Ushauri: Nichukue gari ipi kati ya hizi?

WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,415
1,378
Nawasalimu wakuu kwa jina la nguvu na uchakalikaji wetu.

Baada ya kupitia threads nyingi hapa na kujifunza mengi kuhusu magari nami natupia uzi hapa ili kupata ushauri.

Kiukweli mi mgeni sana wa magari hata kuendesha si mtaalam sana ila naweza sema sijakaa na gari tu nimesota kwa miaka 8 nasuhua bench kutimiza malengo mengine (nyumba ya wazazi kijijini nimemaliza na nyumba yangu mjini nimemaliza) nadhani mnajua ile hustle ya kuwa kichwa cha familia na umetoka kwenye umasikini wa kutupwa na baada ya kusoma ukoo mzima unakuangalia...😀😀😀😀.

Mwaka huu nimejipinda nami nivute gari ya maana kidogo kwa matumizi ya familia na route ndefu km kwenda kijijini huko... (Naishi kanda ya kaskazini kwa rafiki zangu akina Mangi huku ila mimi ni mnyantuzu(Msukuma) kutoka kanda ya ziwa huko😀😀😀

Bajeti yangu ya gari inaanzia 30M-40M hivi, sasa ushauri nichague gari gani kati ya hizi?
1.Toyota
-RAV 4 New Model
-Lenus RX
-Harrier (Hapana nakubali ushauri)
-Vanguard (Hapana nakubali ushauri)

2.Nissan
-Muranno
-QSHANAI
-Dualis (hapana ila nakubali ushauri)
-X-Trail (hapana ila nakubali ushauri

3. SUZUKI
-Escudo Grand (Seat 7)
-Escudo (Seat 5)

Bajeti yangu inaangukia kwenye mid/lower SUV cars.

Kingine nataka kuagiza kutoka Japan (kulingana na maoni ya humu) ilq kuna jamaa yangu nimemshurikisha akasema bora nichukue yard but mimi nasita sababu ya kupata uzoefu wa yard kupitia jukwaa hili.

Pia naukiza ni kampuni gani nzuri kuagiza kati ya hizi
1.Be forwarded
2.SBT Japan
3.Enhance Japan

Natanguliza shukrani wa ushauri wenu na asanteni
 
Toyota RAV4 new model, hakika uko juu
1627613780514.png


Ushuru peke yake ni 44.3 million.
Nimekuwekea hapo link YENYE matokeo ya ushuru unaotakiwa kulipwa
 
Mkuu, Hongera sana.

.Kampuni ya uhakika na yenye machaguo mengi ni Be Foward.

Katika Machaguo mengi, ubovu wa barabara za vijijini na ukubwa wa familia basi opt for Vanguard.

Ni gari nzuri na yenye nafasi ya kutosha. Ni nzuri sana kuliko Harrier na mdogo wake Rav4.

Katika gari za Nissan hapo juu, achana nazo zote isipokuwa X-Trail. The rest is mostly for women (I'm sorry to say). Mwanaume aliyekula age kama wewe, gari ndogo ndogo kama hizo ni za kuhonga tu au kumnunulia mama watoto.

Lakini kwa bajeti yako, kama mwanaume usiyeogopa majukumu (hata ya kuhudumia gari [mafuta na service]) chukua vitu vya wazungu. Nenda na x5 au VW Touareg. Japo hazikuwa katika wishlist yako.

Be a gentleman.
 
Mtoa mada ina maana umejenga nyumba zote hizo ukiwa unakwea bodaboda? Kuna kama ka chai flani hivi. Unless hizo nyumba ziwe unga unga mwana ila mtu anayejenga nyumba mbili za kawaida hawezi kosa hata IST maana bei yake ni kama Tiles za nyumba moja tu
 
Mtoa mada ina maana umejenga nyumba zote hizo ukiwa unakwea bodaboda? Kuna kama ka chai flani hivi. Unless hizo nyumba ziwe unga unga mwana ila mtu anayejenga nyumba mbili za kawaida hawezi kosa hata IST maana bei yake ni kama Tiles za nyumba moja tu
Mkuu kila mtu anakipaumbele chake,Kaka yangu ananyumba tatu ila anaendakazini na bajaji na hajui kuendesha gari na hana mpango wa kujifunza.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom