Ushauri, tahadhari, na maoni kuhusiana na biashara ya juice ya miwa

Edson Carrington

JF-Expert Member
Oct 30, 2022
216
634
Habari wakuu,

Mimi ni kijana mjasiriamali na nimeamua rasmi kujikita huko katika harakati zangu za utafutaji na kuongeza kipato. Na nimejaribu kufuatilia sana kuhusu biashara ya juice ya miwa ambayo kwa sasa ni habari ya mjini hapa dar kutokana na jua linalowaka.

Ombi langu wakuu ni maoni yenu viongozi maana nataka nijikite rasmi huko na nipo mbioni kununua mashine ya juice na baadhi ya vifaa au vyombo vitakavyonisaidia kuendeshea biashara hiyo.

Maombi yangu kwenu ni kama ifuatavyo;
●Je, ni vitu, vifaa au vyombo gani muhimu napaswa kuwa navyo kwa sasa
●Ni aina gani ya mashine ambayo ni bora, ( umeme au petrol)
●Tahadhari gani natakiwa kuchukua kabla ya kuanza mradi huu
●Ni aina gani ya kijana natakiwa kumchagua ili anisaidie

●Wapi naweza pata miwa

●Sehemu gani nzuri kwa kuanzisha biashara hii
●Changamoto za biashara hii

Naomba mchango wenu wakuu
 
Umeshasema ni habari ya mjini alafu unauliza wapi pazuri pa kuuzia. Nina mashaka hata biashara yenyewe huiwezi umeanzisha uzi wa kujifariji tu. Research unafanya ww kama ww usisubiri wana jf waje wakuambie toka zunguka ongea na wenye hizo biashara direct uone reaction zao ujifunze
 
Pamoja brother, nahitaji kuifanya
 
Back
Top Bottom