#COVID19 Ushauri: Rais Samia Suluhu na timu ya Corona fanyeni haya kuboresha mapambano dhidi ya COVID19

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,468
2,000
Mheshimiwa Rais, naomba nikupongeze kwa nia yako nzuri ya kuleta mbadiliko chanya katika ustawi wa taifa. Ama nikupongeze kwa juhudi kubwa unazofanya katika kuendeleza juhudi na upekee wa aliyekuwa rais wa JMT wa awamu ya 5 Rais John Pombe Magufuli. Muendelezo huu ni pamoja na kuboresha pale panapoonekana kuhitaji maboresho kulingana na mahtaiji halisi katiks wakati husika.

Pamoja na hayo, umekuwa mtu wa kusikiliza watu kama alilvyokuwa RAis Magufuli na umekuwa mwepesi wa kuchukua hatua rekebishi ikiwa ni pmaoja na kuunda timu ya Corona.

Sisemi kwamba timu/tume ya corona haikufanya ana ilifanya utafiti wa kina uliopelekea kuchukua hatua za kuagiza chanjo ili kuwachoma watanzania ambao kiwango cha wengi cha uelewa kinaeleweka. Hii ni kwa kuwa report y autafiti wa tume hiyo haikuwekwa wazi.

Pamoja na hayo, ninataka kukubali kwamba timu/tume ya corona ilifanya utafiti sahihi na kugundua kwamba inayoitwa chanjo ya corona siyo chanjo ya corona. Sifahamu ni nini kilipelekea timu hiyo kutoa ushauri wa kuwaacha Watanzania waingie kwenye hili janga la chanjo, badala ya kuboresha juhudi zilizotufanya tuwe juu sana katika upambanaji na corona katika vipindi vilivyopita ikilinganishwa na jirani zetu.

Kuna form imetembea mitandaoni ikiwa inasemekana ni ya wizara ya afya, ikiwataka watakao chanjwa wasaini na imeandikwa kiingereza ambacho kila mtu anajua Watanzania hawakijui. Hii ina maanisha ninikatika ukweli na uwazi? Kwamba mtu asaini ili serikali isiwajibike kwa madhara ya chanjo hizo ambayo yamejitokeza kwa waliotanguliwa kuchanjwa hizo chale?


Mheshimiwa Rais, sote tunafahamu kwamba kuna masuala ya demokrasia na mengine yanatakiwa kuchukuliwa kwa u imra. Mfano masuala ya usafi na afya, ama masuala ya ulinzi na usalama wa nchi, hayahitaji kupigiwa kura. Sesrikali iliyopo madarakani inatarajiwa iwe na macha ya kuona, masikio ya kusikia ndani na nje ya mipaka na nia ya dhati ya kuwalinda wananchi na haki zao zote zikiwemo za kuishi katika mazingira huru na salama.

Form hii haijakanushwa popote na hivyo kuifanya ionekane kwamba ni kweli ni form halali ya serikali.

Ninafahamu kwamba iko nguvu kubwa na agenda kubwa chini ya corono na chanjo zake. Na pengien diyo sababu hakuna nguvu inayopelekwa kwenye tiba, badala yake nguvu kubw ainapelekwa kwenye chanjo ambayo haijafanyiwa utafiti kama kawaida ya chanjo zingine. Dunia ya walimwengu imwamua kuwafanya binadamu kama panya buku wa majaribio.

Mheshimiwa, itakumbukwa katika Corona zilizopita, wwe ukiwa Makamu wa Raisi, tulifanya vizuri katika :-
1) Kuitisha maombi ya taifa zima ambayo ninaamini hata katika awamu hii, ukitamka tu watu tuwe na mda wa kumwomba Mungu, watu wataomba na Mungu alilyetusaidia siku zile atatusaidia tena katika wimbi hili la tatu na hata la nne and mengine yajayo. Mungu ndiye kila kitu.

2) Juhudi za kufuata maelekezo sahihi ya afya ikiwemo kuchukua tahadhari zote kama maji tiririka, kutokpeana mikono, kuvaa barakoa salama, kupunguza misongamano. Leo hii ukienda kwenye sehemu za lazima kama usafiri, watu wanashonana na regulatory authorities hawa effect measures za usalama wa wasafiri. Wanaambiwa wajlinde, wanajilindaje ikiwa vyombo vya usafiri vinawajaza bila hata tahadhari za kuhakikisha kila anayeingia anawa mikono na awe na barakoa kwa mfano? Abiria wakianza kusimamiana wenyewe, kwa kuwa ufahamu wao unatofautiana, wataishia kupigana na kuumizana zaidi. Mfano halisi tu ni ile sheria ya kuvuta sigara vile wavutajiwa sigara wanavyokuwa wakali wakiambiwa wasivute sigara kwenye halaiki.

3) Matumizi ya dawa zetu na ubunifu wa ndani. Kuna dawa zimetanganzwa kutibu na kuzuia corona. Ninaamini TCRA, wamekubaliana kwa kuwa hazikuzuiliwa kutangazwa. Ninadhani tunatakiwa kujikita katika ubunifu wetu na matumizi ya raslimali zetu za ndani katika kutafuta ufumbuzi yakinifu wa matatizo na changamoto zetu. Tusifuate upepoe ambao hawa wanaoufuata hawajui wapi unaelekea hasa kwenye suala hili ambalo ni vita ya dunia.

4. Ninapoandika taarifa hii, ninaomba nikushirikishe hii taarifa hapa kama timu/tume ya corona iliiona na kuidharau ama haikuonekana. Silaha za vita huwa ni siri ya kambi. Kambi ya corona inaju anini wanafanya.


Mhehsimiwa Raisi, ninakuomba sana, kwa Neema ya Mungu iliyojuu yako na juu ya taif letu, bado tunayo nafasi y akufanya vizuri zaidi katika hii vita kwa:-
1) Kusimamishwa utolewaji wa chanjo ngeni badala yake tutumie chanjo zetu za ndani, tiba zetu huku tukiendelea kuziboresha.
2) Regulatory and supervisory bodies, zisimamie kwa kumaanisha compliance na maagizo ya wataalam wetu wa Afya juu ya tahadhari za kujikinga na maambukizi, hasa katika public services kama mashuleni, usafirini, sokonini nk.

3) Wizara ya afya ifanye kampeni kabambe, kama ililvyokuwa miaka ya 70-80 kuhakikisha kila kaya inachemsha maji ya kunywa. Kampeni hii iwe ni matumizi ya vyakula vinavyoinua kinga ya mwili, kupambana na virus and bacteria, magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.

4) Kupitia Wizara ya afya, kitengo cha tiba za asili, serikali iwezeshe uboreshaji, utengenezaji, usambazaji na matumizi za asili. Kama ni kinga zifikie kila familia kwa gharama nafuu na kama ni tiba zipatikane kwa urahisi ili maisha yendelee.

Kwa kufanya haya, Tanzania na vizazi vyote vitakukumbuka kwamba uliotuokoa kutoka kitanzi cha watu wenaodhani wao peke yao wanayohaki ya kuishi duniani kuliko binadmau wengine.

Aksante sana kwa kusikiliza.
 

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,468
2,000
Mkuu usipotoshe watu. Chanjo zote zinazotumika tangu miaka ya sitini; TB, Pepo punda,Polio, Surua, Kichaa cha mbwa, Homa ya manjano, Dondakoo n.k zilifanyiwa utafiti kwa wanyama kwa kipindi kinachozidi miaka mitano na baadaye kuanza majaribio kwa miaka mingine mitano kwa binadamu waliojitolea .... Baada ya kuthibitika kuwa ni salama ndipo zilipoanza kutumika .... Chanjo ya COVID-19 haijapitia mchakato huo muhimu.

Inasikitisha kuona na kusikia kuwa Balozi Riberata Mula Mula nae ameikumbatia hoja hii dhaifu eti hata yeye akiwa mdogo alichanjwa. Mwili una uwezo wa asili wa kujilinda na magonjwa,.... kama tunataka kuusaidia mwili kujikinga kwa haraka zetu, sharti la kwanza ni kuwa na chanjo iliyofanyiwa utafiti na kuthibitika kuwa ni salama... Tusicheze na miili ya watu.
Nidyo ujua rais ana watu wasiojiweza.
 

Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,202
2,000
Sintofahamu ya chanjo ni kubwa sana na mijadala mingi imeonyesha wasiwasi wa watu kuona ni kwanini kuna uharaka wa kutaka watu wachanjwe, na kingine kikubwa ni kwanini kuna chanjo aina tofauti badala ya kuwa na moja ambayo inakubalika na shirika la afya ulimwenguni kwa matumizi ya duniani kote? kwa sasa kila mtu ana chanjo yake Pfizer,Moderna,Johnson Johnson e.t.c na kwingineko yametokea madhara mengi kutokana na chanjo hizo , kingine ni kwamba kuna ambazo ni kwaajili ya afrika pekee hapo ndio watu wanajiuliza kwanini? kimsingi uoga huo una hoja ndani yake maana hata walipata hizo chanjo bado wanashambuliwa sana na Variant , mfano Uingereza last week asilimia 60 ya waliolazwa mahospitalini ni wale ambao wamechanjwa tena full vaccinated yaani waliopokea chanjo zote tatu. Wasiwasi mkuu ni kwa jinsi chanjo hizo hazijapewa ithibati na WHO ni suala la dharura tu, kila mwenye akil achanganye na zake hakuna bingwa wala mjinga kwenye COVID
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom