Ushauri: Paul Makonda magari yako yaandikwe "Polisi" sio " police"

yahoo

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
3,527
1,405
Napenda sana utendaji Wa mkuu Wa mkoa Wa Dar es salaam mh. Paul Makonda. Mbali na hapo, nimeona akikagua ukarabati Wa magari yaliyokuwa mabovu yakikarabatiwa mkoani Moshi, nilifurahishwa na jambo hilo.

Lakini kisichonifuraisha ni kuona magari hayo yakiwa yameandikwa neno "Police" lugha ambayo ni kingereza na ni kinyume na lugha yetu ya Kiswahili. Nakumbuka zamani magari yote ya polisi yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kiswahili yani "Polisi" Hata kama yamenununuliwa uingereza yalibadilishiwa maandishi kabla ya kuingizwa barabarani.

Asante tuienzi lugha yetu
 
Siyo kazi za mkuu wa mkoa kukarabati magari ya polisi! Sheria ya manunuzi ipo wanapaswa waifuate na kumpatia mzabuni hiyo kazi!
Yale magari yalikuwa grounded yeye kaamua kuyafufua. Yalikuwa yanasubiri yaingizwe kwenye mada.
 
Napenda sana utendaji Wa mkuu Wa mkoa Wa Dar es salaam mh.Paul makonda. Mbali na hapo, nimeona akikagua ukarabati Wa magari yaliokuwa mabovu yakikarabatiwa mkoani Moshi, nilifurahishwa na jambo hilo,lakini kisichonifuraisha ni kuona magari hayo yakiwa yameandikwa neno "Police" lugha ambayo ni kingereza na ni kinyume na lugha yetu ya kiswahili ..nakumbuka zamani magari yote ya polisi yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kiswahili yani "Polisi" Hata kama yamenununuliwa uingereza yalibadilishiwa maandishi kabla yakuingizwa balabalani...Asante tuienzi lugha yetu
Minor issue ila ushauri mzuri
 
Siyo kazi za mkuu wa mkoa kukarabati magari ya polisi! Sheria ya manunuzi ipo wanapaswa waifuate na kumpatia mzabuni hiyo kazi!
sheria ya manunuzi inahusiana vipi na ukarabati?? aisee, hivi unaifahamu hyo sharia ya manunuzi au umetamka tu?? ukarabati na sheria ya manunuzi haviingiliani
 
sheria ya manunuzi inahusiana vipi na ukarabati?? aisee, hivi unaifahamu hyo sharia ya manunuzi au umetamka tu?? ukarabati na sheria ya manunuzi haviingiliani
Huijui sheria ya manunuzi. Nakushauri kaisome upya!
 
sheria ya manunuzi inahusiana vipi na ukarabati?? aisee, hivi unaifahamu hyo sharia ya manunuzi au umetamka tu?? ukarabati na sheria ya manunuzi haviingiliani
Kwa taarifa yako. Makonda ameomba msaada kutoka kampuni ya ukarabati magari na kampini hiyo inakarabati bure...na safari ya kuyafikisha huko Kilimanjaro yalibebwa na magari ya jwtz
 
Kwa akili yako lugha ni minor issue? Hapo ni sawa na kusema magari ya polisi ya uingereza yaandikwe "polisi" kwa lugha ya kijapani
Minor issue Tanzania tunatumia kiingereza na kiswahili ni lugha rasmi tunazozitumia.

Ila waaingereza hawawezi kuandika kijapani kwasababu sio lugha wanaoitumia.
 
sheria ya manunuzi inahusiana vipi na ukarabati?? aisee, hivi unaifahamu hyo sharia ya manunuzi au umetamka tu?? ukarabati na sheria ya manunuzi haviingiliani
nani kakwambia ukarabati na sheria ya manunuzi haviingiliani kama hujua kaa kimya wewe
 
Siyo kazi za mkuu wa mkoa kukarabati magari ya polisi! Sheria ya manunuzi ipo wanapaswa waifuate na kumpatia mzabuni hiyo kazi!
Hivi ulichokiandika ulikipitia kukisoma? OK anyway hujui chanzo cha habari.

Note: makonda hajatoa hata sent 5 hapo
 
Ni vizuri mtu akifanya kitu kizuri kwa faida ya nchi apongezwe , mambo mengi anayofanya mkuu wa mkoa anatafuta wafadhili na sio hela za serikali sasa awaambie wafadhili watangaze zabuni na pia magari mengine yalishawekwa pembeni miaka miwili gari jumla 56 zilikuwa mbovu leo zinarudi barabarani tumpongeze tuache siasa ktk kila jambo
 
Back
Top Bottom