Ushauri: Nataka nitoke nje ya Tanzania kiutafutaji, ni nchi gani unaweza nishauri kwenda?

Mangole Valles Michael

Senior Member
May 30, 2021
100
250
Wakuu habarini za leo?

Nikiwa kama muumini ninae amini maisha ni popote, Leo nimeleta Uzi huu nikiwa na lengo la kupata mwongozo kwa walio nitangulia kutoka nje ya Tanzania au walio na uzoefu wa nchi zingine barani Africa au nje ya Africa.

Kwanza kutoka nje ya Tanzania kwenda ku-make life abroad ni ndoto yangu tangu nikiwa mtoto na kwasasa naona umri wa kuiishi ndoto yangu ni Sasa.

Hivyo basi naombeni mwongozo ni nchi gani ambayo unaweza nishauri kwenda kwa ajili ya utafutaji wa maisha kulingana na fursa za nchi husika? Pamoja na mwongozo wa kufika huko.

Mimi kama Mimi nchi ambazo nimekua nikiwaza kwenda nchi ambazo ni visiwa kama sheli sheli (Seychelles) Mauritius n.k
-kwa south Africa sipapi kipaumbele Sana may be Botswana na kwingine.

Kwa wale mtakao shauri kua Tanzania kuna fursa nyingi kuliko nje sikatai ni kweli zipo ila kama una mchongo nipatie nipige, kama na wewe una fursa za mdomoni basi naomba utulie.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom