Ushauri: Serikali ijenge Mall eneo lililobaki baada ya ujenzi wa Stendi ya Kijichi

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,448
2,000
Habari wadau!

Jana nilipata nafasi ya kwenda wilaya ya Temeke kupiga misele baada ya jamaa yangu kuniomba nimtembelee nikapafahamu anapoishi kule Mtoni Kijichi Temeke.

Binafsi kutokana na taaluma yangu ya uhandisi ni mpenzi sana wa ubunifu wa kihandisi ,hivyo jamaa yangu aliniomba anitembeze maeneo yote ya Kijichi ambyo serikali imejenga miundombinu ya barabara na soko.

Kiukweli Kijichi inavutia sana kuliko sehemu yeyote ya wilaya ya Temeke yaani kama Masaki ndogo.

Ila kuna kitu ambacho niliona serikali ilibugi sana, ni lile soko na stand iliyopo pale Kijichi ambayo haitumiki badala yake imekuwa sehemu ya vijana kwenda kukutana usiku na watu wao na kama sehemu ya mazoezi.

Mradi hule wa soko umegharimu pesa nyingi sana lakini unaonyesha, ubunifu hule haukuendana na mahitaji ya wananchi na kufanya kugharimu pesa nyingi sana pasipo kuwa na impact yeyote kwa jamii na serikali.

USHAURI:
Nashauri serikali wajenge Mall kubwa kupitia muwekezaji kwenye eneo lililobaki itasaidia kuchangamsha eneo husika na kuongeza mapato.

IMG_20210607_135028.jpg
 

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
971
1,000
Serikali katika mkoa inaweza fanya, kinakuwa chanzo cha mapato. Sio Serikali kuu.

Sijui kama hilo eneo ni la serikali au lah ila kama sio la serikali bas tufanye mpango tujenge mall yetu sisi wenyewe watu wa private sector tukiwaruhusu sana serikali hawa jamaa wataanzisha ukiritimba kwenye mall za karibu
 

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
826
1,000
Hata mimi nimeshangaa sana kwenye hilo. Labda kama issue ni ardhi.

Kama eneo ni prime, ni wakati wa sekta binafsi kuchangamkia fursa.
Kwenye ofisi zote za serikali za mitaa Kata ya kijichi kuna picha ya mall ambayo inaonyesha itajengwa eneo la kijichi..na bila Shaka ni project ya serikali..ni mzuri Kwa mwonekano pia
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Kwenye ofisi zote za serikali za mitaa Kata ya kijichi kuna picha ya mall ambayo inaonyesha itajengwa eneo la kijichi..na bila Shaka ni project ya serikali..ni mzuri Kwa mwonekano pia
Kama vipi wafanye PPP.

Kama eneo lipo tayari ni wao kutafuta wadau tu.
 

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,448
2,000
Hata mimi nimeshangaa sana kwenye hilo. Labda kama issue ni ardhi.

Kama eneo ni prime, ni wakati wa sekta binafsi kuchangamkia fursa.
Eneo lipo kubwa sana na la wazi tazama picha vizuri utaliona mkuu.Soko limejengwa ushuani sana wakati wakazi wa eneo soko lilipojengwa ni washua kwa sana wazee wa kwenda kuhemea mall,kama walikuwa na mpango wa kujenga soko walipaswa kujenga mitaa ya ushwahilini changanyikeni kwenye waswahili wengi.
 

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,448
2,000
Soko tu limekosa biashara, hiyo mall itapata mteja y

Tunapenda mno kujimwambafai. Heri wangesema watu wajijengee vijiduka badala ya hicho wanachoita "mall".

Amandla...
Pale lilipo soko ni zaidi ya masaki boss ,ni kwa maboss man ,huwezi ukajenga soko la kuuza nyanya za kupanga kwenye meza hauwezi mpata mtu.Option ya mall kubwa yenye kumbi za cinema itawavuta washua na waushazi si unajua sisi watoto wa kishwahili hatupendagi dharau za kuachwa nyumba weekend lazima tukajimix cinema na vishopping vya kizushi hii itapelekea eneo lile kuwa busy sana😂😂
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom