Ushauri: Nifanye nini ili kipato changu kinitosheleze kwa mwezi

Jr. Gong Mira

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
1,279
1,295
Habari wakuu.

Natumai mpo salama. Mimi ni kijana msharaha wangu wa mwezi 350,000/= kwa mwezi.

Nina mke na mtoto mmoja ila naona maisha ni magumu mno kipato changu cha mwezi hakinitoshelezi hata kidogo ndani ya wiki mbili tu sina hela tena.

Naomba ushauri nifanye nini kwa kipato hicho angalau tarehe zikutane.

Ahsnte.
 
Jitahidi ukipata pesa tuu mahitaji yoote ya muhimu nunua kwa jumla....itasaidia kusave sent kidogo sambamba na kumuelewesha bibie lengo la kufanya hivyo ili awe makini kwny matumizi ya hivyo vitu.

Pia tafuta namna ya kumuwezesha wife apate kujishughulisha japo kupitia biashara ndogondogo itasaidia kiasi flani kusukuma gurudumu. Pia kama una kamuda japo kadogo unaweza kubuni njia ya kujiongezea kipato kupitia muda huu hata kama utashirikiana na mkeo katika shughuli hiyo.
 
Bana matumizi kwa sasa ila sio suluhisho la kudumu, anza kujifunza biashara itakayokupa mzunguko mkubwa, au tafuta kazi sehemu yenye mshara mkubwa, ila usiache uliyonayo kwa sasa, au Jifunzi ujuzi ambao una soko na utakupa kipato kikubwa. Usiongeze Mtoto mwingine na usitoe pesa kwa watu wengine.
 
Mimi ni kijana msharaha wangu wa mwezi 350,000/= kwa mwezi.
  • Tenga TZS. 50,000 kama mtaji wa biashara katika mshahara mmojawapo.
  • Mpatie wife, baada ya kuwa mmejadiliana kwa kina na mwambie aangalie ni biashara ipi itafaa na aanzishe hiyo biashara kulingana na mazingira mnayoishi, ili kipato cha biashara kisaidie katika kujikimu.

Baadhi ya biashara ambazo wamama huzifanya kwa ufanisi na zina kipato kizuri iwapo atakuwa na wateja ni kama:-

#1. Kukaanga chapati/ maandazi/ Half cake - na kuuzia hapo hapo nyumbani, ni swala la kuweka stuli na deli/ Container ambayo ni transparent, Kauli na Usafi ni kitu muhimu katika hii biashara.

#2. Uuzaji wa ice cream - Anachuukuwa kwa bei ya jumla, anaweka kwenye friji na kuuuza reja reja, - Hii inalipa sana kama unaishi jirani na shule au kama kuna njia ya kuelekea shuleni, wateja wakubwa ni wanafunzi na watoto.

#3. Miogo ya kukaanga

#4. Uuuzaji wa vitu vya matumizi ya jikoni - Mboga mboga, Nyanya, Vitunguu etl. - Unamtengenezea kibanda/meza/genge hapo hapo nyumbani na takuwa akiuza

#5. wengine wataongezea
 
Pole sana Mkuu,

Udogo wa kipato chako inaweza hata isiwe tatizo la kipato kutotosheleza ila kutopangilia matumizi ya kipato chako...

Ni Rahisi sana kupoteza kipato katika mahitaji yasiyo na msingi na ulazima endapo hutopangilia kipato chako vizuri...

Mkuu kama huna madeni ambayo yanakulazimu kutoa sehemu kubwa ya kipato chako... Kwa ukubwa wa Familia yako, kipato chako ukikipangilia vizuri kimahesabu kinatosha vizuri kabisa na akiba inabaki kukusanya mtaji tosha kabisa kuanzisha biashara kujiongezea kipato...

Fuata hatua zifuatazo kupangilia kipato chako...

Hatua ya kwanza, ainisha na kufanya tathmini ya mahitaji yote ambayo yamekuwa yakikugharimu mshahara wote... Umezungumza kuwa hiyo 350,000 haichukui wiki 2, so hapa ainisha hayo mahitaji yote yanayochukua mshahara wako wote ndani ya wiki 2...

Hatua ya pili, chambua mahitaji yote ya msingi na lazima kutoka hatua ya kwanza... Hapa tunatenga mchele na chuya... Jaribu kuangalia mahitaji ambayo umekuwa ukiyaingia lakini kimsingi hayakuongezei chochote wala kukupunguzia chochote kisha yaondoe kwenye orodha ya mahitaj kama pombe, make up, pampers, nursery... Baki tu na mahitaji ya msingi na lazima...

Hatua ya tatu, katika mahitaji ya lazima, fanya tathmini familia yako inahitaji mahitaji ya lazima kiasi gani na gharama yake kwa siku... Mfano kwa siku familia yako inahitaji mchele kilo ngapi, sukari kiasi gani, chumvi, mboga, umeme, usafiri n.k.. Lengo ni kujua gharama ya kuendesha familia yako kwa siku kwa bei ya rejareja.

Hatua ya nne, Fanya tathmini hayo mahitaji ya lazima ya familia kwa mwezi, kisha jaribu kuangalia namna ya kupunguza gharama ya kununua hayo mahitaji kwa kutumia njia kama kununua kwa bei ya jumla, fanya tafiti mahali unaweza nunua kwa bei nafuu, kuomba punguzo la bei, zima vifaa vinavyofuja umeme, okoa nauli mahali pa kwenda kwa mguu n.k..

Hatua ya tano, Tengeneza bajeti ya mwezi mzima, hapa Mkuu chukua ile tathmin ya siku ya uhitaji wa Familia yako na gharama zake kwa siku kisha zidisha mara 30... Hakikisha inakuwa katika bei ya punguzo Mfano umejua kwa siku familia yako inahitaji kilo 2 za mchele sawa na kilo 60 kwa mwezi.. Unaweka bei ya jumla ya kilo 60 sasa..

Hatua ya sita, nidhamu Mkuu, hakikisha huingii gharama nje na ulivyopanga...

Nb. Usisahau kutenga pesa ya dharura...

Mkuu kama utahitaji usaidizi zaidi wa namna ya kuandaa bajeti ili kudhibiti matumizi yako usisite kunicheki popote hata PM, nitapenda kukusaidia ili uondokane na stress zisizo na msingi. Karibu.
 
Nilivyosikia tu kuwa nchi iko uchumi wa kati nikajua watz wote ni middle income wanakula maisha isipokuwa mimi kumbe nawe upo! Pamoja sana ndugu twende kwa jpm akatupe mbinu za kutuwezesha kuingia uchumi wa kati maana tumebaki mimi na wewe tu nchi nzima wengine wote ni uchumi wa kati.
 
Ahsante sana mkuu ushauri naufata.
 
Nilivyosikia tu kuwa nchi iko uchumi wa kati nikajua watz wote ni middle income wanakula maisha isipokuwa mimi kumbe nawe upo! Pamoja sana ndugu twende kwa jpm akatupe mbinu za kutuwezesha kuingia uchumi wa kati maana tumebaki mimi na wewe tu nchi nzima wengine wote ni uchumi wa kati.
Hahahha ndo maisha
 
Back
Top Bottom