Ushauri tafadhali nataka kulinda ndoa, kazi kikwazo kikubwa

1. tuliza akili yako usidanganyike ukaacha kazi kwa ajili ya kumfuata mwenzio.....ni kosa kubwa sana la kiufundi.hata yeye asiache kukufuata.fikiri kwa makini mfano unatoa notice,unaenda unamfumania,au ana mimba isiyo yako,kazi huna na mke huna.
2.msumbue mwajiri kila siku,kuna siku ataelewa.kama boss wako hataki waone wakubwa zake.usitangulize haiwezekani
3.umbali peke yake hauhatarishi ndoa,kuna hatari kibao hata kama mko ofisi moja na mkeo.
Well said, thanx Mkuu. Bahati mbaya ni pale Mkubwa mwenyewe anapotoa majibu kama hayo ya kukatisha tamaa unakimbilia kwa nani tena? Labda kwa Chief Secretary!!!!!!!!!!!
 
well said, thanx mkuu. Bahati mbaya ni pale mkubwa mwenyewe anapotoa majibu kama hayo ya kukatisha tamaa unakimbilia kwa nani tena? Labda kwa chief secretary!!!!!!!!!!!
1.basi waweza kumuona huyo c/s na wakati huo huo ukichapa kazi sana kupita maelezo.....mwajiri lazima atafanya utakavyo.
2.kumbuka kazi mbaya kama unayo.utamuona shem mchungu pale ukiwa huna kazi au uliacha kazi nzuri kwa sababu yake na bahati mbaya sasa hasomeki.
3.mungu aliewatenganisha wakati huu si mjinga........shukuru kwa kila jambo.
 
QUOTE=Gerrard;2457670]Dah Arusha tena? Mbona kama hakuna tofauti sana na Mbeya? Labda ungesema Moro au Kibaha. Waajiri wetu ni balaa tupu Kaka. Unakutana na Afisa Utumishi aliyezoea kazi anakwambia &quot;chagua Mke au kazi&quot;[/QUOTE]<br />
<br />
Mkuu inafikia kipindi uongee na mkeo na mpange namna ya kusolve hilo tatizo. Maana nakumbuka kuna rafiki yangu alisota miaka mitatu kupata uhamisho wa mke wake kutoka dodoma kuja arusha
So pambana kaka na naamini utafanikiwa wakati huo ukitafuta kazi sehem nyingine karibu na wife
 
1. tuliza akili yako usidanganyike ukaacha kazi kwa ajili ya kumfuata mwenzio.....ni kosa kubwa sana la kiufundi.hata yeye asiache kukufuata.fikiri kwa makini mfano unatoa notice,unaenda unamfumania,au ana mimba isiyo yako,kazi huna na mke huna.
2.msumbue mwajiri kila siku,kuna siku ataelewa.kama boss wako hataki waone wakubwa zake.usitangulize haiwezekani
3.umbali peke yake hauhatarishi ndoa,kuna hatari kibao hata kama mko ofisi moja na mkeo.

Umechukua maneno yangu mdomoni sina la kuongeza
 
1. tuliza akili yako usidanganyike ukaacha kazi kwa ajili ya kumfuata mwenzio.....ni kosa kubwa sana la kiufundi.hata yeye asiache kukufuata.fikiri kwa makini mfano unatoa notice,unaenda unamfumania,au ana mimba isiyo yako,kazi huna na mke huna.
2.msumbue mwajiri kila siku,kuna siku ataelewa.kama boss wako hataki waone wakubwa zake.usitangulize haiwezekani
3.umbali peke yake hauhatarishi ndoa,kuna hatari kibao hata kama mko ofisi moja na mkeo.
.

Bwana Gerrard: Chukua hii kutoka kwa Tall
 
  • Thanks
Reactions: SG8
pole mkubwa, hili ni tatizo ambalo linatukabili tuliajiriwa, ndio maana mie kuajiriwa naona kama utumwa vile, nimekuwa na hali kama yako hadi mwaka jana nilipoamua kujivua gamba! hizi ajira bana zinatusaidia lakini wakati mwingine zinatubomolea familia, kaka nadhani anza kujipanga either wewe au mamsap mmoja atoke kwenye ajira aingie kwenye ujasiriamali, kidogo hapo mtakuwa na uhuru na muda wa kutosha kuwa pamoja hata kama mko mikoa tofauti muda unakuwa nao pale unapokuwa your own boss,kumbuka ukifukuzwa kazini utakimbilia kwa mkeo mkeo kupata faraja() ila ukifukuzwa kwa mkeo kazini huwezi pata faraja yoyote! ..nitakuwa karembu jioni hii tutafutane mkuu
 
Gerrard, mimi niliwahi kupata hiyo challenge na sikukaa hata miezi sita... niliacha kazi mkuu

Ndoa si sawa na mahusiano ya kawaida
 
  • Thanks
Reactions: SG8
"Jamani naitaji msaada mkubwa sana, wa mawazo na saikolojia. Mimi nina mke nimezaa nae. Tangu tufunge ndoa ni miaka 4 sasa.yeye yuko Mkoani mimi niko chuoni Dar es Salaam kimasomo elimu ya juu". By Kipusy

Maneno ya utangulizi wa thread ya ndugu yetu Kipusy kwa yaliyomkuta. Ndoa yangu ina miaka 4 na mtoto 1 na Wife yupo Dar kikazi wakati mimi nipo Mkoani kikazi pia. Tatizo tunalojaribu kukabiliana nalo ni kukwepa majaribu yanayotokana na umbali kati yetu. Hata hivyo kwa nature ya kazi zetu ni mimi tu mwenye uwezekano wa kuhamia Dar kwani mwajiri wa mwenzangu hana ofisi huku mkoani.

Nimejaribu kumshawishi mwajiri wangu anirudishe karibu na familia lakini dalili za kufanikiwa hivi karibuni hazionekani, labda baada ya miaka mitatu hivi. Kwa upande wangu nimechoshwa mno, mno na maisha haya ya kuwa Modified bachelor hasa ukizingatia matatizo ya ndoa za siku hizi.

Naomba ushauri wenu nifanye nini kati ya haya yafuatayo?
1 Kuomba uhamisho ambao nimeshaona mafanikio yapo mbali sana kwa sasa?
2.Kuomba kuhamia kwa mwajiri mwingine mwenye nafasi?. Hili nalo litakuwa gumu zaidi kwani sio rahisi kupitishwa kwa barua yangu ya uhamisho.
3.Nitautafute kazi nyingine serikalini (niliko) au taasisi binafsi ili nisogee jirani na familia au
4.Niendelee kulinda kibarua huku nikihatarisha ndoa yangu hasa ukizingatia tangu siku ya harusi hatujafanikiwa kuishi miezi zaidi ya 6 pamoja huku kila mwezi tukipoteza nauli kusafiri safiri?

Najua humu jamvini kuna watu wenye uzoefu mbalimbali hivyo natarajia nitapata ushauri utakaoniwezesha kufanya maamuzi.

Nawasilisha

Mtafute yule mtoto wa Sheikh Yahaya aliyeachiwa mikoba ya mzee atakupatia MISFORTUNE REMOVER ukaogee muajiri atakulewa.
 
Wote wawili tunakerwa sana na hali hii. Siku niliyopata barua ya kupangiwa kituo huku Mkoani mwenzangu alilia usiku kucha. Na hata kuja kunitembelea afadhali mimi naweza kupitisha miezi mitatu lakini yeye anaweza kuja mara mbili kwa mwezi.

Hujamalizia kujibu maswali yote...... such as:
1. Nani yuko kwenye nafasi nzuri ya kupata kazi ukilinganisha na mwenzie
2. Kipato vile vile, nani anamzidi mwenzie........ hebu rejea hayo maswali ya mwenzangu hapo juu...........
 
kama uko serikalini ni rahisi kupata uhamisho, nenda moja kwa moja hadi kwa boss wako ukiwa na ile barua iuliomba uhamisho watakusikiza na hakikisha unafuATILIA file hatua kwa hatua huwa wanakalia mafaili hadi mhusika awepo, mm nlikuwa MKOANI kikazi nikaomba kuhama ndnai ya miezi 6 nikahama, nlikuwa nakuja dar kufuatilia mwenyewe mabos huwa wanaelewa hali halisi, ndoa ni muhimu bwana na mtoto pia anahitaji uwepo wenu.kama ongea na wife mkubaliane then wakikunyima ruhusa tafuta kazi huku ukiwa kazini, usiache kazi kabla hujapata kazi,Mtangulize MUNGU.
 
Hapo pagumu kwani hata mimi limenikuta tatizo kama lako na tangu tuajiliwe hatujafanya maendeleo yoyote mishahara yetu inaishia kula na kusafiri kila wakati kufuata familia.Nafikiri waajili wanapaswa kulitilia maanani swala hili vinginevyo ndoa zitakuwa hatarini.
 
Pole sana mkuu! lakini chakaecha akili uangalie lipi bora, kuacha kazi na kuajiriwa upya, au kubaki kazini na kuhatarisha ndoa yako. Kama una shule ya kutosha naamini hutakosa kazi.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Pole sana mkuu! lakini chakaecha akili uangalie lipi bora, kuacha kazi na kuajiriwa upya, au kubaki kazini na kuhatarisha ndoa yako. Kama una shule ya kutosha naamini hutakosa kazi.
Akili kumkichwa. Nimekuelewa sana, thanx
 
pole mkubwa, hili ni tatizo ambalo linatukabili tuliajiriwa, ndio maana mie kuajiriwa naona kama utumwa vile, nimekuwa na hali kama yako hadi mwaka jana nilipoamua kujivua gamba! hizi ajira bana zinatusaidia lakini wakati mwingine zinatubomolea familia, kaka nadhani anza kujipanga either wewe au mamsap mmoja atoke kwenye ajira aingie kwenye ujasiriamali, kidogo hapo mtakuwa na uhuru na muda wa kutosha kuwa pamoja hata kama mko mikoa tofauti muda unakuwa nao pale unapokuwa your own boss,kumbuka ukifukuzwa kazini utakimbilia kwa mkeo mkeo kupata faraja() ila ukifukuzwa kwa mkeo kazini huwezi pata faraja yoyote! ..nitakuwa karembu jioni hii tutafutane mkuu
Dah Mkuu nimeipenda hiyo ya Karembu japo najua ni too late. Nilikuwa Shaba jioni hii. Asante Mkuu wangu kwa ushauri mzuri na changamoto
 
kama uko serikalini ni rahisi kupata uhamisho, nenda moja kwa moja hadi kwa boss wako ukiwa na ile barua iuliomba uhamisho watakusikiza na hakikisha unafuATILIA file hatua kwa hatua huwa wanakalia mafaili hadi mhusika awepo, mm nlikuwa MKOANI kikazi nikaomba kuhama ndnai ya miezi 6 nikahama, nlikuwa nakuja dar kufuatilia mwenyewe mabos huwa wanaelewa hali halisi, ndoa ni muhimu bwana na mtoto pia anahitaji uwepo wenu.kama ongea na wife mkubaliane then wakikunyima ruhusa tafuta kazi huku ukiwa kazini, usiache kazi kabla hujapata kazi,Mtangulize MUNGU.
I salute you Mkuu! Nitaufanyia kazi ushauri wako
 
1.basi waweza kumuona huyo c/s na wakati huo huo ukichapa kazi sana kupita maelezo.....mwajiri lazima atafanya utakavyo.
2.kumbuka kazi mbaya kama unayo.utamuona shem mchungu pale ukiwa huna kazi au uliacha kazi nzuri kwa sababu yake na bahati mbaya sasa hasomeki.
3.mungu aliewatenganisha wakati huu si mjinga........shukuru kwa kila jambo.
Nashukuru Mkuu kwa ushauri wako. Ndio maana nimeleta hapa jamvini nikiamini kuna watu wenye busara kama wewe. Be blessed
 
Hujamalizia kujibu maswali yote...... such as:
1. Nani yuko kwenye nafasi nzuri ya kupata kazi ukilinganisha na mwenzie
2. Kipato vile vile, nani anamzidi mwenzie........ hebu rejea hayo maswali ya mwenzangu hapo juu...........

kazi ni ya kupita na familia ina nafasi yake na tena nafasi ya familia ni kubwa zaidi ... kati yako na mkeo ni vyema mkakaa chini mkaangalia ni wapi kuna unafuu na kunapangika kimaisha then mmoja wenu aanze kutafuta kazi ili aungane na mwenzake ...
  • umbali unapunguza uhalisi wa mapenzi kwani hakuna zaidi ya kuongopeana japo pia nafasi ipo kubwa ya kuwa pamoja na kuongopeana ..
  • kwa kipindi mlichokaa mbali pia mnaweza kuwa karibu na kuanza kuishi pamoja mkajikuta hakuna maelewano kwa kuwa kipindi cha utengani lazima kila mtu alikuwa na maisha fulani na mambo fulani aliyokuwa anayafanya chini ya kapeti
cha kufanya ;
  1. kwanza ndugu yangu kaa chini ujichunguze u msafi kiasi gani ??
  2. ongea na mkeo katika hali ya kujenga mtazamo mpya na wa mwelekeo
 
Nianze kwa kuwapa pole na kumwomba Mungu Awaongoze ktk njia sahihi ya kutatua tatizo lenu.

Kumbuka: Ndoa ni wito na ushirika ndio maana sio wote ni wanandoa!
Maisha ya ndoa si lelemama yana matatizo mengi (kama hilo lako), sio majaribio kwa wakristu ukifunga imefungwa.

Ingawa ni jukumu le2 kufanya kazi kwa bidii ili 2pate kipato kitakachotuwezesha kujikimu LAKINI
Kama kweli unataka kuyaishi maisha yako ya ndoa kikamilifu, Nakushauri Ndoa kwanza Kazi baadaye!

Kumbuka maisha ya furaha huleta raha ya nafsi
Hata uwe na pesa vipi! kama huna raha ni kazi bure
Ni bora unenepe bila kula kuliko kula bila kunenepa

Maisha ya ndoa yanahitaji msingi wa kubeba uzito wa ndoa na nguzo za kuimarisha ndoa.Msingi ukiwa siyo imara na nguzo zikiwa mbovu, ndoa haiwezi kudumu kwa muda mrefu. Ni jukumu la wanandoa, kujenga msingi imara na kutumia nguzo bora za kuunda na kutunza ndoa zao. Haki na Wajibu ndio msingi wa ndoa yoyote.Kama wewe ni Mkristu soma: 1Kor:7 ,Ni wajibu wa kila mmoja aliye ndani ya ndoa kuhakikisha anamtimizia mwenzake haki yake, pia Haki yenu ni kushirikishana ktk kila kitu ktk maisha yenu yote kama mlivyoapa.Mpe mwenzio kiukamilifu haki yake. Kumbuka kuachana sio lengo la ndoa na sio mpango wa Mungu.

Usiridhike na hali uliyonayo kwani ikiendelea zaidi inaweza kuwasababishia migogoro ktk ndoa yenu, sbs kuu ikiwa ni UMBALI unaowafanya mshindwe kutimiza msingi imara wa ndoa ambao ni kuambatana na kuwa mwili mmoja.

Kwa upande wangu nakushauri yafuatayo;

Salini mara nyingi (muombeane ili vishawishi viwapitie mbali).
Dumisheni mawasiliano kwa lengo la kufarijiana.
Amueni pamoja na kwa ujasiri kwa kile mnachokiona kitanusuru ndoa yenu na kuwarejeshea hali yenu ya kuishi pamoja,Asikudanganye mtu NDOA NI TENDO LA NDOA,mengine yanafuata kama kweli mnapendana na mmeamua kuishi pamoja milele.
Epuka na kuwa makini na watu wako wa karibu hasa huyo Boss wako anayekutolea maneno ya kukukatisha tamaa, na kamwe usikate tamaa ona kama ni jaribu la kupita tu.(kumbuka sio kila m2 anafurahia ndoa yenu)
Mwisho, kumbuka atafutaye hachoki......hivyo endelea kuwaomba wakuhamishe kituo naamini watakutimizia kwa kadri ya maombi yako wasisitize bila kukata tamaa, lakini pia huku ukiwa unatafuta kazi nyingine na Mungu awatangulie kwa yote .
 
Back
Top Bottom