USHAURI: Rais Samia Suluhu amteue Joseph Magufuli kuwa Mbunge na Waziri

Dahh kuna watu wana mawazo ya kipuudhi sana
Na tabia hii ya kufanya uongozi wa nchi hii kuwa wa kiimla na ikome ni upuudhi tu yaani kabisa unashauri mtu ateuliwe kwenye nafasi ya umma kama kumfuta machozi,
Mawazo ya kipuudhi sana
Sio upuudhi mkuu bali upuuzi
 
Nani amekwambia mama yake hana uwezo ya kujitunza? Unajua amelipwa kiasi gani kama mafao? Unajua kwamba anaendelea kulipwa mpaka kufa kwake? Huyo mama hana shida mapak dakika hii!!
Kwa Pesa walizonazo pamoja na Mali nyingi wakiona tunawajadili hivi wakati wengine hata Nauli tu za kuendea Sokoni Ilala Boma au Buguruni Kesho Alfajiri hatuna wanatuona Mipumbavu mno tu huku wakitucheka kwa Dharau.
 
Nikiri kuwa binafsi nilikuwa simfahamu Joseph Magufuli kwa undani hadi nilipomuona juzi akiongea kwenye kongamano la kidini kule Chamwino, Dodoma.

Kijana huyu jasiri alipokaribishwa kutoa shukrani za familia mbele ya Rais na viongozi wa dini, alionesha ukomavu mkubwa sana. Kwa wale mliofuatilia kongamano hili mtakubaliana nami kuwa hata mama Samia alionyesha kumkubali.




Bila kuwachosha na maneno mengi, naomba niingie kwenye hoja moja kwa moja. Umekuwa ni utaratibu wa kawaida kiongozi anapofariki, hasa mbunge, mtoto wake huchukua usukani wa jimbo alilokuwa akiliongoza marehemu baba au mama yake. Mifano ipo mingi sina haja ya kuitaja.

Sasa kwa kuwa Rais Magufuli kipenzi cha wana wa Tanzania, Afrika na dunia nzima ametutoka ghafla pasipo kutarajia, namuomba sana Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu amteue ndugu Joseph John Pombe Magufuli kuwa mbunge na hata kama itampendeza amteue kuwa waziri katika wizara yoyote atakayoona inafaa.

Ninazo sababu zilizonipelekea kutuma ombi langu hili kwa mama Samia na nitazieleza kwa ufupi sana kama ifuatavyo:

Marehemu Rais John Pombe Joseph Magufuli alikuwa kipenzi cha watanzania wote na dunia nzima kwa ujumla. Kitendo cha kumteua Joseph Magufuli kuwa mbunge kitawafuta machozi watanzania, hasa pale watakapokuwa wakisikia jina la Magufuli likitajwa kupitia kwa mtoto wake.

Tukumbuke kuwa Magufuli alikuwa anapendwa na watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kidini, kisiasa, kikabila, kikanda na kijamii.

Hivyo basi, uwepo wa mtoto wa Magufuli ndani ya serikali utawafariji watanzania wote na watu wenye mapenzi na maendeleo ya taifa letu.

Kama ilivyo kawaida kwa watoto wa wabunge waliofariki kufutwa machozi kwa kupewa ubunge kwenye majimbo waliyokuwa wakiyaongoza wazazi wao, kitendo cha Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mbunge na waziri kitasaidia kuifuta machozi familia kwa kuwa nina imani mshahara atakaokuwa anaupata kutokana na uwaziri utasaidia sana kuboresha hali za kiuchumi za wanafamilia.

Ingekuwa baba yake alikuwa mbunge ingekuwa rahisi sana kuteuliwa kugombea ubunge na kukalia kiti cha jimbo la baba yake.

Lakini kwa kuwa baba alikuwa Rais, na kwa mujibu sheria anayepaswa kukalia kiti hicho ni makamu wa Rais, hatuwezi kusema labda mama Samia ampishe akalie usukani kwa kuwa tukifanya hivyo tutakuwa tunavunja katiba ya nchi. Hivyo, njia pekee ya Joseph Magufuli kupenya kwenye siasa ni kupitia ubunge na uwaziri wa kuteuliwa.

Joseph Magufuli ni kijana msomi na mwenye uwezo wa kuongoza wizara yoyote ijapokuwa hajawahi kuingia kwenye siasa. Hivyo, nina imani kuwa anaweza kuwa waziri mzuri kama alivyokuwa baba yake.

Na ningependekeza mama Samia amteue kuwa waziri wa ujenzi ili kumuenzi marehemu baba yake aliyewahi kuongoza wizara hiyo kwa ufanisi mkubwa.

Ikiwa watoto wa wabunge waliowahi kuziba nafasi za baba/mama zao huko nyuma hawakushindwa, iweje Joseph yeye ashindwe?

Kwa sababu hizi nilizozitaja hapo juu, namuomba sana mama yetu na Rais wetu mpendwa H.E Samia Suluhu Hassan amteue Joseph Magufuli kuwa mbunge na kama itampendeza amteue kuwa waziri wa ujenzi.

Nawasilisha.
Bahati mbaya Tanzania hatuna mfumo wa Kifalme!
 
Kuna Muosha Magari Mmoja hapo ( kapewa Jina la Mchezaji Maarufu wa Yanga SC ) anasema Kijana japo ni Bonge hivi ila anapenda sana Kubinjuka halafu ana allergy na Kofia za Kibailojia za Wanaume tunazohimizwa 24/7 na WHO kuwa tuwe tunazivaa katika Vichwa vyetu vilivyotulia Mafichoni.
Umetembea na key mpaka raha
 
Huyo kijana amtafutie permanent job kwenye taasisi moja safi inatosha (like BOT, TRA & TCRA)

Apate uwezo/uhakika wa kumtunza Mama yake na Bibi yake

Una hakika kuwa JIWE hana kibubu kinachofurika nyumbani kwake? Kumbuka amekuwa waziri wa ujenzi kwa miongo mingi na Rais kwa zaidi ya miaka mitano!! Nina hakika familia yake sio masikini kwani marais wa Afrika wana sifa ya kuyaibia mataifa yao na kuficha fedha nje!!! Don't you think it was strategic to appoint DOTTO ,his blood relative as paymaster general?
 
Wapo wabunge na viongozi mizigo wengi tu, nafikiri Joseph anafaa kuwa mbunge wa kuteuliwa kwa sasa! Uwaziri asikimbiziwe haraka haraka! Kama liz1 ni mbunge basi kila mtu anafaa kuwa mbunge😜!
Kwahiyo ateuliwe tu kwakuwa Kafiwa na Baba yake? Kuna baadhi ya Watanzania Kiukweli Akilini zenu zipo Makalioni badala ya Kichwani.
 
Bangi + Gongo + Njaa = Mleta Uzi huu.
Naona kitu hicho kimemzingua
Screenshot_20210420-004615_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom