Ushauri: Rais Samia usifanye makosa ya kuteua watu walioharibu huko nyuma au kuwa na dosari za kiuongozi kwa msingi wa kuwapa "second chance"

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kwako Rais Samia,

Kuna jambo moja binafsi naona unafanya makosa makubwa sana, na hili linahusu teuzi zako za hivi karibuni ambazo zinatia ndani watu fulani ambao huko nyuma walionekana kufanya makosa makubwa katika uongozi wao na hata kuwa na dosari katika uongozi wao. Mfano mmoja ni huyu mtu ambaye baada ya kupewa msaada wa magari ya serikali na nchi moja ya nje, yeye alifanya dili na baadhi ya viongozi wakagawana yale magari. Ilisababisha aondolewe mara moja kwenye nafasi yake. Sasa inakuwaje mtu kama huyo unarudi tena kumteua?

Inawezekana kabisa una moyo wa kuona kila mtu anastahili nafasi nyingine - yaani second chance. Hiyo ni falsafa (philosophy) inayotumika katika uhusiano binafsi, sio kwenye dhamana za uongozi au mambo yanayohusu utawala. Acha wapeane second chance na waume zao, wake zao nk, lakini sio kwenye uongozi wa nchi. Hili suala la kepeana second chance lina mahali pake. Ni makosa kwa hakimu kumwambia mtu aliyeiba akakamatwa kwa ushahidi wa wazi kwamba sintakuadhibu nakupa second chance!

Katika mambo ya uongozi wa nchi, sahau kabisa kuteua watu kwa kuwapa second chance. Cheo ni dhamana, mtu akifanya kosa au kuvuruga aondolewe sio kumpa second chance. Nafasi za uongozi ni chache sana ukilinganisha na Watanzania waliopo wenye uwezo wa kupewa hizo nafasi. Hakuna mtu ambaye anatakiwa kuwa na "birthright" kwenye hizi nafasi. Kama aliteuliwa akaharibu, basi iwe ndio mwisho wake - fuata concept ya kuwa na "criminal" record ambayo huruhusiwi tena kuteuliwa kwenye nafasi ya uongozi.

Unapoteua watu ambao watu tunajua walifanya makosa au wana rekodi ya dosari katika uongozi wao huko nyuma, inatufanya Watanzania tusikuamini wewe, na kukuona wewe na hao watu ni kundi moja, mko katika kubebana. Na tunkuwa na shaka labda una weaknesses ambazo hao watu wanazijua na inakufanya uwa-accommodate kwa namna moja au nyingine. Kwa ujumla, inakushushia integrity yako katika kuonekana kiongozi mwenye kufuata maadili na kuwa serious kabisa. Inakupa mapungufu sana katika uongozi wako.

Jenga reputation ya kuwa Rais serious, ili wale unaowateua wajue kwamba wakifanya kosa wanatupwa nje kabisa there will be no second chance, sio kuwa watahamishwa, kubadilishiwa kituo au kazi, au kuwekwa pembeni hadi watu wasahau makosa waliyofanya. Katika muda mfupi uliokuwa Rais umejijengea heshima na kupendwa, sasa usiharibu namna watu tunavyokuona kwa kuanza kuwa-accommodate watu ambao wana very questionable backgrounds. Utajiharibia.

In fact, nakushauri waambie TISS wakupe taarifa kamili juu ya wateule wako wote, na inapobidi tengua baadhi ya teuzi ulizofanya. Kuna watu umewateua kutokana na mambo waliofanya huko nyuma hawastahili kabisa. Usiwaonee aibu, waondoe kulinda heshima yako.
 
Mtaje mkuu usiogope hakuna wasijulikana now
Sio mtu mmoja Mkuu, kwa hiyo kumtaja mmoja ni kumuonea, maana kutenda haki inabidi nitaje wote walioteuliwa kwa kupewa "second chance". Ndio maana nikamtolea mfano bila kumtaja jina
 
Aepuke pia wanasiasa wanaopenda kuhonga waandishi wa habari na kutumia media kujitangaza wengi ni wabovu wala rushwa. Wakati wa mwendazake hao walikuwa wengi sana.
 
Aepuke pia wanasiasa wanaopenda kuhonga waandishi wa habari na kutumia media kujitangaza wengi ni wabovu wala rushwa. Wakati wa mwendazake hao walikuwa wengi sana.
Kufanya kitu kama hicho tayari ni makosa katika uongozi. Kama anawajua wanaofanya hivyo hawapaswi kubaki katika nafasi zao au kuteuliwa kwa nafasi nyingine
 
Kufanya kitu kama hicho tayari ni makosa katika uongozi. Kama anawajua wanaofanya hivyo hawapaswi kubaki katika nafasi zao au kuteuliwa kwa nafasi nyingine
Wako wengi sasa hivi fuatilia wakati wa kusubiri uteuzi wa Ma DC, ona wanavyohangaika kwenye TV na kukamata vitu visivyo na kichwa wala miguu, matukio kibao ya kipuuzi mpaka kuendesha baiskeli.
 
Mfano halisi ni aliyekuwa balozi Bw Alphayo Kidata

Enzi za JPM aliteuliwa kuwa Kamishna mkuu TRA, kisha akaondolewa na kupelekwa kuwa katibu mkuu Ikulu, akahamishwa kuwa balozi baadae 2018 akatumbuliwa na kuvuliwa hadhi ya ubalozi na kurudishwa Tz

Alipoingia SSH akamteua kuwa kamishna mkuu TRA
 
Mfano halisi ni aliyekuwa balozi Bw Alphayo Kidata.

Enzi za JPM aliteuliwa kuwa Kamishna mkuu TRA, kisha akaondolewa na kupelekwa kuwa katibu mkuu Ikulu, akahamishwa kuwa balozi baadae 2018 akatumbuliwa na kuvuliwa hadhi ya ubalozi na kurudishwa Tz

Alipoingia SSH akamteua kuwa kamishna mkuu TRA
Tuseme ukweli, kwa mfano huu uliotoa. Inakufanya umuoneje SSH? Hicho ndicho ninachojaribu kumuambia.
 
Wako wengi sasa hivi fuatilia wakati wa kusubiri uteuzi wa Ma DC, ona wanavyohangaika kwenye TV na kukamata vitu visivyo na kichwa wala miguu, matukio kibao ya kipuuzi mpaka kuendesha baiskeli.
I wish I kudu bi prezidenti! Upuuzi unaoona kwa wale tunaoita viongozi hata mie unanikera mno! Ndio maana nasema wazi, mama Samia has to earn my respect, haiji automatically by virtue of being president of my country. Nitapaki gari pembeni akiwa anapita, au kusimama akiingia ukumbini, lakini nataka isiwe tu kwa sababu natii sheria bali pia kwa kuwa namheshimu.
 
Back
Top Bottom