Ushauri : Simba isijaribu kuidharau Yanga , kuna wakati Marehemu hupiga chafya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,643
218,099
Hili ni angalizo ninalolitoa kwa Timu yangu ya Simba , Tusithubutu kudharau yanga kwa sababu ya dhiki waliyonayo , tutaumia ! Inapofika siku ya mazishi Masikini wanakuwa na umoja wa ajabu sana !

Hebu angalia Buguruni kwa Mnyamani au Temeke Mikoroshini jinsi masikini wanavyozikana , hawajawahi kushindwa kumsitiri Marehemu , hata ukiangalia game ya Arsenal vs Man U wacheza kamari wengi waliweka mzigo kwa Manchester United na mikeka kibao ilichanika .

Tuingie kwenye game tukiwa makini sana , vinginevyo tutachapana bakora .
 
kama ulisikia mahojiano ya kocha wa simba aliongea kwa tahadhari tofauti na kocha wa yanga ambaye alikuwa anajitapa simba waje hata leo ni mechi ambayo ina pressure kubwa ila kwa sasa simba benchi lao laa ufundi ni kubwa watakuwa wamewaandaa wachezaji kisaikolojia kuhimili pressure ya pambano
 
Ukiangalia kwa umakini hii game Simba imeicheza vizuri sana,haina kelele kabisa,wanaopiga kelele ukiangalia kwa sana ni mashabiki wa Yanga,Simba inaonekana imeshachukua tahadhari kwenye hii mechi,hata Manara,hajaongea shit zake kama kawaida yake,yanga isiwaunderate Simba
 
Kwani hapa underdog ninani? Kesho tunaweza kushangaza ulimwengu mkija kichwa kichwa. Idumu daima Yanga.
 
Yanga tunawaheshimu, ila ni lazima tuwafundishe hawa wanywa gahawa mpira.
 
Kuna kila dalili ya Yanga kufungwa. Labda Mkwasa abadili mfumo. Huu mfumo wa 4 5 1 hauwezi kuipa timu ushindi maana wachezaji wenyewe ni wazito na wako taratibu sana kwenye kufanya Counter Attack kama mfumo unavyotaka.
 
Back
Top Bottom