Ushauri: TANESCO wapeni kipaumbele kwanza waliolipia Tsh 300,000 waishe kabla ya kuanza kufungia LUKU wale wa Tsh. 27,000/=

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,374
2,000
Nashukuru bei ya kuingiza umeme imeshuka hadi elfu 27000/= mijini na vijijini kwa sasa. Kesho naenda kuomba luku 10 kwa mpigo kila mpangaji awe na yake.

Lakini inasimuliwa wako watu waliolipia bei ya laki tatu ambao hawajawekewa Luku hadi sasa.

Kutokana na ongezeko la mahitaji kwa wateja wapya wanaolipia elfu 27000/=. Ni vyema kama shirika likawamaliza kwanza kuwafungia umeme wote waliolipia bei za awali za laki tatu na tano.

Pia shirika pamoja na kupunguza bei, liangalie namna ya kupunguza mda wa kusubili kufungiwa umeme angalau isizidi siku saba baada ya mteja kufanya malipo.

Pia kama inawezekana shirika liwatazame kwa jicho la ukarimu ( kuwafidia direct au indirect) wale watakaolipia nguzo nyingi kiasi cha kuusogeza umeme uwe jilani kwa wengine.

Kuliko wengine kuvuta umeme kwa gharama kubwa, halafu wengine wanakuja kuchota tu kirahisi.
 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,169
2,000
Wote wana haki sawa cha msingi aliyechelewa kulipia asifunguwe kabla ya aliyewahibkulipia...
Hata ulipe milioni ila kama kjna wa 27k amekutangulia lazima umsubiri.

Its simple Fair game.
 

Baba Heri

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
1,167
2,000
Nashukuru bei ya kuingiza umeme imeshuka hadi elfu 27000/= mijini na vijijini kwa sasa. Kesho naenda kuomba luku 10 kwa mpigo kila mpangaji awe na yake!

Lakini inasimuliwa wako watu waliolipia bei ya laki tatu ambao hawajawekewa Luku hadi sasa!

Kutokana na ongezeko la mahitaji kwa wateja wapya wanaolipia elfu 27000/=. Ni vyema kama shirika likawamaliza kwanza kuwafungia umeme wote waliolipia bei za awali za laki tatu na tano!

Pia shirika pamoja na kupunguza bei, liangalie namna ya kupunguza mda wa kusubili kufungiwa umeme angalau isizidi siku saba baada ya mteja kufanya malipo!

Pia kama inawezekana shirika liwatazame kwa jicho la ukarimu ( kuwafidia direct au indirect) wale watakaolipia nguzo nyingi kiasi cha kuusogeza umeme uwe jilani kwa wengine!

Kuliko wengine kuvuta umeme kwa gharama kubwa, halafu wengine wanakuja kuchota tu kirahisi!
Biashara ya kufungiwa mita zaidi ya moja kwenye jengo moja hamnaga tena mkuu
 

Hajto

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
4,178
2,000
Nimeona leo kwenye hotuba yake anasema anataka hadi 2024 Tanzania yote kuwe na umeme mpaka nyumba za nyasi
 

Chief

JF-Expert Member
Jun 5, 2006
2,556
2,000
Ni hasara kwa shirika
Kwa nini wasitengeneze mita kama simu wewe unanunua mita yako dukani toka watengenezaji mbali mbali halafu TANESCO wanakuuzia chip buku tu ambayo ndio account number yako ? Tatizo la mita linaisha siku moja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom