Ushauri: Rais Magufuli mfutie kesi kijana huyu

Na

Nahisi upepo wako uko kwenye pesa tu lakini hauko kwenye uandishi!
Si kweli.
Msingi wa uandishi ulitaka baada ya kuniuliza kama naelewa maana ya mtandao, ulitakiwa unieleze maana yake, ili iwe wazi kwamba tunajadili kitu kimoja baina yetu.
unaelewa maana ya mtu kukuuliza swali? yani nikuulize swali alafu mimi ndiye nijibu? uko timamu kweli kichwani?
Sasa haya majadiliano umeyafanya yawe marefu bila ya ulazima.
Ni wewe ndiye umeyafanya na sio mimi.
Nini maana ya mtandao?
Hili ndilo swali langu la msingi, na nnahitaji majibu kama huna usini-quote tena.
 
Hata Mungu anajua!
mkuu, ni kweli kabisa. ina maana kila rais anakuja na lake. huyu akiamua kujenga sawa, akija mwingine akaamua kubomoa nayo ni sawa pia. nchi haina utaratibu na awamu za serikali si za wananchi. leo serikali ya john jana ilikuwa serikali ya jakaya.
 
Huwezi kumuita Rais bwege, mwalimu wako tu darasani huwezi kumuita hivyo, sembuse Rais.
kwanini huwezi kumuita hivyo kama anayo yafanya yanastahili hiyo sifa kunakosa gani??utandawazi tunaulazimisha wakati uko speed zaidi yetu alafu tunataka tuukimbize
 
Raisi Magufuli,wewe ukiwa ni mwanasiasa unapaswa kuwa makini na mambo "madogomadogo" ambayo ukiyapuuza yatakujenga zaidi kuliko ukiyapa uzito.

Kwa ushauri wangu,jambo unalopaswa kutolipa uzito kwa sasa na hii kesi ya kijana Isaack wa mkoani Arusha anaetuhumiwa kukutukana.Kesi ya aina hii kwa mwanasiasa katika dunia ya leo si jambo jema sana hivyo ni bora tu kuachananayo.

Mh,ninaakika kesho ukiagiza Polisi waifute kesi hiyo,utakuwa umejizolea point nyingi sana kisiasa kuliko ukiacha kesi hiyo iendelee.Sifa ya mwanasiasa ni uvumilivu na hata mzee Sitta aliwahi sema Bungeni kuwa mwanasiasa unapaswa kuwa na roho ngumu hivyo mh.jambo hili litazame upya.

Mh.Raisi labda nimalize kwa kukuulize swali hili:

Unakumbuka ni nani aliwaita wapinzani watoto ndani ya Bunge?

NB:Mh.Raisi, ukiomba/ukielekeza wahusika wafute hii kesi hawa hawa wanaokejeli hili wazo langu ndio watakuwa wa kwanza kukusifia.
Hasa Ukizingatia, Rais wakati wa Kampeni sio yeye binafsi alikaa katikati ya Vijana Waliomtukana Lowassa Kila tusi Duniani na Kuzimu, Na mengine juu ya Afya yake ambayo hakuna Utamaduni hata wa Kishenzi namna gani utavumilia haya akakaa kimya. Wengine hata ni Mawazi katika serikali yake. Namtoa Nape Kama Mfano.
Ukilinganisha Huyu Kijana (Inangawa simpongezi) na Matusi ya CCM dhidi ya Lowassa huyu Kijana Ni Malaika. Je wale walifanywa Nini?
 
sheria lazima ichukue mkondo wake kamanda, zama zile za matusi hazipo tena. lazima wachache waumie kwa matendo yao ili wengine wajifunze. tuache kuishi kwa mazoea.
Sama hizo ziliisha Lini, Baada ya CCM Kuzunguka na Kumtukana Lowassa Kila tusi Duniani na Kuzimu, huku Magufuli akiwa amekaa na Kuchekelea? Acha unafiki!!!!!!!!!!!! zama za Matusi zimeisha usinitake Nitapike!
 
Yeye katukana Watanzania wenzake kwa kuwaita mashetani, na yeye mkwapuzi wa nyumba na kulitia hasara Taifa ya shilingi 38 trilioini na mnunuzi wa boti bovu kwa shilingi bilioni 8 ambalo lilifanya kazi wiki tatu tu pia mhujumu uchumi tumuite jina lipi baya?

Tatizo lenu bado mnafikiri tuko kwenye siasa na utawala wa miaka ya 70 na 60 kurudi nyuma.
 
Yeye katukana Watanzania wenzake kwa kuwaita mashetani, na yeye mkwapuzi wa nyumba na kulitia hasara Taifa ya shilingi 38 trilioini na mnunuzi wa boti bovu kwa shilingi bilioni 8 ambalo lilifanya kazi wiki tatu tu pia mhujumu uchumi tumuite jina lipi baya?
Sijui tumite member wa uko wa....... kila mtu.....?
 
Back
Top Bottom