Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Kujiajiri mtandaoni ni field inayokuwa kwa kasi sana. Na malipo yake kwa standard zetu ni mazuri. Yanaanza dola moja hadi kumi kwa saa. Uwekezaji mkubwa wa mtu kufanya kazi hizi ni internet na vifaa vya kazi, hasa kompyuta.
Vijana waliomaliza vyuo wanaujuzi mbalimbali wa kufanya kazi hizi. Na kazi ni nyingi sana sababu malipo haya kwa nchi za wenzetu yanaonekana ni kidogo, hivyo kunakuwa hakuna ushindani wa kugombania kazi.
Serikali isaidie kwa kuwapatia internet watu na eneo la kufanyia kazi. Kuna maeneo kama viwanja vya nane nane au saba saba hukaa wazi mwaka mzima. Mfano pale Mbeya, majengo ya uwanja wa nane nane ni mazuri sana na huwa wazi kama miezi 11 hivi.
Serikali ingeweka internet ya bure na kufanya utaratibu vijana kutumia majengo yale, ingewawezesha kujiajiri. Na hili si mpaka serikali kuu, serikali za miji na majiji zinaweza kufanya kitu hicho.
Mnaonaje suala hili?