Ushauri: Nipo Wilaya ya Ilemela Mwanza, kwa mtaji mdogo naweza fanya biashara gani?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Wakuu Salamu kwenu

Nipo Wilaya ya Ilemela kata ya Shibula katika Jiji la Mwanza

Sasa Nina laki 5 (500,000/-) je hii naweza kufungua biashara gani ambayo itanipa faida fresh na haitakuwa na usumbufu usumbufu

Nahitaji ushauri wenu na mawazo yenu hasa kutoka kwa wazoefu wa biashara.

Asante
 
Hapo nakushauri ukachukue miguu ya kuku na shingo, utatoka muda si mrefu
 
Teremka hapo Igombe chukua dagaa, anika kwenye eneo safi wasiwe na mchanga kisha pack kwenye mifuko mafungu ya 1,000 Tsh halafu tembeza kwa baiskeli mtaa kwa mtaa kuanzia Shibula,Nyamwilolelwa,Kahama,hadi buswelu.
 
Back
Top Bottom