superwarkills
Senior Member
- Aug 18, 2014
- 136
- 83
Carola Daniel A. Kinasha ni mwanamuziki wa Tanzania anayefanya muziki wa Asili na akichanganya na usasa, Mwanamama Carola alizaliwa miaka ya 60 katika kijiji cha Longido.
Alianza kujishughulisha na muziki mnamo miaka ya 80 rasmi ikiwa ni mwaka 1988, akijifunza zaidi kupiga gitaa.
Carola Kinasha ni mwanamuziki ambaye anaamini kuwa ili tasnia ya sanaa ya Tanzania iweze kukua na kujulikana kimataifa ni muhimu kurejesha elimu ya sanaa kwenye shule zetu. Pia kuwa na sehemu za kufanyia shughuli za sanaa kwenye kila kitongoji,."anasema
Amekuwa mwalimu wa muziki na muimbaji wa matamasha ya kimataifa, akiwa pia ni mshiriki wa tunzo mbalimbali ikimo tunzo za MA AFRICA AWARD South Africa mwaka 2002, Carola Kinasha licha ya kuimba pia ni MC wa matamasha mbalimbali likiwemo Tamasha la Sauti za Busara na amekuwa akishiriki washa na makongomano mbali ya muziki yakiwemo yale ya kujadili haki za wanamuziki.
Mwanamama huyu ambaye kabila lake ni mmasai alipata elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, akichukua taaluma ya sanaa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor of Arts Degree in International Relations) alifanikiwa kuanzisha bendi yake mwishoni mwa miaka 1980 iliyofahamika kama Kinasha's Shada Band ikiwa na lengo la kutengeneza muziki wa halisi wa Tanzania, amewai kushiriki pia katika wimbo wa mjomba (Mrisho Mpoto)
Carola ana album ya Maono ambayo ni ya pili (2007) kabla ya album ya kwanza ya (UMOJA) iliyotoka mwaka 1997. Corola Kinasha pia ameshiriki filamu mbalimbali ikiwemo Documentary yake iliyotoka 2009 inayofahamika kama "Mwamba ngoma"
Carola Kinasha pia ni mratibu na msimamizi wa tamasha la Music Mayday linalofanyika kila mwaka.
Nadhani huyu kwa maoni yangu ndiye anafaa kuwa msemaji wa shirikisho la muziki, kwa kuwa anaujua muziki, anauishi, na anaufanya muziki.
Shirikisho mchagueni Carola Kinasha.
View attachment 2161201View attachment 2161202View attachment 2161203