Ushauri, Serikali itumie Tozo ya Mitandao ya Kijamii kwa ajili ya kupanga miji na kupima Ardhi

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
8,461
2,000
Habari zenu.

Nimesikia Waziri wa fedha anapanga kutafuta namna ya kupata tozo kwenye mitandao ya kijamii.

Kama hili likiwezekana natoa ushauri kwa serikali kutumia fedha hizo kuunda wakala wa Ardhi na mipango miji.

Kazi hii imekuwa inafanywa na Halmashauri lakini zimeshindwa kupima viwanja vya kutosha,kulipa fidia,kupanga matumizi bora ya ardhi na kutatua migogoro.

Kana kwamba haitoshi Serikali ikahamishia hiyo Idara Wizarani na mikoani lakini bado hakuna kinachofanyika.

Shida kubwa hapo ni upatikanaji wa pesa.Sasa kama wakipata fedha huko waunde hiyo wakala kwa ajili kusimamia matumizi sahihi ya ardhi na mipango miji kote Vijijini na mijini.

Hawa ndio watasimamia utoaji vibali vya ujenzi nk.Ni aibu kuona nchi yote takribani 80% ni slums tupu.Habari za kulasimisha makazi nk vyote viratibiwe na Hiyo Agency.

Serikali imefaulu na kuwa na ufanisi kupitia wakala na mamlaka za serikali kuliko kuwa centrallised.Hii ni njia ya ugatuzi.

Kama wameweza kwa kutumia wakala kama Tanroads, Tarura, Ruwasa,TRA,TBS,Bandari,REA nk ,ni vyema na suala la Ardhi na mipango miji ikawekewa wakali na chanzo chake maalumu cha fedha.

Hili wazo limfikie Waziri wa Ardhi na Waziri wa fedha.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,792

Kwani Bashe au Slaa wanasema je kuhusu mapato lukuki yanayohitajika bungeni?

Labda waongeze kodi kwenye luku. Huku kwingine ambako ikibidi tutarudi kutumia radio for free, Madelu anasubiri sana.

Hakuna miamala hapa!

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
8,461
2,000
Kwani Bashe au Slaa wanasema je kuhusu mapato lukuki yanayohitajika bungeni?

Labda waongeze kodi kwenye luku. Huku kwingine ambako ikibidi tutarudi kutumia radio for free, Madelu anasubiri sana.

Hakuna miamala hapa!

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
Huwezi kwepa teknolojia utakachofanya ni kupunguza matumizi tuu.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,792
2,000
Huwezi kwepa teknolojia utakachofanya ni kupunguza matumizi tuu.
Ndiyo kukwepa kwenyewe huko.

Kwa kunyang'anyana mchana kweupe, kabla ya kumwuunga kikamilifu huyu mwamba:

IMG_20210901_201456_008.jpg

itakuwa ni haki yetu kufanya lolote kumnyima awaye yote pesa za wizi.
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
8,461
2,000
Ndiyo kukwepa kwenyewe huko.

Kwa kunyang'anyana mchana kweupe, kabla ya kumwuunga kikamilifu huyu mwamba:

View attachment 1920071

itakuwa ni haki yetu kufanya lolote kumnyima awaye yote pesa za wizi.
Huna ujasiri kama wasomali unfortunately ni wachache sana,by the way si umeona ajira za mapolisi ? Badala ya kulia Lia humu changamkia fursa Ili upambane na stress.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,792
2,000
Huna ujasiri kama wasomali unfortunately ni wachache sana,by the way si umeona ajira za mapolisi ? Badala ya kulia Lia humu changamkia fursa Ili upambane na stress.

Stress nilisha maliza muda kupambana nazo.

Wewe ungali huko?

"Ajira @tanpol heri nibebe zege" -- Jembe Ulaya.
 
thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,526
2,000
Naomba ufafanuzi kuhusu hizi tozo

Serikali itatoza kampuni husika mfano (FB, Twitter, Google nk) au wanatoza mtumiaji?
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
8,461
2,000
Nchi yetu ilipofikia haiwezekani pangwa

Sent using Jamii Forums mobile app
By 2035 idadi ya watu itakuwa around mil.72-75 tunaweza kupanga kwa sababu tunaanza kujenga na kupanga Miji nje ya Miji slums,kiufupi uendelezaji wake utafanyika kwenye surveyed plots.

Pia tunajenga satellite cities huku tukipunguza uswazi kwa kuvunja kuwafidia maeneo waendenje ya Mji au kujenga apartment blocks na kuweka watu humo.

Inawezekana kabisa mkuu shida ni pesa,unaposema haiwezekani kwamba nchi itakuwa hivi hivi hadi siku Dunia inapinduliwa au?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom