USHAURI: Niende kwenye ajira Serikalini au nisimimamie biashara za nyumbani?

Inategemea na hao wazazi wenyewe, maana wazazi wengi wa kiafrika huwa ni wakoloni sana, ila kama una flow nao vizuri basi simamia vya nyumbani...! Maana kupitia hivyo utatengeneza security ya vizazi vyenu, ila kama ni mbinafsi utakimbilia ajira yenye security yako tu, huku vizazi vyako vije kusota
 
Kama ndugu zako walikupa huo ushauri sasa unakuja kwetu kuomba ushauri wa nini wakati tayari una ndugu zako ,hayo mambo ya ndugu sisi hayatuhusu naomba ukamalizane na nduguzo ,hayo mambo yenu wana ndugu
 
Habari za asubuhi?

Nishaurini katika hili nimepata ajira Serikalini Upande wa afya clinical officer soon tunatakiwa kuripoti kazini .

Upande wa pili wazazi wanamiliki pharmacy 2 na maduka mawili ya jumla ya dawa na dispensary moja , wazazi hawataki niende kwenye ajira ya Serikalini wanataka nisimimamie biashara zao lakini ndugu wamenishauri niende kwenye ajira serikalini kwa sababu serikalini kuna security.

Nisaidieni ushauri mdogo wenu ktk hili .

Ktk familia tupo watoto 2 tu , mdogo wangu bado anasoma.umri nina miaka 24
Kasimamie biashara ya familia ingia kwa asilimia mia moja tena uweke mkakati wa kuikuza uzuri fani yako ni hiyo hiyo, ikiwa utaenda kuajiriwa usiende kwasababu ya ajira bali labda kama unataka kupata uzoefu zaidi wa kazi ili uwe mfanisi zaidi kwenye zahanati ya nyumbani.

Muhimu weka makubaliano na wazazi kwamba utajilipa mshahara kila mwezi sawa na ule ungepata serikalini. Kumbuka biashara hiyo una fursa ya kuikuza zaidi na hata wewe kurithisha wanao.

Ajira ni nzuri lakini kwa wasio na njia mbadala au labda kama ni nafasi kubwa sana.
 
Habari za asubuhi?

Nishaurini katika hili nimepata ajira Serikalini Upande wa afya clinical officer soon tunatakiwa kuripoti kazini .

Upande wa pili wazazi wanamiliki pharmacy 2 na maduka mawili ya jumla ya dawa na dispensary moja , wazazi hawataki niende kwenye ajira ya Serikalini wanataka nisimimamie biashara zao lakini ndugu wamenishauri niende kwenye ajira serikalini kwa sababu serikalini kuna security.

Nisaidieni ushauri mdogo wenu ktk hili .

Ktk familia tupo watoto 2 tu , mdogo wangu bado anasoma.umri nina miaka 24
Mtoto wa kiume ni misimamo naona umekalia ndugu ndugu... mara ndugu waliniambia niombe mara wananiambia niende... sasa hao ndugu ndio wana uchungu na maisha yako kuzidi Mama yako mzazi na baba yako? hopeless kabisa
 
Huo mfumo wa biashara za nyumbani wanauweza wahindi ila kwetu kibongo bongo ni ngumu ukute ukoo mzima unawategemea nyie. So ni bora chako kidogo so mm nashauri uende kazini.
 
Back
Top Bottom