Ushauri: Nilipita mpakani bila kugongewa Muhuri wa kuingia wakati nikirudi Tanzania

M-FINANCE

Senior Member
Aug 19, 2017
107
139
Hello waungwana nina jambo moja linanisumbua akili. Mwaka jana nilipata kwenda kutembea Mombasa Kenya, nikapita mpakani kwa kugongewa muhuri wa EXIT TANZANIA na ENTRY KENYA

Kwa bahati mbaya nikamissplace pasport yangu nikiwa Kenya ikabidi sasa nitafte mbinu ya kuvuka kurudi Tanzania kwa njia ya uchochoro nikiwa na akili kwamba nikifika hapa Dar nitafte passport nyingine, ila kwa bahati nzuri kule Kenya nilipoipotezea passport ikapatikana wakanitumia kwa basi

Swali je nikitaka kutoka Tanzania maana nina safari ya Malawi sitaulizwa kwamba mbona haioneshi entry Tanzania?

Wazoefu naomba mbinu kama hawaulizi chochote hapo nakausha najipanga tu folen border kwenda immiigration office

UPDATE
Nimeshalimaliza Tatizo

Mrejesho: Nimesovu tatizo la Kupita mpakani bila kugongewa muhuri wa EXIT KENYA - ENTRY Tanzania - JamiiForums
 
Rudi Kenya kupitia izo izo njia cha vichochoroni alaf ukishainingia uko ndo uende border Sasa ufanye kama ndo unarudi Tanzania wakugongee iyo mihuri

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
nilipaswa kutoka tarehe 11/10 sasa hivi huoni miezi ilokatika watasema nimeoverstay sana kwao mkuu? nasema nikienda kugonga exit muda huu
 
Ulifanya kosa ungeenda ubalozi Nairobi wakakupa ile pasi ya one way....lakin sio ishu nenda kavuke pale sirari n rahisi kuingia kwa njia za uchochoro coz boda ziko mbali mbali ya ke n tz so pita nenda kagonge haina problem mambo ya overstay eastafrica hayafatiliwi sana sidhan kama unaeza ulizwa tena vuka usiku
 
Ulifanya kosa ungeenda ubalozi Nairobi wakakupa ile pasi ya one way....lakin sio ishu nenda kavuke pale sirari n rahisi kuingia kwa njia za uchochoro coz boda ziko mbali mbali ya ke n tz so pita nenda kagonge haina problem mambo ya overstay eastafrica hayafatiliwi sana sidhan kama unaeza ulizwa tena vuka usiku
mkuu kwani hiyo ya one way nikienda mpakani nikasema kwamba sia nimeisahau itakuwaje, yaan nikapretend nilipita vema mpakani
 
Mkuu umejiingiza kwenye mgogoro wa kimataifa ambao mara nyingi wanakuingiza kwenye kundi la waharifu na ni vigumu sana kuwasomesha wakaelewa zaidi ya kukupa adhabu ya kutotembelea Kenya kwa miaka mitano au kwa Tanzania kutokukupa ruhusa ya kutoka nje ya nchi. Maelezo zaidi utayasikia kwao wenyewe.

Ni hivi; Kwa kuwa uliingia kwa njia halali na kugongewa, ina maana kuwa bado uko Kenya kwa mujibu wa taarifa za uhamiaji Kenya. kitendo cha kurudi kupitia njia za panya, kina tafrisi pana kiusalama kwa pande zote mbili, hivyo huwezi kujitetea vyovyote zaidi ya kukiri kuwa wewe ni mharifu.

Kwa upande wa Tanzania, nadhani kuna taarifa ulizotoa kabla hujapata pasi yako, na ndiyo hizo hizo zinazotumika kukupa pasi mpya, Kwenda kutengeneza pasi mpya kwa taarifa za kupikwa pia ni uharifu kwa kuwa unaenda kutoa taarifa za uongo. Ukisema ulipoteza pasi ukiwa Kenya, linakuja swali ulirudi kwa njia gani tena bila pasi wakati ungeweza kutoa taarifa za upotevu ukiwa Kenya na pengine kuomba msaada kwenye ubalozi wetu Kenya.

Ufumbuzi wake hauwezi kuwa rahisi kama unavyofikiria na hasa kwa sasa ambapo uhamiaji kwa upande wetu na Kenya pia wameimarika sana katika utendaji wao kuliko wakati mwingine wowote. Unachoweza kufanya ni kwenda uhamiaji kuwaeleza ukweli nini kilitokea ili walibebe tatizo lako na kukutetea kwa uhamiaji ya Kenya, jambo ambalo nina hakika hawawezi kufanya.

Kila la kheri!.
 
Back
Top Bottom