Ushauri: Serikali itengeneza internet hotspot za bure ili vijana waweze kujiajiri kama Freelancers mtandaoni

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,285
2,000
Kujiajiri mtandaoni ni field inayokuwa kwa kasi sana. Na malipo yake kwa standard zetu ni mazuri. Yanaanza dola moja hadi kumi kwa saa. Uwekezaji mkubwa wa mtu kufanya kazi hizi ni internet na vifaa vya kazi, hasa kompyuta.

Vijana waliomaliza vyuo wanaujuzi mbalimbali wa kufanya kazi hizi. Na kazi ni nyingi sana sababu malipo haya kwa nchi za wenzetu yanaonekana ni kidogo, hivyo kunakuwa hakuna ushindani wa kugombania kazi.

Serikali isaidie kwa kuwapatia internet watu na eneo la kufanyia kazi. Kuna maeneo kama viwanja vya nane nane au saba saba hukaa wazi mwaka mzima. Mfano pale Mbeya, majengo ya uwanja wa nane nane ni mazuri sana na huwa wazi kama miezi 11 hivi.

Serikali ingeweka internet ya bure na kufanya utaratibu vijana kutumia majengo yale, ingewawezesha kujiajiri. Na hili si mpaka serikali kuu, serikali za miji na majiji zinaweza kufanya kitu hicho.

Mnaonaje suala hili?
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,285
2,000
Zikiwepo watabet na kustream u tube ,africa hatuna ustarabu huo ,kila mtu apambane tu kutoboa tupo uchumi wa kibepari km kazi yako inahusu internet utaipenda lazima bandle huwez kutegemea serikal

sent from HUAWEI
Haiwezi kuwa hivyo mkuu. Watu wanaotafuta ugali hawawezi kufanya hayo. Na hata hizo nchi za kibepari utakuta kuna maeneo yana free wifi. Yapo huko NY, Soul, Honh Kong nk. Mtu akipewa mafunzo kidogo juu ya freelancing na akiwa na uhakika wa internet atapiga kazi. Mwisho wa siku hizo pesa wanazopata Inarudi kuongeza mzunguko wa pesa mtaani.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,285
2,000
Wazo zuri sana hili mkuu, hivi ile project ya Coke Free wi-fi toka coca-cola liliishia wapi au bado linaendelea, maana ilisaidia vijana wengi sana kuhusu internet Japo wengi waliishia kupakua movies and porn

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Sijajua inaendeleje. Ila vijana wakielekezwa jinsi ya kupata pesa kupitia freelancing, na wakiiona pesa, hawawezi kuhangaika na porn.
 
KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
1,139
2,000
Haiwezi kuwa hivyo mkuu. Watu wanaotafuta ugali hawawezi kufanya hayo. Na hata hizo nchi za kibepari utakuta kuna maeneo yana free wifi. Yapo huko NY, Soul, Honh Kong nk. Mtu akipewa mafunzo kidogo juu ya freelancing na akiwa na uhakika wa internet atapiga kazi. Mwisho wa siku hizo pesa wanazopata Inarudi kuongeza mzunguko wa pesa mtaani.
Nimekaa sana ujeruman ,ni kweli kuna free wif but zina condition na ni limited kwa baadhi ya matumizi ,Africa hakuna nchi iliyofikia hiyo level wala serikal haiwez kudgubutu kwa kuwa freelencer ni kazi ambayo haitambuliki serikali , haijaraaimishwa

sent from HUAWEI
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,285
2,000
Nimekaa sana ujeruman ,ni kweli kuna free wif but zina condition na ni limited kwa baadhi ya matumizi ,Africa hakuna nchi iliyofikia hiyo level wala serikal haiwez kudgubutu kwa kuwa freelencer ni kazi ambayo haitambuliki serikali , haijaraaimishwa

sent from HUAWEI
Mambo mengi tu hayajarasimishwa mkuu. Na ukitaka kurasimisha freelancing lazima utaharibu. Ni kama ukitaka kurasimisha kazi ya uyaya. Asilimia kubwa ya wafanyakazi nchi hii wanafanya sekta isiyo rasmi. Cha msingi hapa serikali isaidie vijana kujipatia kipato

Na kusema hakuna serikali Africa imaweza kufanya nakataa. Serikali imeweza kuprovide free Wi-Fi vyuoni. Unakuta Campus nzima ina free internet. Na sometimes hazina limitation yoyote. Inaweza fanya kitu kama hicho ili kutengeneza ajira.
 
