USHAURI: Nimeyakimbilia maisha naenda kuumbuka!

Niambie Tu

Senior Member
May 29, 2022
162
272
Habari

Mimi ni kijana mwenye miaka 27 mhitimu wa chuo, nimebahatika kufanya kazi sehemu mbalimbali na pia nimewahi kufanya biashara tofauti tofauti, japo sijawahi kukaa kwa muda mrefu katika biashara.

Nimekuja hapa JF naombeni mawazo yenu.

Iko hivi, Kuna binti nilimpa ujauzito sikuona budi kumuacha wakati mimi niliyesababisha hivyo, nikaamua kuanza kuishi naye na kupeleka posa ukweni mahari itatolewa mbele. Kwa sasa nafanya kazi katika shirika moja ambapo mkataba wangu unaenda kuishia.

Napata changamoto kadhaa ambazo zimenifanya nije humu ndani, sijanikiwa kufanya akiba yoyote hadi sasa. Napata lawama nyingi sana kutoka kwa ndugu, kwa maelezo yao binafsi nimewahi kuishi na mwanamke.

Huyu binti nilimfungulia duka-denge na ndiyo analofanya hadi leo, japo halikui, muda mwingi naona hela natoa mfukoni mwangu.

Hivyo naombeni ushauri wana JF maana naona kwenda kuumbuka. Kiumbe kinapokuja pasipo na maandalizi ya kimaisha, uwezo wa yeye kwenda kujifungua hiyo hela ninayo, mimi ninachoumiza kichwa nitawezaje kuishi na mwanamke na familia ilihali sina kazi kwa sasa.

Kuna muda namchukia na kumuongelea vibaya hadi najisikia vibaya. Nilikuwa nasali ila nimeacha. Nayaogopa maisha ya mbele yangu.
 
Kusema kweli, sisi tutajaribu kushauri ila maamuzi ya mwisho ni wewe na binti.

Kwa mtazamo, ni tamaa za kimwili ndio ziliosababisha umpe mimba na mihemko ndio iliopelekea kupeleka posa, ila sahivi unaona mapenzi hamna. Kwamba uyo binti we ilitakiwa upige na kutembea we umeweka kambi. Ukimuoa utamnyanyasa na utajinyanyasa na ukimuacha Anakua single maza.

Cha kufanya:
1. Kaa na binti, kikao kirefu muongelee muhafaka wenu. If possible akakae kwa wazazi wake wewe uwe unahudumia mimba.

2. Huyo demu inaelekea haumpendi, kwa sasa sababu sahivi anauza genge hayupo soft soft kama zamani. Na wewe ndio uliomuweka ivo. Kwahiyo bro, mara moja unamuambia chukua hii 20 kaweke fresh nywele, shika ten kanunue gauni, etc. Hao viumbe ukiachana nao wanaanza kupendeza ni nyoko.

3. Umri wenu mdogo sana. We una 20 yeye atakua 18 naona mna rush. Lakini sio mbaya kikubwa kama mnajielewa.

4. Mrudi kanisani. Kusali kutawafanya muwe closer.

5. Muongoze kwenye biashara. Kama ya genge kaishindwa muulize yeye anataka nini afu ndio umsaidie.

Kikubwa naona usimuache mtoto wa watu naona atapotea sana bwana, ebu muongoze uyo binti.
 
Sauto Sol walisema usitoe mimba, Mungu akileta mtoto analeta na sahani yake.
Sasa wewe kwa mwendo huu usishangae ukapata mapacha tena ukafungishwa na ndoa ya mkeka kabisaaa.
Utatembea uchi kwa kudata arif.
Manzi hajakukosea kwa unavoeleza, n wewe na wenge lako. Tuliza mshono, kaa chini tafuta chochote upambane ulee familia. Mbona wengine wanaweza? Hicho kidogo utakachopata mtakula wote maadam upendo upo.
Unaeza kumkimbia ndo ukakutana na maajabu ya firauni baada ya kustaajabu ya Musa
 
Unataka usaidiwe pesa ama?

Maana kama ni uzoefu wa kazi umeandika kwamba unao, hivyo tafuta kazi nyingine...

Kama ni uzoefu wa biashara tayari unao vile umefunguw genge, hivyo waweza jumuika na mkeo mtarajiwa mkaendesha genge kwa pamoja...
 
Back
Top Bottom