Ushauri: Nimepata milion 4, nifanye finishing au niongeze eneo kufanya ufugaji?

DAVID PALMER

JF-Expert Member
Jan 19, 2020
285
1,447
Wakuu. Habari zenu.

Katika pita pita zangu za kusaka pesa, nimekutana na milioni 4. Sasa nashindwa nifanye kipi kati ya hayo mawili.

Mi naishi Madale kwenye kibanda changu vyumba wiwili na sebule. Nimehamia nyumba haina finishing bado. Si marumaru, si plaster, na sakafu ni rough floor. So nawaza hii milioni 4 nifanyie finishing.

Au wazo jingine ni hili. Hapa jirani ninae pakana nae anataka kuniuzia eneo lake 2m. Nawaza ninunue, then nijenge banda la kuku, nianze ufugaji wa kuku kienyeji. Then wife atakuwa anasimamia na kuhudumia. Me nikiwa naendelea kwenda job.

Hii milion4 siitegemei kwa ajili ya kula.. maswala ya kula na maisha mengine me ni mfanyakazi nalipwa kila mwezi.
 
Chukua eneo mkuu then fuga kuku wa nyama na wakienyeji ikiwezekana na weka na kuku wa mayai kikubwa pesa mkuu
 
Nunua eneo, halafu helabinayobaki, nunua tiles, then anza kufuga hela za finishing.
 
Chukua kiwanja
Au Kama eneo ulilopo ni kubwa nalipo barabarani Jenga chumba kimoja Cha duka kwa m2 hizo m2 nyingine jaza vitu
Sio barabarani. So hakuna uwezekano wa kuweka duka.

Naona wadau wote mmeshauri nichukue eneo.

Basi naungana na mawazo yenu. Na nashukuru sana.

Nitaleta mrejesho soon.
 
Nunua eneo kwa ajili ya matumizi ya baadae hata kama usipofuga kuku litatumika kwa kazi nyingine.

Lakini ukitaka kuanza hiyo biashara ya kufuga kuku hakikisha kuna ukuta wa fensi,vinginevyo utakuwa unawafugia watu baadae watu wanakuja kujichukulia.

Huko madale napajua kuna vibaka sana.
 
Wakuu. Habari zenu.

Katika pita pita zangu za kusaka pesa, nimekutana na milioni 4. Sasa nashindwa nifanye kipi kati ya hayo mawili.

Mi naishi Madale kwenye kibanda changu vyumba wiwili na sebule. Nimehamia nyumba haina finishing bado. Si marumaru, si plaster, na sakafu ni rough floor. So nawaza hii milioni 4 nifanyie finishing.

Au wazo jingine ni hili. Hapa jirani ninae pakana nae anataka kuniuzia eneo lake 2m. Nawaza ninunue, then nijenge banda la kuku, nianze ufugaji wa kuku kienyeji. Then wife atakuwa anasimamia na kuhudumia. Me nikiwa naendelea kwenda job.

Hii milion4 siitegemei kwa ajili ya kula.. maswala ya kula na maisha mengine me ni mfanyakazi nalipwa kila mwezi.
Hiyo pesa ni ndogo sana, na maisha ni mafupi sana. Nakushauri usinunue hilo eneo, badala yake kaweke heshima baa
 
Ulipo Jenga ulitumia muda upi mpaka ukamaliza pasipo finishing? Ukipata jibu naimani hiyo 4m hutachezea. Kuna kesho utajuaje Kama huta nunua eneo lenye mgogoro? Malizia nyumba ndugu yajayo yatapendeza.
 
Japokuwa hakuna mrejesho, naomba kikazia eneo ni muhimu given kama halina mgogoro
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom