Ushauri tafadhali - Toyota Vitz, Duet, Allex, RunX, Suzuki SWIFT,

Korosho

Senior Member
Nov 30, 2007
132
29
Tafadhali naombeni ushauri kwa wote wanaomiliki au waliowahi kumiliki moja kati ya gari hizi: Toyota Vitz, Toyota Duet, Toyota Allex, Toyota RunX na Suzuki Swift.

Nataka kununua gari yenye injini ndogo ( 1- 1.3 litres) na ningependa kupata uzoefu juu ya uimara wa magari haya, upatikanaji wa vipuri (spare parts) na maelezo mengine kiujumla.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Umesahau Toyota Starlet (SOLEIL 4DOORS) sio REFLECT ni bomba mbaya hasa ukiweka spot tyre unasafiria popote confortable, mi ninayo SOLEIL ya mwaka 96 ila huwezi amini naipiga masafa ya Mza, Mby na Arusha haichemshi wala kupata miss, 4E FE ni njini bomba na ndizo mjapani alipotulia na kuziunda.
 
Mkuu,

Sina uhakika kama tayari ushanunua gari, ila kwa hayo magari uliyoyalist, ushauri wangu ni kama ifuatavyo:

Toyota Vitz
Ni nzuri kwa utumiaji wa mafuta. Spea zipo ila bei mbaya. Sio gari imara sana kwa kifupi. Kama una hela ya kununua spea kwa gharama, ni gari nzuri.

Duet
Hili sikushauri hata kidogo. Lina 3 pistons. Hii engine inasumbua na kuna wakati inaweza kuleta mlio fulani kwenye engine (kawaida ya 3 pistons engine) ambao kuurekebisha ni ngumu (au haiwezekani kabisa). Utaangaika tu kwa mafundi.

Utumiaji wake wa mafuta ni mzuri, ila engine ni kimeo.

Allex
Hii sijawahi kuigusa, hivyo sina uzoefu wa spea wala uimara wake. Haina tofauti na toyota RunX, zote zinatumia engine sawa (inategemea na model lakini)

RunX
Hii ni Corolla Runx. Ni nzuri, ila sina uhakika na ubora wa engine wala upatikanaji wa spea. Ila, kama ilivyo kawaida, gari mpya spea zake ni ngumu kidogo kupata na bei huwa juu. Hii inawezekana kwa Allex na RunX, ingawa sina uhakika.

Pia, kama unatazamia kununua Allex au RunX, angalia pia na IST. Zote zinatumia Engine sawa, na bei zake zinakaribiana sana, lakini zipo juu. FOB ya chini ni around USD 3,600 (kwa gari nzuri)

Suzuki SWIFT
Achana na hii gari mkuu. Spea ni ngumu kupata.

Inatumia mafuta vizuri, na ni gari nzuri. Ishu itakupata kwenye spea tu.

Bottom line:

Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, engine ndogo ya Toyota 4E-FE ni engine bomba sana, imetulia na spea ni bei chee kila kona. Inatumika kwenye Toyota Starlet na Raum (na model nyingine nyingi tu)

Toyota Starlet ni model ya nyuma kidogo, ni nzuri, ila Raum ni ya mpya zaidi ya Starlet.

Kama unataka gari ndogo, spea zinazopatikana ki urahisi na bei nafuu, Toyota Raum is among the best options out there.

Ila, kama wewe sio mtunzaji mzuri, mlango wa nyuma unaweza kuharibika mapema. But anyway, spea zipo na ni bei nafuu.

Kazi kwako.

Ramthods
 
Ya mwaka gani........??? isije ikawa unazungumzia la 2010 na mwenzio ameliona la 1991
 
02.jpg 10.jpg 022.jpg kama ni kwa gari mimi ninau zoefu wa Suzuki Swift 2006-2010 sio zile za kizamani, ni gari nzuri sana namimi nimekuwa nikiitumia kila siku kwa shughuri mbali mbali,uzuri zaidi ni kwamba service yake ni karibu bure kabisa, sijawahi kununua hata spea moja eti imeharibika yaani hakuna kabisa ,ni gari nzuri utipenda sana kwani hata apperance yake ni nzuri.
01w.jpg Ila sijui unaongelea suzuki zipi, usije ukawa unaongelea za kizamani yaani below 2005
 
sijawahi kununua hata spea moja eti imeharibika yaani hakuna kabisa ,ni gari nzuri utipenda sana kwani hata apperance yake ni nzuri

Mkuu, embu tu jaribu kwenda ilala, au maduka mengine ya spea, then jifanye unatafuta spea, lets say, uliza kama gear box ipo, au AC Compressor, then utajijibu wewe mwenyewe.

Ni zuri likiwa zima, ila litakapohitaji matengenezo ndipo mchakato unapoanza.

Kuhusu service, hilo ni jambo la kawaida. Gari zote zenye engine ndogo, service ni bei ya kutupa.
 
Kuna mdau ameni PM kuhusu ni gari gani achague kati ya Subaru Forester na Nadia. So I thought I would share it with all of you and get more input from the entire community.

Subaru Forester ni gari ngumu, kama ilivyo RAV 4 (Engine 3S-FE model 1994 - 2000, 1997 - 2003 RAV4 EV). Spare zake kwa wastani zipo juu, zaidi hata ya RAV4.

Kwa kifupi, Subaru Forester ina compete na RAV4, na zote zimetolewa almost at the same time.

Subaru Forester ina engine kubwa, 2500cc (RAV4 2000cc), hivyo lazima ujiandae kuweka mafuta ya kutosha, ukizingatia na foleni zetu za bongo.

Engine kubwa ni nzuri kwa safari, au kama una mizunguko ambayo hakuna foleni. Kama kula foleni, injini kubwa itakula mafuta mengi zaidi ya engine ndogo. Unapochagua ukubwa wa engine, zingatia matumizi na uwezo wako kiuchumi.

Kwa kifupi, kwa mtu wa kipato cha chini anaeanza maisha, Subaru Forester si gari ya kununua period.

Toyota Nadia.

Nadia inatumia engine ya D4, na hii ni pamoja na RAV4 (Engine 1AZ 2000 - 2005) na gari nyinginezo.
Kwa kifupi, D4 engine ni technologia mpya, mafundi bongo hakuna.

In short, KAA MBALI na D4 engine.

Soma hizi links:

Toyota Nadia with a D4 engine - AA New Zealand

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/49023-mtaalam-wa-engine-za-d4.html

Bottom line:

Kama unaanza maisha, kati ya Subaru Forester na Nadia hakuna la kununua hapo.

Kama una budget ya kutosha na uchumi mzuri, Forester in not a money wester.

You are welcome,

Ramthods
 
Nunua toyota yenye ingine ya 4e,5e,7e,ti,au ,premio,carina,ti usinunue,d4 kimeo,/Vtiz ni vvti ninzuri haisumbui ila kama unasafari zako nyingi sikushahuri,Allex ni corolla inaweza kuwa se au fe.
 
---------- Corrections to my above post ------------

Subaru Forester comes with 2000cc and 2500cc, check the model that you are buying.
 
Nunua toyota yenye ingine ya 4e,5e,7e,ti,au ,premio,carina,ti usinunue,d4 kimeo,/Vtiz ni vvti ninzuri haisumbui ila kama unasafari zako nyingi sikushahuri,Allex ni corolla inaweza kuwa se au fe.

Let me correct your post.

Hakuna engine ya FE au SE. FE na SE ni features za engine husika.

SE inamaanisha Direct Injection,
FE ina maanisha Economy Narrow Angle Double Over Head Camshaft with Electronic Injection

Kwa mfano Toyota RAV4 yenye engine ya 3S-FE inamaanisha:

3rd Generation of S engine Block with FE features (nimezitaja hapo juu).

Toyota RunX and Toyota Allex zote ni Corrolla (Actually, Allex ni Corolla Sprinter).
Toyota IST ni platfrom ya toyota Vitz.
Zote hivi tatu ninatumia engine ya 1NZ-FE VVT-i 1500cc
 
Mkuu,

Sina uhakika kama tayari ushanunua gari, ila kwa hayo magari uliyoyalist, ushauri wangu ni kama ifuatavyo:

Toyota Vitz
Ni nzuri kwa utumiaji wa mafuta. Spea zipo ila bei mbaya. Sio gari imara sana kwa kifupi. Kama una hela ya kununua spea kwa gharama, ni gari nzuri.

Duet
Hili sikushauri hata kidogo. Lina 3 pistons. Hii engine inasumbua na kuna wakati inaweza kuleta mlio fulani kwenye engine (kawaida ya 3 pistons engine) ambao kuurekebisha ni ngumu (au haiwezekani kabisa). Utaangaika tu kwa mafundi.

Utumiaji wake wa mafuta ni mzuri, ila engine ni kimeo.

Allex
Hii sijawahi kuigusa, hivyo sina uzoefu wa spea wala uimara wake. Haina tofauti na toyota RunX, zote zinatumia engine sawa (inategemea na model lakini)

RunX
Hii ni Corolla Runx. Ni nzuri, ila sina uhakika na ubora wa engine wala upatikanaji wa spea. Ila, kama ilivyo kawaida, gari mpya spea zake ni ngumu kidogo kupata na bei huwa juu. Hii inawezekana kwa Allex na RunX, ingawa sina uhakika.

