Ushauri: Ni bora kuwa na mkono mfupi unaofanya kazi kwa ufanisi

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,521
2,109
Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukiaminishwa na wengi wetu tunaamini kuwa kuna taasisi moja ina mkono mrefu sana na unaweza fika popote. Lakini cha kushangaza kila kwenye uhitaji wa ule mkono mrefu unakuwa unashindwa kufika kule kunakohitajika. Bila shaka unaweza kuwa ni mkono mrefu kweli lakini kushindwa huku kufika kule kunakohitajika ni kuamua tu au umeoza na kumelemaa kwa pamoja. Hivyo utakuwa hauna tofauti na zile taasisi zisizo na mkono kabisa lakini zinafanya kazi zake kwa uhadilifu.

Hivyo ni borakuwa na mkono mfupi unaofanya kazi kwa ufanisi hata kwa kutumia visaidizi kuweza kufika kule unakohitajka. Tumechoka kusikia hii hadithi na maneno ya mkono mrefu huku ni dhahili kuwa ni dhaifu na unashindwa hata kufika hata sehemu za mwili wake. Ni nini hasa haja ya kuwa kuwa na mkono mrefu dhaifu, uliolemaa na kuoza kwa pamoja? Hii ni falsfa wenye kutafakari watanielewa.
 
Back
Top Bottom