Ushauri: Serikali ijenge ofisi za makao makuu kwa kila chama cha upinzani kilichoasisiwa 1992

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Kwa sababu wakati mfumo wa vyama vingi vya siasa ukianza rasmi 1992 CCM ilibahatika kurithi mali zote ilizozimiliki wakati wa mfumo wa chama kimoja ambazo kimsingi zilikuwa ni mali za watanzania wote.

Ikumbukwe kuwa vyama vya upinzani 1992 viliundwa na wanaccm wenye mawazo mbadala na hiyo haikuwa dhambi.

Nashauri serikali sikivu kupitia Tozo za kizalendo ziwafute machozi wanasiasa hawa kwa kuwajengea ofisi bora kwani vyama vya siasa ni mali ya Umma.

Na ikiwapendeza, chama kikuu cha upinzani Chadema wajengewe jengo la ghorofa 7 tofauti na ile Jogoo house ya TLP.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom