Ushauri: Somo la Ujasiriamali liongezwe katika Mitaala ya viwango vyote vya Elimu

Jul 16, 2021
2
2
Ninaishauri serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kuanzishwa kwa mtaala wa ujasiriamali katika kila level, ili iweze kuwasaidia vijana wengi pindi wanapomaliza au kuhitimu mafunzo mbalimbali waweze kukabiliana na hali ya maisha watakayokutana nayo bila kutegemea ajira kama njia pekee ya mafanikio.

Hivyo kutasaidia sana kuwaweka vijana sawa kiakili, kimawazo na kisaikolojia.

Pia somo hili litawasaidia vijana wengi kutambua vipaji walivyonavyo tangu elimu ya msingi hadi chuo na jinsi ya kuviendeleza ili kuweza kuwapatia kipato pasipo kutegemea ajira tu kama njia pekee ya mafanikio.

Asanteni
 
Back
Top Bottom