Ushauri: Nina milioni sita nahitaji kuwekeza katika ufugaji

relis

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,188
4,762
Salaam wakuu!

Baada ya kuhangaika sana nimefanikiwa kupata milioni 6 ya mkopo bank, sasa nilikuwa nahitaji kuwekeza katika ufugaji, eneo la kufugia ninalo tayari lenye ukubwa wa heka 30 na ni eneo la mashambani kidogo.

Kwa eneo nilipo kwa ujenzi naweza tumia tofali za kuchoma kwa ujenzi kwa kuwa zinapatikana na pesa niliyonayo nahitaji kuitumia kwa ajili ya ujenzi wa kibanda cha mlinzi, mabanda ya mifugo na ununuzi wa mifugo.

Msaada na nini nifuge kwa kurudisha pesa haraka.
 
Mpaka hapo umeshafeli, kabla ya kuchukua pesa inabidi mipango yote na taarifa zote za unachoenda kufanya ziwe tayari, na hapo umeshakusanya taarifa zote muhimu.

Sasa ndugu hizo pesa zinawezapotea pasipo cha maana kwasababu utafanya vitu ambavyo haviko katika mpango na mpangilio.
 
Ulipaswa ukachukue hela ukiwa na framework nzima ya mpango huo, kama mpk sasa hujajua hata unataka kufuga nini na kitakulipaje basi mambo yashaharibika.
 
Mpaka hapo umeshafeli, kabla ya kuchukua pesa inabidi mipango yote na taarifa zote za unachoenda kufanya ziwe tayari, na hapo umeshakusanya taarifa zote muhimu.

Sasa ndugu hizo pesa zinawezapotea pasipo cha maana kwasababu utafanya vitu ambavyo haviko katika mpango na mpangilio.
Mkuu nilishawaza kabla nahitaji kuongezea mawazo kwa ma GT
 
kama huna ujuzi wa kufuga basi usitumie pesa ya mkopo kwa majaribio ya ufugaji.
Mkuu wengi waliofanikiwa walijaribu,nimepata wazo nimeona si vby niokote mawazo yenu kuboresha zaidi wazo langu.
 
Ok sawa ila minakushauri ingia kwenye browser yako uta daunilodi vijarida vya ufugaji aina tofauti za kuku pdf soft copy.zipo nyingi tu.
 
Jambo la kwanza uwepo wewe karibu ili kuweza kufwatilia hadi mradi usimame. Hiyo kitu haitaki mtu mwenye haraka. Sio unakaa tabata mradi bagamoyo lazma upigwe.

Jambo la pili kama unafuga tafuta mbegu bora na itunze vizuri. Kama ni ngombe basi tafuta wa kutoa maziwa ya kutosha na mbegu ya kisasa kabisa. Pia tumia mbolea na ulime bustani. Ni rahisi kuuza bidhaa za maziwa na hizo mboga mboga kwa pamoja.

Tatu, fahamu vya kutosha kitu unachotaka kufanya na weka gharama za wataalamu. Pengine ikaongeza gharama kidogo lakini itakuepusha na gharama kubwa baadae ikiwa kuna jambo utakosea. Kama ni kilimo pima udongo na pata ushauri zao gani linafaa na kwa namna gani utafaidika.
 
Ushauri mzuri kabisa huu.
 
Nimepokea ushauri wako mkuu nitaufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom