Ushauri: Serikali msitafute malumbano na upinzani yasiyo na tija

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,600
8,741
Raisi Samia anafanya makosa ambayo Hayati Magufuli na wapambe wake walifanya. Magufuli alifanya vitu vingine ambavyo havikuwa na tija kwa taifa.

1. Kubishana na Lissu kuhusu yeye kupigwa risasi ilikuwa haina tija. Haya ni malumbano ya kijinga kwasababu huwezi kujadili swala lililo wazi kama Lissu kupigwa risasi na ukashinda hoja kama wewe ni serikali. Hivyo Serikali ilitakiwa kunyamaza au kuomba msamaha badala yake hili swala limeitia historia ya Hayati doa kubwa ambalo haliwezi kufutika. Kuna washauri wanaofikiria kubishana kwenye kila kitu ni kushidwa badala ya kuangalia swala muhimu na kuangalia kwa upana wake litaishia wapi.

2. Kuiba kura hakujasadia CCM, Serikali wala nchi kwa ujumla. Tulishatengwa na mataifa, wafanyabiashara walishakimbia , sifa ya nchi iliondoka kwasababu tu ya kuzuia madiwani wa upinzani au wabunge 40 wa upinzani kati ya wabunge zaidi ya 300! huu ni ujinga wa hali ya juu kwa taifa. Ukijiuliza Tanzania tumenufaika nini kwa kuwa na wabunge feki hakuna cha kuonyesha. CCM imenufaika kwa kupata pesa karibu zote za ruzuku ambazo zitaenda kunulia viongozi wao magari huko wilayani lakini haya magari ukiuliza yanaleta vipi maendeleo ni ngumu kuona.

Raisi Samia kwenye hili swala la Mbowe serikali inafanya tena yaleyale ya Lissu. Watanzania wanamjua Mbowe kuliko Raisi Samia! kuanzia shule, familia yake, biashara zake na mapungufu yake. Huwezi kuwadanganya watu kwa mtu mashuhuri kama Mbowe!. Yaani familia ya mbowe inajulikana kuliko familia ya Rais Samia sasa leo ukija kuwaambia watanzania kwamba Mbowe ni gaidi Watanzania wanajua sio kweli.

Huwezi kusema mtu ni gaidi wakati ujumbe wake mkubwa kwa miaka zaidi ya 20 ni kutokulipiza visasi, huwezi kusema mtu gaidi wakati kwa miaka 20 akiwa kijana hakufanya ugaidi eti sasa ni mtu mzima aweze kufanya ugaidi sasa hivi!. Hivyo serikali inacheza mchezo ambao matokeo yake tunajua hayatakuwa mazuri kwa upande wa serikali.

Yaani kwa muda mfupi tu Rais Samia kuna watu wameshaanza kumuona tofauti kwa sababu ya Mbowe kwasababu watu wanamfahamu Mbowe. IGP na mwendesha mashitaka usije ukashangaa Mbowe ndiye akawapeleka kwenye kustaafu. Angalieni Sabaya kaishia wapi sio kwasababu ya Rais Samia pekee lakini angalieni wananchi hata wa CCM wanamgeuka. Nahauri Serikali ipinge vitu kwa hoja kama ni katiba wekeni hoja au nendendi kwenye midahalo na kuelezea ni kwanini huu sio wakati mzuri badala ya kushika na kufunga
 
Back
Top Bottom