Ushauri: Nimemkuta mume wangu na binti wa jirani nyumbani kwangu

Mwalimu S

Member
Sep 20, 2015
41
33
Naomba msaada wako nifanye nini?

Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu anaangalia TV.

Sikufika mbali gari ghafla likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu anisaidie.Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa jirani yetu.

Nilimkabili mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo.

Je hii ni sawa?

Nifanye nini?

Naomba ushauri
 
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako,
kitu
ambacho nimekiona mara moja ni hili
tatizo la
gari kuzimika ghafla. Kwanini
uendeshe gari na
baada ya muda mfupi lizime? Hapa
kuna
matatizo kadha wa kadha ambayo
yanaweza
kuwa chanzo. Inawezekana plag
mbovu au uchafu
umeingia kwenye mrija unaopeleka
mafuta
kwenye injin. Au pengine ni tatizo la
umeme, au
fuel pump, ulicheki kama petroli ipo?
Ikiwezekana
waone mafundi warekebishe hivyo
nilivyovitaja.
Nategemea ushauri huo utakusaidia
mwanangu
 
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako,
kitu
ambacho nimekiona mara moja ni hili
tatizo la
gari kuzimika ghafla. Kwanini
uendeshe gari na
baada ya muda mfupi lizime? Hapa
kuna
matatizo kadha wa kadha ambayo
yanaweza
kuwa chanzo. Inawezekana plag
mbovu au uchafu
umeingia kwenye mrija unaopeleka
mafuta
kwenye injin. Au pengine ni tatizo la
umeme, au
fuel pump, ulicheki kama petroli ipo?
Ikiwezekana
waone mafundi warekebishe hivyo
nilivyovitaja.
Nategemea ushauri huo utakusaidia
mwanangu
Mkuu hueleweki, we c ndo umepost mada sasa mambo ya ufundi garage yametokea wapi,.??? mmmh ebu ngoja waje wajuvi,.
 
Thread Hizi Zipo Nyingi Sana Humu Na Zimejadiliwa Sana Nadhani Watu Huzileta Kwa Style Mpya
 
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako,
kitu
ambacho nimekiona mara moja ni hili
tatizo la
gari kuzimika ghafla. Kwanini
uendeshe gari na
baada ya muda mfupi lizime? Hapa
kuna
matatizo kadha wa kadha ambayo
yanaweza
kuwa chanzo. Inawezekana plag
mbovu au uchafu
umeingia kwenye mrija unaopeleka
mafuta
kwenye injin. Au pengine ni tatizo la
umeme, au
fuel pump, ulicheki kama petroli ipo?
Ikiwezekana
waone mafundi warekebishe hivyo
nilivyovitaja.
Nategemea ushauri huo utakusaidia
mwanangu
Unajishauri mwenyewe. Hivi kwani lazima uanzishe uzi jmn?
 
Babu zetu waalikua wakirudi safari lazima wapumzike sehemu na wazee wenzao maeneo ya kijijini hapo hapo alafu wanatanguliza fimbo na koti home kupitia wajukuu au watoto wa mtaani pale ili bibi kama ana jambo lake ajue mtabe karudi sio kwa kua ni wajinga hapana walijua hawana ubavu wa kuwaacha bibi zetu.
Kuomba ushauri hapa inaonyesha hauna ubavu wa kumuacha mumeo ivyo kausha tu siku ukiwa na ubavu wa kumtema basi mteme.
 
aise mm nimeshindwa kushangaa hii story kama vipi fanya chochote unachoweza mdau alafu tuletee mrejesho ukimaliza
 
Back
Top Bottom