Ushauri: serikali zijengeeni simba na yanga uwanja halafu mzikate mapato

Rockcity native

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
2,167
1,403
Ni ushauri wangu kwa serikali ya mh kikwete kuzisaidia vigogo vya soka yani simba na yanga walau kuvijengea viwanja kama kirumba kila timu halafu kila mechi serikali ikate mapato ya timu husika hadi hapo deni litakapoisha... Nasema hivo kwa maana timu zetu hizi zimekosa mipango mikakati ya kujenga viwanja vyao. Kila siku viongozi wao ni blah blah tu. Simba na yanga ni tunu ya taifa iliyojificha. Kwa kufanya hivyo serikali itakua imevifungua macho vilabu hivi kukabiliana na haki miliki zake ambazo zinapotea katika mikono ya wajanja wachache kama jezi,majengo n.k
 
Kwanini hizo fedha wasinunue matrekta na kukodisha wakulima. Au wasikopeshe wanafunzi.
Ni wakati sasa timu zijiendeshe km kampuni
 
Yanga na Simba ni kama Vampire...hazina mwenyewe hata serikali ikijenga hivyo viwanja itamkabidhi nani? Au itawapa hao wanachama walioshindwa kusimamia hata majengo yao wenyewe yanayonuka?
 
mbali na ushabiki we utakuwa mnazi kwa kupenda maharagwe yaliyo chacha alaf ujambe kisha unuse arufu, watu wanajiandaa kufungiwa zenji ili watupe matokeo stahiki we unawaza upumbavu kama unawapenda waambie waende chamazi
 
Ni ushauri wangu kwa serikali ya mh kikwete kuzisaidia vigogo vya soka yani simba na yanga walau kuvijengea viwanja kama kirumba kila timu halafu kila mechi serikali ikate mapato ya timu husika hadi hapo deni litakapoisha... Nasema hivo kwa maana timu zetu hizi zimekosa mipango mikakati ya kujenga viwanja vyao. Kila siku viongozi wao ni blah blah tu. Simba na yanga ni tunu ya taifa iliyojificha. Kwa kufanya hivyo serikali itakua imevifungua macho vilabu hivi kukabiliana na haki miliki zake ambazo zinapotea katika mikono ya wajanja wachache kama jezi,majengo n.k

Mkuu,vilabu hivi vikongwe bado havijawa na muundo mzuri wa kiuongozi ndio maana,ukilinganisha na vilabu vingine hapa barani Afrika vilsb hivi viwili vipo nyuma.

Vilabu hivi vina washabiki na wanachama.lakini tatizo hakuna muundo unaweza kufanya wakapatikana viongozi watendaji,ambao wanaweza kuwatumia wapenzi na wanachama katika kupata mapato kutokana na chanzo hiki.na vilabu hivi hata maheasabu yao ninashaka kama zinakaguliwa.

Muda unavyokwenda vitakuja vilabu makini,na kufanya vilabu hivi aidha vijifunze au vinunuliwe na wenye pesa hapo ndipo utaona mabadiliko katika vilabu hivi viwili.

Kwa sasa uswahili ni mwingi sana katika hivi vilabu,unajua kuna watu wanatoa fedha zao kusaidia vilabu hivi na wala hatangazwi na matumizi ya fedha walizotoa hakuna mrejesho?!!

Vilabu hivi imekuwa ni daraja lawatu kujitafutia umaarufu na nafasi za kisiasa.
 
Serikali ivifunge viwanja vile viwili. Cha taifa na uhuru,vitugke kwenye mechi za kimataifa tu,tuone watachezea wapi.
 
kwani hiyo serikali yenu ina viwanja vingapi zaidi ya taifa na shamba la bibi (uhuru)??? acheni kuzitukana simba na yanga bila sababu za msingi
 
Mkuu,vilabu hivi vikongwe bado havijawa na muundo mzuri wa kiuongozi ndio maana,ukilinganisha na vilabu vingine hapa barani Afrika vilsb hivi viwili vipo nyuma.

Vilabu hivi vina washabiki na wanachama.lakini tatizo hakuna muundo unaweza kufanya wakapatikana viongozi watendaji,ambao wanaweza kuwatumia wapenzi na wanachama katika kupata mapato kutokana na chanzo hiki.na vilabu hivi hata maheasabu yao ninashaka kama zinakaguliwa.

Muda unavyokwenda vitakuja vilabu makini,na kufanya vilabu hivi aidha vijifunze au vinunuliwe na wenye pesa hapo ndipo utaona mabadiliko katika vilabu hivi viwili.

Kwa sasa uswahili ni mwingi sana katika hivi vilabu,unajua kuna watu wanatoa fedha zao kusaidia vilabu hivi na wala hatangazwi na matumizi ya fedha walizotoa hakuna mrejesho?!!

Vilabu hivi imekuwa ni daraja lawatu kujitafutia umaarufu na nafasi za kisiasa.

yote kwa yote mkuu, unasemaje kuhusu kukopeshwa viwanja kwa wakati huu ni sahihi au bado sana?
 
Back
Top Bottom