USHAURI: Rais avunje Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Chimbuko la migogoro ya ardhi iwe ni wafugaji kwa wakulima, iwe ni wananchi na wawekezaji kama maneo yenye madini au iwe ni maeneo ya mijini kama nilivyosikia kinondoni nyumba 400 zinabomolewa au iwe ni ngorongoro

Chimbuko la migogoro hii ni wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi.

Kwa utabiri wangu tukiendelea na wizara hii, miaka 100 ijayo tanzania haitakiwa na miji wala vijiji bali makazi yatakuwa yametapakaa nchi nzima.

Miji itaungana, vijiji vitaungana na migogoro itakuwa ni mingi sana.

kwa nini ninaituhumu wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi?

Hii Wizara jukumu lake la msingi ni kuweka utaratibu wa matumizi bora ya ardhi yetu kwa kutazama maendeleo.
wataalamu wanasema hatua ya kwanza ya maendeleo ni mpango wa ardhi na maendeleo ya makazi.

Katika nchi yetu, wizara hii wamekaa tu hawapangi chochote, hakuna utaratibu wa chochote uiowekwa na wizara hii.

Ukitazama miji mingi makazi ya zamani yalikuwa yakijengwa kwa mpangilio, wakiacha nafasi kwa ajili ya huduma mbalimbali. Lakini sijui miaka gani wizara hii iliangukia kwa watoto wa mjini wakaacha kufanya majukumu yao na kuingia kwenye kufanya biashara za ardhi. waliacha kupanga watu wakaeje mijini na yule aliyehitaji hati za ardhi au kukaa sehemu iliyopangwa vizuri waligeuza ama biashara ya wizara au ya watumishi binafsi.

Jambo hili limevuruga miji yote, ukitazama miji inavyokua kwa sasa ni upuuzi mtupu

Athari za ukuaji holela wa miji hii ni kufanya kazi ya serikali ya utoaji huduma kuwa ngumu kutokana na watu kutapaa maeneo makubwa na hivyo serikali kuwapatia huduma inalazimika kutandaza miundombinu ya huduma maeneo makubwa sana na kuhitaji fedha nyingi.

Usalama kwa watu umekuwa shida maana watu wnavyokaa mbalimbali ndivyo vibaka wanavyotumia mianya hiyo kufanya uporaji. katika maeneo haya hata ulinzi shirikishi ni ngumu kwa kuwa maeneo makubwa yana wakazi kidogo.

Yaani wizara imejaa watu wasiojua majukumuyao ambao hawaoni adha anazozipata mtu wa chini. Mtu anaweza kukamata ardhi yenye ukubwa wa ekari mbili tatu katikati ya mji, awe na hati au asiwe na yo hawana habari.

Badala ya kupanga miji watu waishije, badala ya kutunga kanuni za kuongoza watu waishije, makazi yawe na sifa gani, kila makazi yawe maximum umbali gani kutoka huduma za kijaamii na kuwapanga watu waishi kulingana na kanuni zinavyosema

Hawa wanachokifanya unaweza kujiuliza hivi hawa wamesoma hata angalau kidogo? wanahangaika kusuluhisha migogoro na siyo kutatua migogoro.

Kutatua migogoro ni kujua chimbuko na kulitolea suluhu lakini wao wanahaika kuhalilisha kila mtu alivyokaa ilimradi watu walipe kodi. Swala la kukusanya kodi liachiwe wizara ya fedha na wao jukumu lao ni kuweka misingi ambayo inarahisisha kazi za wizara nyingine zote.

Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makzi, mtu anabomoa nyumba 400 mjini kama nilivyosikia kinondoni Dar es salaam na serikali nzima imekaa kimya? bila kumuwajibisha waziri husika? Mwananchi ni muhanga ambaye wizara hii ilitakiwa kuweka taratibu zinazodhibiti wahuni mjini.

Tumesikia watu ngorongoro wanahamishwa kwa gharama kubwa. hivi hii wizara imeweka utaratibu gani wa makzi vijijini? imeweka utaratibu gani wa mashamba ya kilimo? imeweka utaratibu gani wa maeneo ya malisho ya mifugo. wameacha watu bila utaratibu, ukifika popote unaweza kujenga nyumba na kuishi . ila akiibuka mtu mmoja siku moja akasema uko ndani ya hifadhi utachomewa nyumba, utafyekewa mazao na ujingaujinga mwingi tu.

Tumeiacha wizara haifanyi majukumu yake, wamejiweka kwenye shughuli zenye ulaji tu na sote tunaridhika na kuona wachapa kazi. Ama kweli kama hatuoni matatizo makubwa yaliyoko katika wizara hii basi elimu yetu ina matatizo makubwa sana.

Kupanga miji ni jambo linalowezekana kabisa bila kukopa hela kutoka benki ya dunia za kuwahamisha watu kama matapeli wanavyoshauri.

0. Wizara ya ardhi iundwe upya ikipewa muundo na msukumo mpya.
1. Ni lazima wizara ya ardhi itoe miongozo inayoelekeza upangaji wa makazi
2. Halmashauri kuajiri watumishi wa kutosha (surveyors na CAD technicians)
3. Halmashauri kushirikiana na serikali za mitaa kuwaelimisha na pengine kuwa na kamati za upangaji makazi kwa ngazi ya kata au mitaa
4. Kuanzisha kodi ya upangaji miji. (hapa nieleweke kuwa hii siyo kodi ya kutoa fidia au kuwatengenezea ulaji wapimaji na walipa fidia, serikali inatakiwa kupanga bure na wananchi wakipimiwa maeneo yao wanaweza kuuza wenyewe na pengine serikali ipate asilimia ndogo tu ila kodi itumike kwenye vitu ambavyo gharama haiepukiki)
5. Wenyeviti wa mitaa na kamati zao zinaweza kufundishwa jinsi ya kuweka mpangilio sahihi hata kama wataalamu wa serikali hawajafika kuingiza taarifa kwenye mifumo ya serikali.
6. Ni lazima ukuaji wa miji uwekewe utaratibu ikiwa ni pamoja na kudhibiti utunzaji wa ardhi, bei za ardhi zipangwe na miji lazima ikue kwa pamoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom