Ushauri: Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ibadilishe taasisi hizi ziwe independent kwa asilimia 100

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,987
144,319
Mimi mpaka leo hii huwa nashindwa kupata logic ya mifuko hii kuendeshwa kwa style ambayo ni kama iko chini ya serikali wakati fedha za mifuko hii ni mali ya wananchama tena wanachama wengine wakiwa ni wafanyakazi wa sekta binafsi.

Nafikiri wakati umefik tubadili sheria kwa lengo la kuifanya hii mifuko kuwa ni taasisi zinazotijtegemea kwa asilimia 100 bila kuingiliwa na serikali kwa namna yoyote ile hata katika uteuzi wa wakurugenzi wa mifuko hii pamoja na wenyeviti na wajumbe wengine wa bodi wanaosimamia mifuko hii.

Hata taasisi ya kudhibiti mifuko hii (SSRA) sheria yake nayo itazamwe upya kama inatoa mwanya wa serikali kudhibiti mifuko hii kupitia SSRA basi nayo ifanyiwe marekebisho.

Haya mambo ya serikali na sasa chama tawala kukopa kutoka katika hii mifuko na kutorudishwa fedha kwa wakati bila shaka ni matokeo ya sheria inayounda na kusimami mifuko hii inayozifanya taasisi hizi kukosa nguvu ya kuidai serikali.

Ni wakati wa kubadili sheria ya uundaji wa hii mifuko na kuifanya mifuko hii iwe more independent.

Nimeshindwa kabisa kuelewa inakuaje mkopoji anakopa fedha kutoka katika hii mifuko kisha mkopaji huyo huyo anajilipa kwa kujihamishia fedha kama tweet ya Zitto kabwe akimnukuu CAG inayoeleza.
 
Back
Top Bottom