MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,447
Interest declaration: Mimi ni mfuasi wako, shabiki wako na nina imani na wewe sana kwa sababu ya dhamira yako njema. Mimi si mmoja kati ya wanaotarajia kudahiliwa maana nimemaliza hizo process miaka mingi sana.
Honestly speaking;
A: Tuliosoma wakati wa mfumo wa zamani wa udahili tunajua changamoto zake.
Kuomba nafasi ya chuo moja kwa moja kulikuwa na faida zifuatazo:
· Kupata nafasi kwenye chuo unachokipenda, Kupata nafasi kwenye kozi unayoipenda na kwa hiyo kuwa na utayari kisaikolojia kuvumilia mazingira hayo hata kama ni magumu.
Lakini kulikuwa na changamoto zifutatazo pia:
· Uwezekano mkubwa wa kukutana na ushindani wa hali ya juu wa ufaulu katika machaguo yote ya kozi unazozipenda hivyo kukosa nafasi kwa mwaka huo.
· Ili kukabiliana na changamoto hii, ilitulazimu kuomba nafasi zaidi ya chuo kimoja hivyo kulazimika kulipa gharama za udahili zaidi ya mara moja pamoja na usafiri. Ikitokea umechaguliwa vyuo vyote maana yake kuna wenzio wamekosa nafasi kwa kuwa umewashinda ufaulu hivyo basi umewapotezea nafasi zao katika hatua ya kwanza.
B: Mfumo wa CAS,
Faida
Kwa ujumla huu mfumo uliziondoa changamoto hapo juu kwa kiwango kikubwa sana ikilinganishwa na uhitaji wa wanafunzi kupata nafasi vyuoni. Mfumo ulitoa nafasi kwa mwanafunzi kuchagua vyuo angalau vitatu anavyopenda na kozi ambazo angesoma. Faida yake ni kwamba analipa gharama za udahili mara moja tu. Na ikitokea kwenye chuo kimoja ameshindwa kupata nafasi kwa ufaulu wake kuwa duni ikilinganishwa na wenzie basi atapelekwa kushindanishwa na wengine kwenye chuo kingine kulingana na nafasi aliyokipa. Kwa ufupi mfumo huu ni bora sana maana unatoa nafasi na uwanja sawa na mpana kwa wanafunzi wengi.
Changamoto
Pamoja na hivyo mfumo huu ulitengeneza mfereji kwa baadhi ya vyuo na watumishi wasio waaminifu kupeana rushwa na kujinufaisha wao binafsi na vyuo vyao huku wakiwaumiza baadhi ya wanafunzi. Hata hivyo mapungufu haya hayatoshi kuufuta huu mfumo maana ni mapungufu ya kibinadamu. Tunafahamu uwezo wa vyuo vyetu bora (kwa rank UDSM, SUA, MUHAS, MZUMBE etc), na uwezo wa madarasa yetu. Kuna kozi ambazo hukimbiliwa na wanafunzi wengi wa sayansi na kwa upande wa masuala ya jamii vilevile! Kwa mantiki hiyo hakuna uwezekano chuo kimoja kuchukua wanafunzi wote watakaoomba kozi hizo, hili linaongeza nafasi ya wanafunzi wengi kukosa udahili. Kama mwanafunzi huyu aliomba chuo kimoja tu kwa sababu ya uwezo mdogo wa kiuchumi anakuwa na hatari ya kupoteza mwaka mmoja mtaani.
C: Nini kifanyike:
Mifumo hii miwili inahitaji harmonization. kwa sasa CAS ni bora zaidi ingawa kuna vyuo waliitumia vibaya! Ni kweli kila mwanafunzi anahitaji kuchagua chuo anachotaka na kozi anayotaka, hivyo basi wangeboresha CAS ili itoe fursa za mwanafunzi kuchagua vyuo vitatu na kila chuo kozi tatu ambazo angependa kuzisoma!Hii inatoa fursa kwake kama akikutana na ushindani mkali kwenye chuo kimoja kwenye kozi zote tatu basi anakuwa na nafasi ya chuo cha pili kwenye kozi zote tatu na cha tatu vivyo hivyo! Lakini hii ya kuomba direct chuoni (manual) sio rahisi na ni very costly kwa watoto wa maskini! Wengi hawatamudu application fees na transport costs wakati wa kufanya application. Hivyo basi mwanafunzi atajikuta anaishia kujaza chuo kimoja anachokipenda lakini kwa sababu kuna wenzie wenye ufaulu zaidi yake kwenye chuo hicho atakosa nafasi na kujikuta anapoteza mwaka mtaani! Kumbuka next admission year competition itakuwa stiff kuliko ya mwanzo.
NB: Vilevile kuwe na kanuni ya mwanafunzi kukata rufaa kujiridhisha kama kweli alishindwa kwa haki endapo amekosa chuo (yaani waliochaguliwa wamemzidi ufaulu katika kozi alizoomba katika chuo husika), na ikitokea kwa namna yeyote mwanafunzi hakutendewa haki hatua kali zichukuliwe kwa wahusika. Hili litakomesha kabisa tabia za ubinafsi za kibinaadamu.
Iam confident My beloved President huu ushauri ni bora sana kuufikiria na kuutumiaa ili kutoibua hisia hasi za vijana hapo baadae wakati wa zoezi la udahili, and it’s us tunaokupenda na kukutetea daily humu tukusaidie namna ya kuboresha huu mfumo.
“Rais wangu naomba nisikilize, CAS haitakiwi kufutwa bali kuboreshwa”
Mtendahaki