Ushauri: Nipo diploma ila napanga kurisit

Aug 13, 2017
17
11
Mimi ni muhitimu kidato cha sita mwaka 2017 kwa bahati mbaya nimepata Div.3.14 yaani DEE mchepuo wa CBG kwa bahati mbaya sina sifa za kujiunga katika ngazi ya degree kwenye chochote hapa nchini.

Lengo la uzi huu baada ya kukaa kwa muda mrefu kufikiria nikapata mawazo ya kurudia mtihani yaani kuresiti kama private candidate lakini kutokana na matokeo ya PC wa mwaka wangu matumaini yanapotea kabisa nikaona bora ni unge moja kwa moja chuo kwa ngazi ya diploma miaka mitatu na nishaanza chuo tayari kwenye chuo kimoja huko Boko lakini wakati nimeanza chuo nikapata wazo la kuresiti wakati nipo naendelea na diploma pale nitakapotusua naachana na diploma napiga degree!

Kwenu wakuu mnaonaje wazo langu ushauri wenu, je inawezekana?
 
kweli,Mshika mbili moja humponyoka..! Mkuu chagua kimoja,kama nia yako awali ilikua kurudia mitihani,basi hapakua na sababu ya kuanza diploma, kumbuka kurudia mitihani tena "CBG' kunahitaji utulivu na maandalizi mazuri ili uweze kufaulu vizuri.
 
Sasa ww acha kujichanganya deploma ya pharmacy iko njema ukimaliza unaweza tafta kaz au ukaapply bachela kwa kutumia deploma acha kujichanganya ndugu yangu stick Na kitu kimoja ndoo utaona faida yake
 
Mimi ni muhitimu kidato cha sita mwaka 2017 kwa bahati mbaya nimepata Div.3.14 yaani DEE mchepuo wa CBG kwa bahati mbaya sina sifa za kujiunga katika ngazi ya degree kwenye chochote hapa nchini.

Lengo la uzi huu baada ya kukaa kwa muda mrefu kufikiria nikapata mawazo ya kurudia mtihani yaani kuresiti kama private candidate lakini kutokana na matokeo ya PC wa mwaka wangu matumaini yanapotea kabisa nikaona bora ni unge moja kwa moja chuo kwa ngazi ya diploma miaka mitatu na nishaanza chuo tayari kwenye chuo kimoja huko Boko lakini wakati nimeanza chuo nikapata wazo la kuresiti wakati nipo naendelea na diploma pale nitakapotusua naachana na diploma napiga degree!

Kwenu wakuu mnaonaje wazo langu ushauri wenu, je inawezekana?

OK
Kwanza nikupe hongera kwa kupata nafasi japo ya kuendelea na diploma maana wapo wenye matokeo kama yako hawajui pa kwenda

Mpaka hapo ndoto yako nadhani itakuwa pale pale maana ukimaliza diploma unaweza ajiriwa kwa ngazi hiyo au ukaamua kuingia degree
Ushauri wangu ni kwamba kaza buti utoke na GPA nzuri ya kukuwezesha usonge mbele ngazi ya degree ,ukileta GPA ya kichovu utakwama pia uko mbele
Achana na mawazo ya kuresit madamu umepata nafasi ya kuendelea na diploma utapomaliza hiyo utafika uko unakokutaka kwa sasa acha kupoteza muda piga shule GPA inatakiwa mkuu

Mara nyingi anaye resiti ni yule aliyekosa pa kwenda anarudia pepa ili mambo yawe sawa asonge mbele
Sasa ushapata pakuanzia bado unawa kurudi kwenye mitihani ya kidato cha sita??? Haloooo vipi mkuu,afu unaweza shangaa ukirudia ata ulichopata saivi usipate ukachemka zaidi utajikuta unajuta kwamba kwanni sikukazia buti diploma tu
Kwa hiyo mkuu hayo mawazo futa,tulia kamua ulete GPA iliyosimama huende huko kwenye degree unakokutaka

Unajua mfumo wa form 6 umetuharibu sana mpaka watu wana kariri kwamba akitoka form 6 basi ni degree
Ndo maana wakati mwingine nashauri MTU akimaliza ata kidato cha NNE tu inatosha kuanza kutimiza ndoto yake kwa kwenda certificate/diploma ya kitu anachokitaka baadaye degree kama tu ada ya kulipa college itakuwepo hakuna haja ya kwenda advance,nadhani ata Leo utakubaliana na mm
Kwa mfano wewe ulivomaliza form four ungeamua kuingia moja kwa moja kwenye hiyo diploma ya pharmacy ungekuwa umemaliza au unaelekea kumaliza na ungekuwa unazungumzia mengine saivi
Kulko kupoteza muda advance matokeo yakija tofauti unaenda college kwa kutumia Cheti cha o level unakuwa sawa na asiyepita advance na pengine anakukimbiza darasani na form 6 yako
 
Kama una uwezo wa kupambana na maphamacology huku ukiendelea na michakato ya kurisiti fresh..
ila kama ni kichwa panzi utaishia kusup na kushindwa kupata kile unachotaka.

kwa hiyo jaribu kukaa chini na kutafakari kama una uwezo wa kufanya hivyo basi heri ila kama hauna uwezo achana nayo
 
Jamani nimepangwa diploma Mbeya University of Science & Technology... nmechelewa registration sababu ya ada.. vipi ndo nataka niende nimechelewa au,? Nisaidieni
 
Back
Top Bottom