Ushauri: TANESCO wabadili jina la huduma ya "Emegency" halafu waite "Genge la mafundi" italeta maana halisi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Iko shida sana kwenye matumizi ya majina ya huduma hapa kwetu bongo!

Kuna haja BAKITA kutoa elimu kwenye Taasisi ili zisadifu huduma kulingana na majina.

Kisaikolojia inatamkwa kuwa jina ni sehemu ya Huduma.

Emergency Service maana yake ni dharula (Maana yake Ni huduma pasipo Maandalizi).

Ukipiga simu Tanesco Emergency Leo, Huduma ya Haraka utakayopatiwa ni KUULIZWA JINA NA NAMBA YAKO YA SIMU BHAASI!

Lakini huduma usishangae kabisa mafundi wakakufikia baada ya saa 48, wiki au wasije kabisa.

Sina tatizo na uchelewaji wao yamkini hawana bajeti ya kutosha kutoa huduma kwa wakati.

Hoja na lawama zote ni kuendelea kutumia neno la EMERGENCY (Hii ni saikolojia) WAFUTE NENO Emergency na waandike ni HUDUMA YA KIUFUNDI.

Magari yao wayaandike (GENGE LA KIUFUNDI).

Kuendelea kuita EMERGENCY SERVICE sidhani kama ni sahihi! Ni ushauri tu katika kuboresha ili kuondoa lawama.
cc. Tanesco Yetu
 
Sijui Afrika tuliangukia wapi aisee hakuna mahali unaweza kupata huduma za dharula kwa wakati nadhani kuna kitu kinapungua sio bure.Yahani awa jamaa ukiwambia kuna short nyumbani wanakwambia zima nyumba nzima mafundi watakuja sijui
 
Yaani ni aibu kwa yaliyonikuta siku nimepatwa na dharula ....ni aibu ....kwakweli ni bora afanye ulichoshauri kuliko majina waliyojiita...
 
Yaani ni aibu kwa yaliyonikuta siku nimepatwa na dharula ....ni aibu ....kwakweli ni bora afanye ulichoshauri kuliko majina waliyojiita...
Halafu wakifika wanakata tu umrmr na kusema watarudi
 
Tanga jiji no ya customer care ni 0658122412 ila hawapokei kabisa hata uwe na dharura ya kuunguliwa na moto
 
Piga simu Tanesco..
Piga simu polisi
Piga simu ambulance...

Shida sio wao..shida iko serikali kuu

Tunatakiwa tuwe na huduma hizi kwenye kata yako....
Polisi kata yenye magari ya doria
Ambulance ya kata..
Na huduma zote za kiserikali kwenye kata yako
 
Ili hizi huduma ziwepo.. itabidi ifanyike investment ya watu na pesa nyingi
 
Nawashauri Tanesco na huduma nyingine za dharura waweke hata malipo kidogo tutalipa na sio waseme ni bure na bado hawana uwezo na nia ya kuhudumia.Lakini natoa ushauri, tutafuteni hela, bure alishazikwa zamani katika ulimwengu wa leo na kaburi lake lilibebwa na mafuriko ya mwaka ...
 
Iko shida sana kwenye matumizi ya majina ya huduma hapa kwetu bongo!

Kuna haja BAKITA kutoa elimu kwenye Taasisi ili zisadifu huduma kulingana na majina.

Kisaikolojia inatamkwa kuwa jina ni sehemu ya Huduma.

Emergency Service maana yake ni dharula (Maana yake Ni huduma pasipo Maandalizi).

Ukipiga simu Tanesco Emergency Leo, Huduma ya Haraka utakayopatiwa ni KUULIZWA JINA NA NAMBA YAKO YA SIMU BHAASI!

Lakini huduma usishangae kabisa mafundi wakakufikia baada ya saa 48, wiki au wasije kabisa.

Sina tatizo na uchelewaji wao yamkini hawana bajeti ya kutosha kutoa huduma kwa wakati.

Hoja na lawama zote ni kuendelea kutumia neno la EMERGENCY (Hii ni saikolojia) WAFUTE NENO Emergency na waandike ni HUDUMA YA KIUFUNDI.

Magari yao wayaandike (GENGE LA KIUFUNDI).

Kuendelea kuita EMERGENCY SERVICE sidhani kama ni sahihi! Ni ushauri tu katika kuboresha ili kuondoa lawama.
cc. Tanesco Yetu
Tena angekua Bashungwa huko watu wangekaa gizani hata mwezi mzima
Angewaambia wawashe mchana kwaajili ya viwanda halafu usiku mitambo na watu nimapumziko.
Yani TFF ya Taneaco kwenye emergency nisawa na ile ya ngosha Bashungwa
 
Back
Top Bottom