Ushauri, natarajia kuanza biashara ya vitu vya jumla vya dukani kutokea Dar es Salaam kuja mikoani

Mowwo

JF-Expert Member
Aug 15, 2015
321
227
Nawasalimu wote.

Mimi ni kijana mjasiriamali ninaetarajia kufanya biashara ya jumla ya vitu vya dukani(Arusha&Moshi) lakini ningependa kupata mawazo na ushauri namna ya kuagiza vitu hivyo kutokea Dar kuja mkoani.

Uzoefu wa biashara hii ningeupata kutoka kwenu ningeshukuru pia. Vitu ninavyotarajia kuagiza ili niuze kwa jumla ni kama vifuatavyo;

-Vitambaa
-Soksi
-Madaftari
-Rula,Penseli, Kalamu,vichongeo
-Miswaki
-Super glue
-Toothpick
-Pipi na biskuti za aina zote
-Dawa za mbu
-Kufuli
-Rangi za viatu nk

Changamoto ni kwasababu naanza kwahiyo ningependa kufahamu wale wanaoagiza Dsm wanaagiza wapi, changamoto zake? Umuhimu ni kuagiza au kufuata? Na faida zake.

Natanguliza shukrani🙏🙏

images.jpeg

 
Kwanza funga safari mwenyewe, fika kwa wauzaji wenyewe, usitumie madalali kufahamu mahali wanapouza kwa bei za jumla sababu wataongeza garama ya bidhaa, ukija sokoni unapishana na wafanyabiashara wengine, hakikisha unaenda mwenyewe safari ya mara moja, baadae unakua unawatumia tu hela kwenye akaunti zao wao wanakupelekea mizigo yako kwenye makampuni yanayosafirisha mizigo mahali ulipo.
 
Hongera kwa wazo zuri, fanya utafiti eneo lako, wape tip wasaidizi maduka shindani, wakupe ABC, na contact wanapotoa mzigo,utajua pia makisio mtaji,anzia hapo kisha funga safari ana kwa ana.
 
Njoo Dar maeneo ya Kitumbini nenda ktk Duka la Mohamed Zakaria kila unachokihitaji utakipata kwani wafanyabiasha wengi wa Jumla ndiko wanakonunulia bidhaa zao.
Sio mbali ukishatoka hapo Mnazi Mmoja NBC Banki
Ahsante sana nami umenisaidia maana naagiza vitu dar to mkoani lakn naagiza kwa mtu sijui ana supermarket yule Bei yake imechangamka
 
Ahsante sana nami umenisaidia maana naagiza vitu dar to mkoani lakn naagiza kwa mtu sijui ana supermarket yule Bei yake imechangamka
Lakini unapata faida? Hapo ukisoma somo la kumuepuka mtu wa kati utatoboa
 
Njoo Dar maeneo ya Kitumbini nenda katika Duka la Mohamed Zakaria kila unachokihitaji utakipata kwani wafanyabiasha wengi wa Jumla ndiko wanakonunulia bidhaa zao.

Sio mbali ukishatoka hapo Mnazi Mmoja NBC Banki
Finally nipo Dar kwaajili ya mzigo. Ndo naenda kwenye hilo duka mkuu
 
Njoo Dar maeneo ya Kitumbini nenda katika Duka la Mohamed Zakaria kila unachokihitaji utakipata kwani wafanyabiasha wengi wa Jumla ndiko wanakonunulia bidhaa zao.

Sio mbali ukishatoka hapo Mnazi Mmoja NBC Banki
Yupo Kwa upande upi huyu jamaa
 
Leta mrejesho sasa wa baadhi ya bei za vitu, mfn miswaki kwa carton anauzaje, kufuli ndogo ama kubwa anauzaje, wembe carton anauzaje n.k . TAMBUA ULIOMBA WAUNGWANA WAKAKUONESHA SASA NA WEWE KUWA BINADAM MWEMA LETA MREJESHO HAPA.
 
Utofauti wa Bei ukoje ukilinganisha na Bei za super dealers kama mama mtei na mama neema?
Inategemea na baadh ya vitu mkuu. Mimi nimebase zaidi vitu vya dukani lkn kimachinga ila wale wapo general. Mpaka vitu vya kula km mafuta...nk wanauza.
Kwa vitu vya dukani Dsm bei iko chini
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom