Ushauri: RC Simiyu, David Kafulila fanya haya kuuendeleza mkoa

Mar 31, 2020
67
58
Mkuu Wa Mkoa mheshimiwa Kafulila, kwanza hongera kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, hiyo ni heshima kubwa kwa kuwa wengi walistahili ila wewe neema imekudondokea.

Mkuu wangu umepewa jukumu kubwa kuuongoza mkoa huu hasa ikizingatiwa mtangulizi wako alifanya mambo makubwa kwenye sekta za elimu,viwanda na kuutambulisha mkoa vizuri kwani mkoa huu ni mchanga kulinganisha na mikoa mingi ya Tanzania.

Mkuu wangu kuna mambo mengi ukiyafanya utaacha alama kubwa hata kumshinda mtangulizi wako mheshimiwa Mtaka

Mimi Leo nakupa mchache:
Kwanza ni kuufanya mkoa uvutie watu wengi has a kutoka maeneo jirani kama Mwanza, Musoma, Tarime, Shinyanga na hata Kahama

Kitu unachotakiwa kukifanya hakikisha Mkoa una vivutio vya kutengenezwa kama uwanja mzuri wa mpira, kumbi kubwa za burudani ili hata wasanii wavutiwe kuja kufanya matamasha mbalimbali.

Mbili hakikisha mji hasa wa Bariadi unajengwa kwanza vizuri kuliko kutawanya baadhi ya huduma mbali eti kwamba unapanua mji kama alivyofanya Mtaka. Huu ni mji mdogo hivyo jitahidi kuweka sekta karibu na mji sio kupeleka mbali. Mfano uwanja wa ndege ujengwe karibu na mji, Hoteli za kitalii zijengwe nyingi ili watu wanapokwenda Serengeti wavutiwe kuja kupumzika Bariadi mjini.

Tatu hakikisha lile soko la Jumanne linaboreshwa maana Halmashauri wameliacha tu bila kuwa na mipango ya kulifanya liwe la kisasa kwani lina watu wengi ambao huja kwa ajili ya kuuza na kununua bidhaaa hasa wanyama kama ng'ombe na mbuzi, watu hupata nyama choma ingawa haliendelezwi kuwa la kisasa.

Nne: Kuna mradi wa kujenga Soko la kisasa karibia na stendi ya Somanda, naomba uufuatilie ili kuboreshwa mji wetu.

Tano: Stendi ya Somanda isimamiwe vizuri kwani inashangaza, kuna vibanda vingi kwenye jengo hili lakini havitumiki. Nilipata taarifa kuwa vina bei ya juu sana so nawashangaa wahusika je ni bora kupangisha kwa bei ndogo ili upate hata kidogo au kuacha ukose kabisa?

Nawaomba wanaohusika wafikirie vizuri, ni aibu stendi kuwa doro hivyo

Vile vile magari yote yawe yanashushia stendi na kuegeshwa hapo ili kuichangamsha stendi. Hata hilo mpaka uende chuo kikuuu kufikiri! Ila kwa wahusika tumsaidie mkuu wetu.

Sita kuna eneo ambalo ni karibia na stendi ambalo wanasema ni la Ushirika, kiukweli ni aibu maana haliendelezwi lipo tu. Mimi nadhani ni wakati wakuwany'angany'a maaana mtu asipofikiria vizuri mpe anayefikiri vizuri.

Eneo hilo linawezwa kujengwa vihoteli, vipabu au vibanda ilikuweza kukusanya mapato na kuuongezea mkoa wetu fedha za kujiendesha.

Mwisho nikushukuru kwa juhudi unayoifanya hasa kwenye suala la pamba, Mungu akupe ujasiri utumikie kwa uaminifu na haki.

Mimi ni mkereketwa mzuri wa mkoa wa Simiyu
 
Back
Top Bottom