Salaam wana JF,
Kama mada inavyodokeza, mimi niliwahi kuajiriwa serikalini kama mwalimu wa secondary kwa muda wa miaka minne. Baada ya hapo niliomba ruhusa ya kwenda masomoni kujiendeleza. Mara baada ya kufika chuoni, niliamua kubadili kozi na kusoma fani niliyokuwa naipenda hapo awali kwani nilishindwa kuisoma kutokana na changamoto za maisha ikiwemo kukosa ada. Kozi yenyewe ni ya miaka minne.
Mwaka mmoja baadae, nilitakiwa kuwasilisha ripoti kazini ila sikufanya hivyo kwani sikuwa nasomea education. Kila likizo nilikwepa kurudi kituoni kwa sababu mbalimbali. Nikiwa chuo mwaka wa mwisho(wa nne), likapita fagio la Magufuli mshahara ukasimama. Nilihesabika kama mtoro kazini.
Kwasasa nakaribia kuhitimu elimu yangu, na nipo katika mchakato wa kujiajiri na changamoto ni lukuki. Nikakumbuka nilipokuwa kazini nilikuwa mwanachama wa mifuko kadhaa ikiwepo PSPF na CWT na nilikuwa nachangia wastani wa 25,000 kwa mwezi kila mfuko kipindi nasitishiwa mshahara.
Naombeni ushauri katika haya na mengineyo:
1.Naweza kupata stahiki zangu kwa kipindi nilichodumu kazini?
2.Nawezarudi kazini ili hali sikusomea nilichoombea ruhusa?
3.Ikitokea nafasi nyingine ya kuajiriwa serikalini kupitia hii kozi mpya bila tatizo?
4. Ushauri wa ziada wa nini nifanye kuhusu hili.
Ahsanteni.