Pia, kama unatazamia kununua Allex au RunX, angalia pia na IST. Zote zinatumia Engine sawa, na bei zake zinakaribiana sana, lakini zipo juu. FOB ya chini ni around USD 3,600 (kwa gari nzuri)

Suzuki SWIFT
Achana na hii gari mkuu. Spea ni ngumu kupata.

Inatumia mafuta vizuri, na ni gari nzuri. Ishu itakupata kwenye spea tu.

Bottom line:

Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, engine ndogo ya Toyota 4E-FE ni engine bomba sana, imetulia na spea ni bei chee kila kona. Inatumika kwenye Toyota Starlet na Raum (na model nyingine nyingi tu)

Toyota Starlet ni model ya nyuma kidogo, ni nzuri, ila Raum ni ya mpya zaidi ya Starlet.

Kama unataka gari ndogo, spea zinazopatikana ki urahisi na bei nafuu, Toyota Raum is among the best options out there.

Ila, kama wewe sio mtunzaji mzuri, mlango wa nyuma unaweza kuharibika mapema. But anyway, spea zipo na ni bei nafuu.

Kazi kwako.

Ramthods
je vipi kati ya suzuki escudo na RAV4 ipi ni imara zaidi
 
je vipi kati ya suzuki escudo na RAV4 ipi ni imara zaidi

Zote hizi ni imara kaka. Nunua moja kazi ya hizo itakufaa.

Ila kwa Escudo kuna version tofauti za engine. Kuna ya 1,500cc hadi 2,400. So angalia hapo wewe ipi inakufaa.

Hizo zenye engine kubwa ni V6, so kama unakuwa kwenye foleni muda mrefu mafuta yatatumika sana. Ingawa kwa safari ndefu (kama mkoani) ndo nzuri.

Binafsi napenda RAV4 kwa sababu ya muonekano wake. Ila nimeshawahi kuwa na zote, na zote nimezifurahia kwa kweli
 
Mkuu vipi kuhusu Toyota OPA, au ipsum? Au gaia?

Ipsum/Gaia ya mwaka gani?

Ipsum na Gaia zinafanana sana, tofauti kubwa ipo tu kwenye mwonekano wake. Kuna zenye 2,000cc na 2,400cc kutegemeana na mwaka. Za miaka ya nyuma kidogo nyingi zina engine ya 3S ambayo ndio inatumika kwenye RAV4 (za zamani).

Opa ni nzuri pia, ingawa ipo chini sana. Huwezi itumia kwenye barabara mbovu mbovu. Opa inatumia engine ileile kama ya Runx au IST na ipo poa kabisa. Ni VVTi.

Kuna watu wanasema OPA ni mayai sana (so delicate) but me binafsi sina uhakika na hilo.
 
Duet ni gari nzuri sana ingawa ina piston tatu, hauwezi ukanunua gari bila ya kuifanyia modification lazima itasumbua baadaye tu kuanzia kwenye engine hadi matairi kutokana na barabara zetu kuwa mbovu lazima uangalie hili,tairi za hii gari ni saizin13 ambazo ni ndogo na nyembamba sana kwa hiyo gari inakuwa iko chini sana na kwenye rough road inakuwa ni ngumu kupita, hapa inabidi ubadilishe rim pamoja na tairi kwa kufunga size 14 hali kadhalika kwenye engine inashauriwa uweke plug original ili ulipuaji wa mafuta uwe wa uhakika baada ya hapo service za mara kwa mara, baada ya hapo gari haitakusumbua tena , nina mwaka wa pili na nasafiri. Ayo kwenda moshi na tanga bila wasiwasi
 
Ipsum/Gaia ya mwaka gani?

Ipsum na Gaia zinafanana sana, tofauti kubwa ipo tu kwenye mwonekano wake. Kuna zenye 2,000cc na 2,400cc kutegemeana na mwaka. Za miaka ya nyuma kidogo nyingi zina engine ya 3S ambayo ndio inatumika kwenye RAV4 (za zamani).

Opa ni nzuri pia, ingawa ipo chini sana. Huwezi itumia kwenye barabara mbovu mbovu. Opa inatumia engine ileile kama ya Runx au IST na ipo poa kabisa. Ni VVTi.

Kuna watu wanasema OPA ni mayai sana (so delicate) but me binafsi sina uhakika na hilo.

Ram shukrani sana,hakika jf ndio kila kitu ni true alive google
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom