zikiwa Zina mzigo hapo siku zikifeli hapo maafa yatakua makubwa mno. Huyo mteremko ni mkali sana kuweka mataa pale
samahani huenda sijaelewa nisaidiye.Mataa na kufel break kuna mahusiano gani?
 
Hapo enzi mkapa ni Raisi wananchi walijipanga kumpokea roli likafeli breki lilifyeka watu sana. Bugando walikuwa wanapokea nyama zinarundikwa kwenye turubai mortuary.
 
Kwani mataa yanasababisha ajali kutokea mkuu? Kama vipi huo mteremko udhibitiwe, pajengwe hata bridge ili kudhibiti ajali.
 
hujaeleza ni mataa ya aina gani na je yanasababishaje ajali najua una point ya maana lakini toa ufafanuzi maana mteremko kama huo sio peke yake Tanzania hata ukitokea Mwenge kuelekea Tegeta hadi Bunju kuna sehemu kuna mataa ya namna hiyo.
We unataka ufafanuzi upi ambao hujaelewa hapo?
 
Huwa naumia sana traffic kunipiga fine wakati huo migari ya Coca inapita tu kama hawaioni nachukia sana aisee,,
 
Haya mataa mmeyaweka kwa lengo zuri. Lakini ni hatari sana kila siku husababisha ajali ya magari kufeli break. Mteremko wa kutokea national kushuka buzuruga ni mkali sana.

Magari hasa ya Mizigo hufeli sana break. Na ikishafeli hamna namna ni kugonga tu magari kwa nyuma. Jana imetokea na kugongana magari matano. Juzi hivyo hivyo.

Yaondoeni kabla hayajaleta maafa makubwa. Kuna gari za coka na Peps zikiwa Zina mzigo hapo siku zikifeli hapo maafa yatakua makubwa mno. Huyo mteremko ni mkali sana kuweka mataa pale
Hizo taa ni upigaji mtupu yani zimewekwa hovyohovyo tu,fikiria hapo nata na mlango mmoja taa za nini...njoo kaluta,uhuru dampo napo wameweka taa,unakuja uturn,nyanza primary,halmashauri ya jiji napo wameweka taa...funga kazi ni taa roundabout ya nyerere road nayo inataasijawahi kuona hilo engineer wa tarura atakua katoka gamboshi au chato kilimani
 
Tulia wewe ,,,taa zingine ziko kwa ajili ya wavuka miguu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom