Ushauri: Nini kifanyike ili kupunguza adha ya usafiri pale stendi ya Mwenge kwenda Goba na Bunju

Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,414
4,292
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini unaweza kuona daladala haina abiria hata mmoja, lakini inapita kituoni (hasa vituo vya mwisho) bila kupakia wakati hapo kituoni mpo abiria kibao wa ruti ya gari hiyo, lakini konda hafungui mlango anapita anaenda kupakilia vituo vya mbele?

Kama ulikuwa hujui basi na kusanua, mbali na sababu nyingi, MAKONDA & MADEREVA walishafanya RESEARCH zao na kugundua kuwa; ABIRIA WANAOPANDIA MWANZO/KWENYE VITUO VIKUBWA HUWA HAWASHUKI MPAKA MWISHO WA RUTI/SAFARI.

Kwa tafsiri nyepesi ni kuwa abiria hawa hawana faida sana muda huo wa biashara, Mfano; abiria anaepanda kituo cha CCBRT/MACHO pale Msasani gari ya kwenda S/2000 (mida ya biashara/jioni) mara nyingi huwa hawashuki mpaka S/2000, kwa hiyo wanakua ni kama wamezuia siti.

Siti inabidi iuzwe mara tatu mpaka nne kutoka Macho mpaka S/2000.
Abiria wa namna hii tuwaite MAWE(Hawana faida/wakikaa wamekaa/ hawahamishiki).

TURUDI KWENYE MADA
Tatizo la uhaba wa usafiri/daladala kituo cha mabasi mwenge(bagamoyo road) linazidi kukua siku hadi siku.
Inapofika jioni huwa ni mshike mshike kweli pale mwenge kupata usafiri ruti za goba, tegeta na bunju.
Kwa nature ya eneo la Mwenge(eneo la biashara na ofisi na sio makazi) ni eneo ambalo lilitakiwa kuwa na stand kubwa(daladala ziishie/zianzie pale)kama Makumbusho ili kuweza kuwamudu abiria kwa wakati(nilipata kusikia itajengwa).

Kwa hali ilivyo sasa, abiria wa ruti za goba, tegeta na bunju wanategemea daladala zinazotoka Makumbusho, Gerezani na Ubungo, ambazo huwa zikifika Mwenge tayari zinakua zimejaza sana wale ABIRIA MAWE(Mwenge hakuna Makazi)
ambao huanzia kushuka kituo cha bondeni nakuendelea, sina maana pale Mwenge huwa hawashuki la hasha, lakini unaweza kukuta anashuka abiria mmoja au wawili tu, huku nje kukiwa na rundo la abiria wakigombea nafasi.

NINI KIFANYIKE?
Kila inapofika jioni/mida korofi, wahusika/jeshi la polisi waruhusu baadhi ya daladala(sio zote) ambazo hutoka Goba, Tegeta na Bunju Kwenda Makumbusho na S/2000, ziwe zinaishia Mwenge na kwenda kugeuza pale round about ili kurudi kituo cha Mwenge kupunguza ule mrundikano, nadhani kukiwa na daladala kama kumi na tano zinazopishana pale kila jioni kwenda Goba na Bunju wale abiria wa Mwenge hawatokua yatima tena.

Hizi zitakua zinatoka Bunju na goba zikiitia abiria Mwisho Mwenge, ikifika Mwenge abiria wote wanashuka inaenda mpakani round about inageuza kisha inakuja ikiwa tupu kuanza kuchukua abiria hapo Mwenge wa kwenda Goba au Bunju.

Naimani kama wazo langu likifanyika chini ya uangalizi mzuri litakua na matokeo Mazuri.

FB_IMG_15769479648512537.jpg

FB_IMG_15769482248660029.jpg
 
View attachment 1515371

View attachment 1515372
Latra ndio wenye mamlaka hayo,Ungeenda ofisini kwao ama ukawapigia simu basi ingekuwa ni vizuri sana
 
Back
Top Bottom