Ushauri: Sijapata mtoto kwenye ndoa nahitaji wa kuzaa naye nje. Naumia kwa msongo wa mawazo (Depression)

Natumai wote mu wazima wa afya .

Mimi ni kijana wa miaka 31 kwasasa na toka niko na miaka 25 nilikua na hamu sana ya kupata mtoto na kuwa na familia kiujumla. Kama unavyojua maisha ya ujana kuna ujinga na makosa mengi tunafanya, nikiri kwamba nilifanikiwa kuwapa mimba mabinti wawili katika mahusiano ya nyuma katika vipindi tofauti, ila wote walizitoa kitendo ambacho kiliniuma sana sababu ikiwa ni mapema kwao kuwa mama maana pia bado walikua wanasoma na walikua kwa wazazi wao hivyo waliogopa kuzalia nyumbani.

Mwaka juzi mwez wa 4 nilifanikiwa kufunga ndoa na mimi na mke wangu hatuja fanikiwa kupata mtoto.

Mke wangu huwa hormone zake hazija balance na inaweza kupita ata miezi mi 3 hajaona period. Tumeenda hospitali na kutumia madawa ya kienyeji ila bado haijakaa sawa.

Nampenda mke wangu sana na nina msapoti sana ila nimefika maali nakata tamaa maana pia umri wanguunasonga na ninaumia sana kutokua na wakuniita baba.

NAHITAJI WA KUZAA NAE KWA MASHARTI MADOGO TU.

Sijawai kuwaza kutoka nje ya ndoa yangu kwani mimi sio mtu wa wanawake sana na muda mwingi nipo kimya na kwa umri wangu sasa sio mtu wakufikiria pisi bali kujenga familia.

Nahitaji mdada wa kuzaa nae tu ata mtoto mmoja tu na mimi niitwe baba maana kuna wakat nawaza napambana sana kutafta pesa ila namtaftia nani kama sina mtoto.

Niko tayari kumuudumia yeye na mtoto na tutapanga malezi ya uyo mtoto kwa kadri ya makubaliano yetu. Kipato changu sio kikubwa sana ila kinatosheleza mahitaji ya msingi na kufanya maendeleo.

Kwetu tumezaliwa wa tatu, wanaume wawili na msichana mmoja na ndugu zangu wote wamebaatika uzao wa mapacha. Natamani sana namimi nishike wangu

Kwasasa nina miradi niliyo wekeza na nahitaji kuwa na warithi (watoto) maana maisha haya hatujui wakati gani unadondoka.

Kimuonekano mimi ni mrefu, maji ya kunde na kitaaluma mimi ni IT. Aina ya mdada ambaye ningependa kuzaa nae awe tu ni mature, mwenye malengo, msikivu na anayependa kujishughulisha. Asizidi miaka 30

Kama upo tayari please nitumie message kupitia telegram kwa kubonyeza link apo chini or njoo inbox apa apa jf.

Nina mengi ya kuandika kwa hali ninayopitia ila naomba niishie apa kwa leo.
View attachment 2233943
Kuna sababu Mungu hajakupa mtoto au kizazi, Kama una imani pokea ulicho nacho kwa mikono miwili na wacha kutafuta kitu kwa za haramu. ukitajirika na huna mtoto wakuzaa, kuna watoto wengi wanaohitaji misaada, saidia yatima. Jenga visima vya maji kwa wana vijiji masikini
 
Usijaribu kufanya hivyo. Itaku cost.
JIULIZE - Ingekuwa ni wewe una hiyo shida na mkeo afanye hivyo ungekubali? Usiwe mbinafsi wewe. Tafuteni suluhu ya tatizo kwa pamoja bila kuchoka.

Kwa muda uliokaa kwenye ndoa ni mdogo sana kwa wewe kuanza kuwa na pressure, kuna workmate wangu alikaa 15yrs na bado akaja kubarikiwa watoto wawili.
 
Natumai wote mu wazima wa afya .

Mimi ni kijana wa miaka 31 kwasasa na toka niko na miaka 25 nilikua na hamu sana ya kupata mtoto na kuwa na familia kiujumla. Kama unavyojua maisha ya ujana kuna ujinga na makosa mengi tunafanya, nikiri kwamba nilifanikiwa kuwapa mimba mabinti wawili katika mahusiano ya nyuma katika vipindi tofauti, ila wote walizitoa kitendo ambacho kiliniuma sana sababu ikiwa ni mapema kwao kuwa mama maana pia bado walikua wanasoma na walikua kwa wazazi wao hivyo waliogopa kuzalia nyumbani.

Mwaka juzi mwez wa 4 nilifanikiwa kufunga ndoa na mimi na mke wangu hatuja fanikiwa kupata mtoto.

Mke wangu huwa hormone zake hazija balance na inaweza kupita ata miezi mi 3 hajaona period. Tumeenda hospitali na kutumia madawa ya kienyeji ila bado haijakaa sawa.

Nampenda mke wangu sana na nina msapoti sana ila nimefika maali nakata tamaa maana pia umri wanguunasonga na ninaumia sana kutokua na wakuniita baba.

NAHITAJI WA KUZAA NAE KWA MASHARTI MADOGO TU.

Sijawai kuwaza kutoka nje ya ndoa yangu kwani mimi sio mtu wa wanawake sana na muda mwingi nipo kimya na kwa umri wangu sasa sio mtu wakufikiria pisi bali kujenga familia.

Nahitaji mdada wa kuzaa nae tu ata mtoto mmoja tu na mimi niitwe baba maana kuna wakat nawaza napambana sana kutafta pesa ila namtaftia nani kama sina mtoto.

Niko tayari kumuudumia yeye na mtoto na tutapanga malezi ya uyo mtoto kwa kadri ya makubaliano yetu. Kipato changu sio kikubwa sana ila kinatosheleza mahitaji ya msingi na kufanya maendeleo.

Kwetu tumezaliwa wa tatu, wanaume wawili na msichana mmoja na ndugu zangu wote wamebaatika uzao wa mapacha. Natamani sana namimi nishike wangu

Kwasasa nina miradi niliyo wekeza na nahitaji kuwa na warithi (watoto) maana maisha haya hatujui wakati gani unadondoka.

Kimuonekano mimi ni mrefu, maji ya kunde na kitaaluma mimi ni IT. Aina ya mdada ambaye ningependa kuzaa nae awe tu ni mature, mwenye malengo, msikivu na anayependa kujishughulisha. Asizidi miaka 30

Kama upo tayari please nitumie message kupitia telegram kwa kubonyeza link apo chini or njoo inbox apa apa jf.

Nina mengi ya kuandika kwa hali ninayopitia ila naomba niishie apa kwa leo.
View attachment 2233943
If in any way you happen to see this through. Rafiki yangu, nakuahidi, Haitakuwa mwisho wa 'depression' . This will no way be your happy ending.
a) Kwenye vita anayesaliti kikosi anakuwa mhaini na kuna laana zinaambatana naye. You are married to your wife and by your choice. Kipindi hiki ni kigumu kwenu (Yes, especially for her), ni kama mko vitani. Na wewe unataka kuchomoa betri. Hakuna baraka huko uendako.
b) Umesema una mali unataka watoto wa kuwaachia. I can assure you sio wote waliokufa wakimiliki mali nyingi zilifanikiwa kufika kwa watoto walioowaacha.

USHAURI: Kama hii habari yako ni ya kweli. Omba Mungu, Mpende mkeo. Mtabarikiwa kinachowastahili. Na kama Mungu atachelewa kuwabariki, sisi ni binadamu tu. Hakuna tulichompa Mungu imlazimu kuturudishia. You can not inherit blessings in the world of God by going against Him. Usingebarikiwa mali speed yako ya kutafuta watoto ingekuwa hivi?
 
Hiyo presha ya kuwa na mtoto ni yako au ni ya ndugu zako???Tuanzie hapo kwanza...Kama ni ya ndugu yaani external pressure basi amini unaenda kuua ndoa yako iwapo lengo lako litatimia...Maana presha hiyo hiyo itaibukia upande wa uliyezaa nae kuwa huyu ndio anafaa maana katuletea uzao na utabaki njia panda tena...It's not such simple...Fikiria vizuri hasa presha inatoka wapi...Kama ni presha yako mwenyewe angalu utaweza kupambana nayo...mtizamo
 
Kwa mazingira haya na mengine Uislamu ukaja na utaratbu mzuri xn wakuoa mke zaidi ya mmoja ili usizini, ona xx unataka kufanya dhambi ya usaliti, kuwa makini usije ukakosa mke wa huyo mtoto. Kwanza watoto wenyewe wa siku hizi ni watoto basi ahh tabu tupu, si watoto ni kokoto. Badili dini then oa mke mwengine kisheria wala hutojificha.
 
Mkuu usikate tamaa mbona wengi wanapitia changamoto kama zako lakini Mungu huwakumbuka.

Mimi baada ya kuoa nilikaa miezi 8 hivi hola japo kila mwezi wife ana bleed na tunatiana mwanzo mwisho, ikabidi niende hapo rabinisia hospital nikapewa dawa za kuimalisha sperm lakini wapi ikagoma, nikahama hospital nikaenda kairuki Kwa doctor mmoja maarufu kama Piere akamuandikia dawa ( nakumbuka ilikuwa kama lectrozole kama sijakosea) wife vidonge 5 nikalipia 10K, huwezi amani wife alimeza na mwezi huo huo akanasa.
Mbaya zaidi tukaona tusitumie majira Bali tutumie kalenda kutokana na changamoto tumeopitia yaani mtoto Ile kafika miezi 6 akanasa nyingine, hapa hata hamu Sina tena ya kutaka watoto.
Mambovip mkuu
 
Kwa kuwa wewe ulishawajaza mimba wasichana, wewe una uwezo ila tafuta hosipitali yenye mabingwa wa magonjwa ya akina mama mkeo akapimwe. Nakusihi usichepuke mpaka upate majibiu ya daktari.
 
Usihangaike sana ,Mungu atawapa double double , hormonal imbalance sio tatizo permanent kiasi cha kutaka kwenda nnje .
Kuhusu umri usikupe mawazo kilakitu ni mipango ya Mungu
 
Nenda kijinini tafuta pisi kali itakayo kufit matie mimba mwandalie kila kitu rudi mjini jikaushe , low cost
 
Back
Top Bottom