USHAURI: Tafadhali tafadhali, mchakato wa ajira serikalini usirejeshwe kwenye Taasisi za Umma

DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
544
558
Nawasalimu kwa jina JMT

Moja kwa moja najikita kwenye mada.

Nimepata ndogo ndogo kwamba kuna baadhi ya taasisi za umma zinaomba/zinataka warejeshewe mamlaka ya mchakato wa ajira kama zamani kinyume na Sekretarieti ya ajira PSRS inayosimamia suala hilo kwa sasa.

Naishauri serikali isisikilize hilo ombi/takwa kwani PSRS angalau wanajitahidi kutenda haki ktk zoezi zima la recruitment ingawa nako pia kuna changamoto, lakini ni afadhali wao kuliko turudi kwenye kizazi cha vimemo.

Tafadhali tafadhali naiomba serikali kama ina nia njema na sisi basi waifanyie maboresho PSRS na sio kurejesha mamlaka ya kuajiri kwenye taasisi za uma kila taasisi ijiajirie yenyewe.

Ni hilo tu!

Kazi Iendelee
 
Yaani watu wamepanic,kila huyo anataka ale atakavyoweza,Magu alikua na madhaifu yake,ila naona nchi inataka irudi kama kipindi cha nyuma.Watu waitafune hadi basi.Vimemo vitatumika hadi basis.
 
Back
Top Bottom