Vyuoni ni muhimu kufanya hivyo sababu ni kurahisisha source of acceas material na sio kwa ajili ya free lancer eti vijana wajiajiri hiyo ni ndoto kaka

sent from HUAWEI
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,285
2,000
Vyuoni ni muhimu kufanya hivyo sababu ni kurahisisha source of acceas material na sio kwa ajili ya free lancer eti vijana wajiajiri hiyo ni ndoto kaka

sent from HUAWEI
Siyo ndoto mkuu ni nia tu. Na return yake kwenye uchumi inaweza kuwa kubwa mara nyingi ya gharama ya serikali. Freelancing inakuwa kwa kasi sana. Itafika siku majority ya watu duniani watakuwa wameajiriwa huko.
 
Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
16,833
2,000
Na hivi mitandao pendwa imefungiwa.

Huenda kweli MB za serikali zikatumika vizuri sio kuangalia picha za X na kunyetuka tu.
 
Patra31

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
3,659
2,000
Nimekaa sana ujeruman ,ni kweli kuna free wif but zina condition na ni limited kwa baadhi ya matumizi ,Africa hakuna nchi iliyofikia hiyo level wala serikal haiwez kudgubutu kwa kuwa freelencer ni kazi ambayo haitambuliki serikali , haijaraaimishwa

sent from HUAWEI
Kama sijakosea visiwa vya shelisheli katika ya mji mkuu wao kuna hii huduma.
 
pmama

Member
May 8, 2021
30
95
Yan nimeingia upwork ku bid project kabla sijamaliza chochote bando langu la buku limekata ...kama kweli kungekua na free bando ni kweliingesaidia kwa baadhi ya watu.....
 
Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
4,131
2,000
Nchi za kiafrika viongozi wanajua tozo tu na vijana mjiajiri huku wao miaka zaidi ya 20 wameajiriwa.
Mm hata hiyo free wifi hotspot siitaki. Waruhusu PAYPAL tu hayo mengine nitafanya mm mwenyewe.
 
Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
980
1,000
Yan nimeingia upwork ku bid project kabla sijamaliza chochote bando langu la buku limekata ...kama kweli kungekua na free bando ni kweliingesaidia kwa baadhi ya watu.....

Sasa mkuu una bid kazi ya kukupa Laki lakin kutoa buku 5 kununua bando hutaki kweli ?
 
Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
4,131
2,000
Hii nchi kwenye sekta muhimu yamejazana mazee tu hayajui lolote. Lenyewe linajua kazi ni kulima tu.
Kutoa hela paypal inapitia kwenye simu au mabenki yalivyokuwa hayana akili yanawaza utakatishaji fedha tu.
Huwa natamani sana ningekuwa mzaliwa wa Kenya
Kuishi kwenye nchi ya dunia ya 3 haina tofauti na kuishi kuzimu
Paypal iruhusiwe
Mnakubali kushindwa na manyang'au
Waambie waache uzamani.
 
GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
3,027
2,000
Hii nchi kwenye sekta muhimu yamejazana mazee tu hayajui lolote. Lenyewe linajua kazi ni kulima tu.
Kutoa hela paypal inapitia kwenye simu au mabenki yalivyokuwa hayana akili yanawaza utakatishaji fedha tu.
Huwa natamani sana ningekuwa mzaliwa wa Kenya
Kuishi kwenye nchi ya dunia ya 3 haina tofauti na kuishi kuzimu
Hapa ndio wanapofeli sasa huwezi kukimbizana na dunia kwa mawazo ya kizamani,vitu vidogo vinashindikana sasa vikubwa itakuwa ndoto mkuu.
Kenya wako mbele yetu sana
Mkuu nyumbani ni nyumbani tu...siku moja mambo yatabadilika tukipata viongozi wenye muono jicho la tatu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom