Ushauri tafadhali nataka kulinda ndoa, kazi kikwazo kikubwa

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
"Jamani naitaji msaada mkubwa sana, wa mawazo na saikolojia. Mimi nina mke nimezaa nae. Tangu tufunge ndoa ni miaka 4 sasa.yeye yuko Mkoani mimi niko chuoni Dar es Salaam kimasomo elimu ya juu". By Kipusy

Maneno ya utangulizi wa thread ya ndugu yetu Kipusy kwa yaliyomkuta. Ndoa yangu ina miaka 4 na mtoto 1 na Wife yupo Dar kikazi wakati mimi nipo Mkoani kikazi pia. Tatizo tunalojaribu kukabiliana nalo ni kukwepa majaribu yanayotokana na umbali kati yetu. Hata hivyo kwa nature ya kazi zetu ni mimi tu mwenye uwezekano wa kuhamia Dar kwani mwajiri wa mwenzangu hana ofisi huku mkoani.

Nimejaribu kumshawishi mwajiri wangu anirudishe karibu na familia lakini dalili za kufanikiwa hivi karibuni hazionekani, labda baada ya miaka mitatu hivi. Kwa upande wangu nimechoshwa mno, mno na maisha haya ya kuwa Modified bachelor hasa ukizingatia matatizo ya ndoa za siku hizi.

Naomba ushauri wenu nifanye nini kati ya haya yafuatayo?
1 Kuomba uhamisho ambao nimeshaona mafanikio yapo mbali sana kwa sasa?
2.Kuomba kuhamia kwa mwajiri mwingine mwenye nafasi?. Hili nalo litakuwa gumu zaidi kwani sio rahisi kupitishwa kwa barua yangu ya uhamisho.
3.Nitautafute kazi nyingine serikalini (niliko) au taasisi binafsi ili nisogee jirani na familia au
4.Niendelee kulinda kibarua huku nikihatarisha ndoa yangu hasa ukizingatia tangu siku ya harusi hatujafanikiwa kuishi miezi zaidi ya 6 pamoja huku kila mwezi tukipoteza nauli kusafiri safiri?

Najua humu jamvini kuna watu wenye uzoefu mbalimbali hivyo natarajia nitapata ushauri utakaoniwezesha kufanya maamuzi.

Nawasilisha
 
Pole sana mkuu, maamuzi yanayokukabiri ni magumu sana hivyo nitarudi baadaye.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
  1. je wewe uko mkoa gani???
  2. kati yako na mkeo yupi ambaye security ya kazi ni kubwa (pato)
  3. je nani ana uwezekano mkubwa wa kupata kazi kati yenu??
 
Tafuta kazi nyengine huku ukiendelea na kazi yako ya sasa kwa kuanzia
 
  • Thanks
Reactions: SG8
  1. je wewe uko mkoa gani???
  2. kati yako na mkeo yupi ambaye security ya kazi ni kubwa (pato)
  3. je nani ana uwezekano mkubwa wa kupata kazi kati yenu??

  1. Haya maswali ni ya msingi sana, kama ukiyajibu, nitakuwa kweye nafasi nzuri ya kukushauri............. lakini pia na mimi niulize swali la nyongeza, Je mwenzio anaonekana kukerwa na kutokuishi kwenu pamoja kama wanandoa, au anachukulia powa tu?
    Kama ukijibu hayo maswali yote na hilo la nyongeza nadhani sio mimi tu, bali wadau wengine humu jamvini watakuja na ushauri mzuri tu.
 
Haya maswali ni ya msingi sana, kama ukiyajibu, nitakuwa kweye nafasi nzuri ya kukushauri............. lakini pia na mimi niulize swali la nyongeza, Je mwenzio anaonekana kukerwa na kutokuishi kwenu pamoja kama wanandoa, au anachukulia powa tu?
Kama ukijibu hayo maswali yote na hilo la nyongeza nadhani sio mimi tu, bali wadau wengine humu jamvini watakuja na ushauri mzuri tu.
[/LIST]
Wote wawili tunakerwa sana na hali hii. Siku niliyopata barua ya kupangiwa kituo huku Mkoani mwenzangu alilia usiku kucha. Na hata kuja kunitembelea afadhali mimi naweza kupitisha miezi mitatu lakini yeye anaweza kuja mara mbili kwa mwezi.
 
Nilifikiri magumu kwangu tu, kumbe na kwako?

Kwa situation kama hio hapo juu, kutoa ushauri ni rahisi but na Imagine ndo yamenikuta na ndo inatakiwa nifanye maamuzi - inakua ngumu saaana.
 
  1. je wewe uko mkoa gani???
  2. kati yako na mkeo yupi ambaye security ya kazi ni kubwa (pato)
  3. je nani ana uwezekano mkubwa wa kupata kazi kati yenu?
1.Niko Mbeya Mkuu,
2.kazi zetu wote zina security ila yake ina kibano zaidi kwa kuwa mwajiri anamlipia ada ya Masters so lazima atumikie miaka mitano na hakuna ofisi zingine huku mkoani,
3. Yeye ana nafasi zaidi hasa baada ya kupata shahada ya Pili lakini atatakiwa kumtumikia mwajiri wa sasa miaka 5
 
Kwa situation kama hio hapo juu, kutoa ushauri ni rahisi but na Imagine ndo yamenikuta na ndo inatakiwa nifanye maamuzi - inakua ngumu saaana.
Ok nipe ushauri wako basi ndugu yangu maana kichwa changu kimeelemewa kabisa.
 
Mkuu hapo kwa sasa wewe ndio unatakiwa utafute kibarua kingine maana kama wife ana mkataba wa kumtumikia mwajiri wake miaka mitano duh hapo pagumu
Wewe angalia uwezekano wa kupata another work hata mikoa ya karibu na wife kama arusha kule kulingana kazi yako
Ila ni mwajiri gani huyo asiyejua umuhimu wa mke na mume au familia kukaa pamoja
 
Maisha ni changamoto, hiyo hali wa kuibadili ni wewe!! Acha uoga fanya maamuzi naimani kazi zipo nyingi ukianza mchakato saizi kufikia mwakani unaweza kupata kazi ambayo itakutoa kifungoni. Ndoa zinaathiri sana watu wengi tena wengi sehemu mbali mbali duniani. Kwa hiyo wewe, una bahati ya kuwa na mke ambaye hamjagombana kutokana na hilo. Fanya juhudi uwe naye karibu.
 
Hujajibu swali la msingi iwapo mwenzako anaichukuliaje hali hii ?
Mkuu nimejibu hapo juu kwamba siku nilipopata barua ya kuja mkoani Mwenzangu alilia usiku kucha na hata sasa hivi yeye ndie anayepiga trip za Mkoani walau twice a month. Infact anaumia sana hadi huruma japo inatuathiri wote wawili vibaya sana
 
Maisha ni changamoto, hiyo hali wa kuibadili ni wewe!! Acha uoga fanya maamuzi naimani kazi zipo nyingi ukianza mchakato saizi kufikia mwakani unaweza kupata kazi ambayo itakutoa kifungoni. Ndoa zinaathiri sana watu wengi tena wengi sehemu mbali mbali duniani. Kwa hiyo wewe, una bahati ya kuwa na mke ambaye hamjagombana kutokana na hilo. Fanya juhudi uwe naye karibu.
Asante sana Mkuu RD kwa ushauri, nakubaliana sana na wewe ndoa zinasumbua sana. Be blessed
 
1. tuliza akili yako usidanganyike ukaacha kazi kwa ajili ya kumfuata mwenzio.....ni kosa kubwa sana la kiufundi.hata yeye asiache kukufuata.fikiri kwa makini mfano unatoa notice,unaenda unamfumania,au ana mimba isiyo yako,kazi huna na mke huna.
2.msumbue mwajiri kila siku,kuna siku ataelewa.kama boss wako hataki waone wakubwa zake.usitangulize haiwezekani
3.umbali peke yake hauhatarishi ndoa,kuna hatari kibao hata kama mko ofisi moja na mkeo.
 
Mkuu hapo kwa sasa wewe ndio unatakiwa utafute kibarua kingine maana kama wife ana mkataba wa kumtumikia mwajiri wake miaka mitano duh hapo pagumu
Wewe angalia uwezekano wa kupata another work hata mikoa ya karibu na wife kama arusha kule kulingana kazi yako
Ila ni mwajiri gani huyo asiyejua umuhimu wa mke na mume au familia kukaa pamoja
Dah Arusha tena? Mbona kama hakuna tofauti sana na Mbeya? Labda ungesema Moro au Kibaha. Waajiri wetu ni balaa tupu Kaka. Unakutana na Afisa Utumishi aliyezoea kazi anakwambia "chagua Mke au kazi"
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom